Mwanamke katoroka kwao, nifuate njia gani za kisheria?

Mwanamke katoroka kwao, nifuate njia gani za kisheria?

MGODOLO

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2020
Posts
209
Reaction score
174
Habari zenu Wana JF?

Kuna nyuzi kadhaa nilizowahi kuziandika hapa na nikapata shauri mbalimbali toka kwenu.

Mwanamke nilie zaa naye, ila tumechelewa kufunga ndoa kulingana na ukosefu wa mahari, Sasa mwanamke huyo kachoka kusubiri, kaja kwangu Siku ya jana asubuhi akiwa na nguo zake na mtoto wetu

Kwa muonekano ule, haikua na haja ya kumuuliza kwasababu alisha wahi kuniambia kuwa (ikipita mwezi fulani bado hatujafunga ndoa, naondoka) hivyo moja kwa moja nikajua ile siku imetimia na kwakua nampenda, Mama mtu kaingia kisha mimi nikaenda kwao kutoa taarifa.

Wakasema (kwakua mmeamua kutoroshana, na kukiuka kauli zetu. Sasa ishini mnavyojua, ila litakalo wapata msitutafute, na endapo litatokea baya kwa mtoto wao, basi huyo sio wao, bali ni wangu ila wao yupo salama (mfano akifa)

Familia yangu ipo mkoani, hivyo nikawapa mawasiliano, lakini hawakuelewana, wanachotaka ni pesa tu,

Mpaka sasa hakuna suluhu yeyote. Mama mtu hataki tena kurudi kwao, na hata walezi wake hao pia hawamtaki mtoto wao arudi, nilijaribu kwenda ofisi za serikali za mitaa, wakaniambia nipeleke wazee. Jambo ambalo nimelitanguliza kabla ya kwenda kwa mwenye kiti.

Je, nifuate njia gani za kisheria, maana pia siwezi funga naye ndoa kwa hali hii walezi wake wakiwa na makasiriko. Nipeni ushauri ndugu zangu, mana midomo inaumba.

Nawasilisha
 
Mwachie chumba kaishi asipopajua....Atarudi tu home njaa ikimkolea.Wanawake wengine bhana....kujishusha thamani kisa tu kuogopa kuitwa singlemom🙄 Nini kukimbilia Kwa mwanaume ambaye hajaja kwenu?

🤔🤔🤔
Kwahiyo ni heri aitwe single Maza?

#YNWA
 
Habari zenu Wana JF?

Kuna nyuzi kadhaa nilizowahi kuziandika hapa na nikapata shauri mbalimbali toka kwenu,

Mwanamke nilie zaa naye, ila tumechelewa kufunga ndoa kulingana na ukosefu wa mahari, Sasa mwanamke huyo kachoka kusubiri, kaja kwangu Siku ya jana asubuhi akiwa na nguo zake na mtoto wetu

Kwa muonekano ule, haikua na haja ya kumuuliza kwasababu alisha wahi kuniambia kuwa (ikipita mwezi fulani bado hatujafunga ndoa, naondoka) hivyo moja kwa moja nikajua ile siku imetimia na kwakua nampenda, Mama mtu kaingia kisha mimi nikaenda kwao kutoa taarifa

Wakasema (kwakua mmeamua kutoroshana, na kukiuka kauli zetu,.. Sasa ishini mnavyojua, ila litakalo wapata msitutafute, na endapo litatokea baya kwa mtoto wao, basi huyo sio wao, bali ni wangu ila wao yupo salama (mfano akifa)

Familia yangu ipo mkoani, hivyo nikawapa mawasiliano, lakini hawakuelewana, wanachotaka ni pesa tu,

Mpaka sasa hakuna suluhu yeyote,.. Mama mtu hataki tena kurudi kwao, na hata walezi wake hao pia hawamtaki mtoto wao arudi, Nilijaribu kwenda ofisi za serikali za mitaa, wakaniambia nipeleke wazee,.. Jambo ambalo nimelitanguliza kabla ya kwenda kwa mwenye kiti...

Je? Nifuate njia gani za kisheria,.. Mana pia siwezi funga naye ndoa kwa hali hii walezi wake wakiwa na makasiriko. Nipeni ushauri ndugu zangu, mana midomo inaumba.

Nawasilisha
Hawana lolote zaidi ya kutaka pesa. Wape japo laki tano kujitambulisha unaishi na binti yao.
 
Back
Top Bottom