Mwanamke huyu ana dhamira gani?

Status
Not open for further replies.

April26

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2020
Posts
1,405
Reaction score
2,147
Wakuu hili swali sijawauliza ninyi ila nimejiuliza mwenyewe sijapata jawabu mnaweza kunisadia.

Huyu ni mwanamke rafiki ake na mpenzi wangu wa zamani ,anajuwa nilivo kuwa na care rafiki yake sema tulikuja kuachana baada ya kuniingiza hasara kubwa kiuchumi na kifikra na ndo alikuwa mpenzi wa mwisho kuwa nae kabla sijahamia kwenye kunywa masanga kama kipozeo.

Last month aliniambia anahitaji nimtoe out tukaongee akidai ana issue kubwa ya kunambia, sikusita kwa sababu nilikuwa na mpunga wa kutosha si unajuwa mwisho wa mwezi tena.

Tulikaa sehemu tukapiga masanga baada ya kulewa akaanza kuniponda kwamba nimemwacha rafiki yake, mtu mzima nikawaza ina maana kaniita hizi lawama means hajui kama rafiki yake ndo alikuwa tatizo!

Iko mida ya saa 7 usiku akasema anahitaji akalale, nikwamwambi ngoja niite boda akupeleke akazinda anataka tuondoke nae nikasema sio tabu, tuko kwa boda ananambia haendi home kwake anataka nichukue chumba guest tukaongee maana jambo lenyewe hajanambia.

Nikamwambia poa. Wakuu hakuamini nimechukua room nikaoga akaoga tukalala kajiachia kama yupo na bwana wake mimi nikatupia suruali langu na mkanda juu mkao wa kusikia alichoniahidi, ukumbuke tulikuwa mtungi wote ila yeye alihelemewa sana.

Huwezi amini hadi asubuhi hatujalala maana nilivoona mizinguo nikahamia kuangalia TV hadi asubuhi, alibaki na mshangao hadi anaondoka.

Jana kanichek kwa phone tuonane nikamkatalia, katuma meseji kibao anadai nimkubalie wala X wangu hatajuwa.

Hapa nilipo najiuliza niumize au niendee kunywa pombe zangu zinazo nisaidia kuondoa genye ?

Mbona namuona kama na yeye ni tatizo au nifanyeje huyu mdada, kiukweli kaumbika na rangi ya mtume shape kama 8 japo hamzidi X wangu!

Niko njia panda ,baada ya kuwaza sana sahivi Niko nakunywa masanga hapa kwa mangi nikasema.niwashirikishe kidogo!

Nyongeza: baada ya matatizo na huyu X wangu ilibidi niuze gari langu maisha yakaendelea, Nina machungu mengi SIJUI LINI NITAPATA MWANAMKE WA KUNIELEWA moyo unaumia sana navoona bado nawindwa.

Ni hayo tu.
 
Katika wanaume wajinga unaongoza, mwanamke anakupelekesha na kukuamrisha namna hiyo, eti chukua chumba gest nikueleze jambo lenyewe na wewe unaenda kuchukua chumba, how old are you brother? Isije tukawa tunakulaumu kumbe wewe ni mvulana
 
Hapana mdogo wangu Mimi sio mjinga ,nilisona mchezo mbaya kumbuka huyu ni rafiki wa X wangu na mm akiniingiza hasara kubwa sana na had Leo huwa natafuta namna ya kulipiza alivonambia ana issue kubwa nikajuwa mpango wangu unaweza kuwa sawa kumbe anataka ngono na mm ngono nishagaacha nakunywa zangu mtungi unakata nye.....g...e nikihelemewa sana huwa nachukua tusiegandana.
 
Pole sana, ila inaleta utata kusema unaingia lodge na rafiki wa ex wako, kwa mazoea gani?
 
Pole sana, ila inaleta utata kusema unaingia lodge na rafiki wa ex wako, kwa mazoea gani?
Yani kuna back story kiasi niliwahi mwambia mission yangu sema sasa yeye kaja kivingine, ukiachilia mbali mission mm huwa nikitumua pombe sinaga hisia kabisa na mwanamke so nilikuwa naona kawaida.
 
Katika wanaume wajinga unaongoza, mwanamke anakupelekesha na kukuamrisha namna hiyo, eti chukua chumba gest nikueleze jambo lenyewe na wewe unaenda kuchukua chumba, how old are you brother? Isije tukawa tunakulaumu kumbe wewe ni mvulana
Likizo time ...shule zmefungwa
 
We jamaa naomna nitangulie na kusema "Lofa ww" πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ hebu acha ujinga japo kwa heshima yangu tu. Leo ita huyo mjane umpelekee moto wa tipa
 
Likizo time ...shule zmefungwa
Mkuu maamuzi niliyofanya sio ya kitoto ,nadhani kama wewe umepevuka kiakili utajua maana ya vita baridi.
 
Reactions: Lee
Mkuu maamuzi niliyofanya sio ya kitoto ,nadhani kama wewe umepevuka kiakili utajua maana ya vita baridi.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…