Mwanamke fahamu mambo haya kabla hujawa mchepuko wa mume wa mtu

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
1,497
Reaction score
2,681
Ukubali ukatae huu ndio ukweli na utabaki kuwa ukweli,

1) Ukiwa umetoka kula bata na mume wa mtu,
Wewe utaenda nyumbani kwenu lakini yeye atarudi nyumbani ambapo anaishi na familia yake.

2) Kumbuka kua mkimaliza ku sex nae hutupa condom ambazo mlitumia mbali zaidi,
Ili mke wake asifkirii chochote na anafanya hivo kwa hofu ili asivunje ndoa yake.

3) Akifika barabani hununua pipi ili asafishe harufu yako yote,
Hufanya hivyo Ili kuilinda ndoa yake isivunjike.

4) Mara nyingi wanaume wenye tabia kama hii,
Hujutia sana kufanya uhalifu huo wakati wakiendesha gari kuelekea majumbani kwao.

5) Kumbuka akimaliza ku sex nawewe lazima aende bafuni aoge vizuri,
Ili aondowe jasho lako chafu Ili akienda kwa familia yake awe msafi.

6) Wengi wao wakati wakiwa bafuni hujutia saaana,
Kwa kuona wamemaliza ku cheat na kusema kua,
Kamwe hawawezi kufanya kitendo kibaya kama hicho tena.

7) Waume wenye tabia kama hizi wanaporudi home,
Huwa kumbatia wake zao na kuanza kujali watoto muda ule.

8) Acha ni waambie kitu nyie wanawake,
Waume za watu huwatafuta nyie michepu,
Wakati akiwa na stress na mke wake kipenzi,
Lakini si kwamba anakupenda kweli hapana.

9) Ukiwa mchepuko wanaume hukuchukulia kama bidhaa za dukani,
Kwa sababu kuna ambazo zinagharama lakini ni used.

10) Atatumia gharama zote zote ili akupate,
Lakini si kwamba anakupenda weli hapana,
Yupo nawewe kwa tamaaa zake tuu za mwili,
Lakini akili na mapenzi ya dhati vipo kwa mkewe.

11) Watu hawawezi kukuheshimu ikiwa wewe unapendwa na mume wa mtu Nooo,
Na hiyo sio sifa nzuri katika jamii haijalishi wewe ni mzuri kiasi gani,
Hata kama ukiwa umeenda chuo cha Harvard,
Ukiwa na tabia hiyo watu watakuweka katika nafasi ambayo haustahili kuwepo dada angu.

12) Umehongwa zaidi ya milioni 10 na umempelekea mama yako milioni 2,
Mama yako anainua mikono kwa Mungu anaomba dua,
Eweeee Mungu wa Mbinguni naomba ummbariki mwanangu,
Apate zaidi hivi mama yako anafahamu sehemu ambapo umetoa hizo pesa,
Hajui kua umepewa kwa njia ya uzinifu wala hajui maskini ya Mungu,
Hiyo dua Huwa inageuka na kuwa laana kubwa kwako.

13) Tambua kua tofauti yako na malaya anaejiuza,
Ni vile yeye anatambulika na kila mtu tu basi,
Lakini wewe ni wakisiri siri tuu lakini wote ni malaya.

Dada yangu ambae bado hujaolewa hujachelewa,
Tambua thamani yako ili uwe na malengo wewe ni zaidi ya jinsi unavyojifkiria,
Acha kabisa tabia za kuwatafuta sugar Daddy,
Pesa zao haziwezi kukufkisha sehemu yoyote,
Kwa sababu zina nuksi, mikosi na laaana tuuupu,
Tambua thamani yako na umsubiri mwanaume ambaye ni sahihi kwako,
Wanaume wenzangu naomba tuwe tunawafunza dada zetu,
Heshima na thamani yao na pia tuwafunze wake zetu,
Jinsi yakuwashauri binti zetu ili wasiishi katika tamaa za wenye pesa,
Wewe mwanamke tambua Mungu hajakuumba ili uwe chanzo cha ndoa za watu kuvunjika,
Mwanamke acha tamaa ridhika na ulichonacho,
Tambua kua siku zote mwanaume mzinifu,
Na asie muheshimu mke wake hata wewe atakuafanyia hivyohivyo akikuoa.
 
Maelezo meeeengi, hebu michepuko watengwe kidogo

Kuna muda wanasaidia sana pale njia kuu inaposumbua
 
Bongo kwa kujadili nonesense issues kama michepuko na Simba/Yanga wako makini kweli kweli.
Hawajadili ni kwa nini umbali kutoka Ethiopia mpaka Arusha/Kilimanjaro ni KM 1,935.5
Na umbali kutoka Arusha/Kilimanjaro mpaka Rufiji(kwenye bwawa la kuzalisha umeme) ni KM 805.6 lakini kodi za walalahoi zinaenda kununu umeme Ethiopia badala ya kununua kutoka Rufiji ambapo tulishaambiwa kuwa umeme umezidin mpaka mitambo mingine imezimwa.
 
Comrade, ishi maisha yako. Na hao michepuko waache waishi maisha yao! Ok?
 
Kuna wanawake wengi leo wana maisha mazuri kwa kuwapa waume za watu. Jokate angekuwa ana bana asingefika hapo alipo. Tofauti ya wema na Jokate ni kuwa Jokate aliwapa wanaojielewa na alikuwa anatoa kimipango.
 
umeongea point sana!!!
 
One in a million
Sio one in a million tatizo mnakariri maisha, mimi ni mwanaume. Wanawake ninawashauri mjibane na mtoe kimipango. Zunguka huko serikalini, kuanzia sekta za juu mpaka wabunge wa viti maalumu wanawake wapo kwa sababu wametoa kimipango. Dini inahaharibu fikra zetu waafrika, ishu ni kujua tu mtu wa kumpa. Ukishajua jinsi ya kujua na kuwa na malengo na kutoa mbususu kutoboa easy sana. Nimetoa mfano wa jokate maana yeye hana historia ya kuwapa wavulana yeye ni wanaume tu. Kuanzia Hasheem Thabeet mpaka marehemu Mzee Mengi. Unadhani ukuu wa wilaya kapata bure bure. Amkeni wanawake ukiwa Jokate kamaliza UDBS ana viwanja vitatu. Huku kuna watu wanamaliza chuo na watoto.
 
So unawashauri wote wauze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…