Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MWANAMKE INITIATIVES FOUNDATION (MIF) YANUFAISHA KIMASOMO WANAFUNZI 96 WALIOHITIMU
Mbunge wa Viti Maalum na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF), Mhe. Wanu Hafidh Ameir katika kuadhimisha Siku ya Vijana alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza ya Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Makunduchi tarehe 13/8/2024.
Mahafali ya kwanza ya Wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Makunduchi ilikuwa na Jumla ya wanafunzi 376 ambao wamehitimu kozi mbalimbali za muda mrefu na mfupi.
Akizungumza, Mhe. Wanu Hafidh Ameir amesema Kati ya Wanafunzi 376 waliohitimu katika Chuo cha Mafunzo ya Amali Makunduchi, Wanafunzi 96 walifadhiliwa masomo na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)
Aidha, Mhe. Wanu Hafidh Ameir amesema kuwa Taasisi ya MIF imekuwa ikitoa ufadhili kwa wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne na kushindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano katika vyuo vya amali.
Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ameongeza kuwa Taasisi ya MIF inaamini na itaendelea kuamini kuwa vijana ndio nguvu kazi muhimu kwa maendeleo endelevu ya Taifa lolote ulimwenguni, hivyo, MIF itaendelea kuweka nguvu kuwezesha vijana nchini.