Mzigua90
JF-Expert Member
- Sep 23, 2014
- 38,342
- 88,625
Unakuta mwanamke yuko on her 20's ila anavaa kama mwanamke wa 60's. Jijali, jiweke smart. Sio lazima utumie vitu vya gharama uonekane mzuri. Tumia resources ulizonazo kujiweka vizuri. Achana na kina sisi wavaa weaves/wigs kuna nyie wenye mnakata nywele. Kata nywele zako vizuri vaa nguo nzuri sio unakata nywele na unavaa masketi marefu hayaeleweki hata mke wa mchungaji anakuzidi kupendeza. And hivi vipodozi kama lipstick wanja mascara vipo kwa ajili yetu tuvitumie. Hamna mwanamke mbaya kama atajijali kwenye muonekano wake. Pendezeni jamani. Kuna wake za watu wakishaolewa tu wanajizeesha kwa kujiweka rough kama vibibi vya miaka 70. Jiweke mpya kwa mumeo kila siku. Kama alikupenda kwa kukuona umevaa Brazilian hair kwanini uache kuvaa ukiwa wife? Unapenda vitenge shona basi mshono ueleweke. Sio unashona hips 40 wakati unavaa 34 ukivaa unaonekana kama mfuko wa mashineni.
P.S. wanaume wapendezesheni/waacheni wake zenu wapendeze. Sio ukiomuoa unaanza masharti hutaki lipstick hutaki weaves wakati ulivyomfuata alikua anavifanya. Mnakataa kwa wake zenu ila michepuko mnawanunulia hata nywele ya 400k.