Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Kijiji cha kata ya Kisumu ni kilio baada ya mwanamke mmoja kuwaua watoto watatu wa mkewe mwenzie kabla ya yeye pia ujiua. Majirani wanasema mwanamke aliyekuwa na ugomvi na mshirika wake aliwafunga watoto nyumbani mwao katika kijiji cha dago na kuwaua.
Citizen
===========================================
Mwanamke mmoja katika kijiji cha Nyahera Kaunti ya Kisumu nchini Kenya, amewaua watoto watatu wa mke mwenzie, na kisha mwenyewe kujinyonga.
Tukio hilo limeelezwa kwamba mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Jacinta Otieno, aliwaita watoto hao wanne kwenda kunywa uji nyumbani kwake, na ndipo alipoanza kuwacharanga na mapanga mpaka kuwaua na kisha mwenyewe kujinyonga, huku mtoto mmoja akinusurika baada ya kukataa kwenda kunywa uji.
Jacinta alifanya tukio hilo baada ya mke mwenzie kwenda kanisani na kuwaacha watoto peke yao nyumbani ambako wanaishi jirani, huku mume wao akiishi jijini Nairobi na watoto wake wengine.
Kwa mujibu wa majirani, wawili hao wameelezwa kuwa hawakuwa na maelewano mazuri kutokana na wivu kwa mume wao, na kwamba Jacinta alishajaribu kutaka kujiua wiki moja iliyopita.
Watoto hao waliouawa walikuwa na umri wa miaka 7, 4 na 2, walikuwa wa mke mwenzie Hellen Otieno.
Dar24