Kwanza definition ya kuhonga nadhani ni ngumu sana.
Ila mtazamo wangu, 'kuhonga' as you put it, ama kumnunulia mwenza shati, soksi hata suit na simu haihitaji uwe umemzidi kipato. Kuna watu wana a 'giving heart'. Na haijalishi kama ni kitu cha tshs 500 ama kupika maandazi matamu na kumpelekea mpenzio. Kama unampenda mtu automatikale ukiona hata shati zuri unalipatia picha lilivyomkaa na unaamua kumnunulia.
Mie nahonga sana kama hiyo ndo definition ya kuhonga aisee. Huna kakako kimeo kimeo hivi yuko pending?
mwanaume ahongwi analelewa
mwanaume ahongwi analelewa
Naomba kupata mawazo yenu
imekaaje kwa mwanamke 'kumhonga' mwanamme?
Nadhani nimeishi kwenye jamii amabayo mwanamme ndio 'breadwinner' na ndio inaonekana halali hata yeye kumhonga mwanamke na si kinyume chake.
Labda nitoe mfano
Mdada ana kipato kuliko mpenzi wake (ikimbukwe si mme)
Na kuna vitu ambavyo anataka kumpa ili waende sambamba
vinaweza kuwa vitu vidogo vidogo kama mavazi n.k na aina hizo za huduma.
Je hii imekaaje? Inakubalika machoni pa walaji?
Na kama wewe ni mkaka mwanamke akikupa vitu hivyo utajisiakiaje?
Kongosho sijui maisha kwanii yako bias kwa mwanamke. skiliza mwanaume aitoa inaonekana ama kutoa kwa ulazima lkn mwanamke inaonekana kama analinunua penzi umeona eeh! Ila ukweli binafsi nilipopenda hata pesa ya gesti nilitoa pale ambapo mwenzangu alitindikiwa na pia kwakua nilikuwa napenda apendeze basi hata pamba nilimnunulia za woolworth sikuweza lkn za manzese nilimudu.Mi naona kuna tofauti pale mwanamme anapokuwa ana kipato kuliko mwanamke
Hapo mwanamke hata akimpa ataoneka anampa zawadi tu sababu kapenda na mwanamme kaamua kuchukua tu.
Lakini pale mwanamke anapokuwa na kipato kuliko mwanamme, lazima utasikia 'huyu dada kiazi kweli, anamhonga mwanamme. Yaani anamnunulia kila kitu hadi pichu'
Watu huwa hatuisemi kama ' a giving heart' rather mwanamke anaonekana 'mjinga au kipofu wa mapenzi'
unajua neno kuhonga halisound vizuri.. Tatizo kubwa la jamii yetu; mwanamke akimfanyia kitu mwanaume itaitwa kuhonga. cha msingi ni kudecide mapenzi yenu mnayaendesha kama nyie mnavotaka au kama jamii inavotaka.