Mwanamke kumtongoza mwanaume hii imekaaje?

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Nimekumbuka miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nafanya kazi kwenye kiwanda fulani maeneo ya A-town.

Mida ya 'lunch break' tumekaa nje ya kiwanda tunapunga upepo na kupiga stori mabalimbali,
mara akatokea msichana mmoja akaniita, akaniambia ana maongezi na mimi kama sitajali,
Basi nikamwambia hakuna shida, wakati huo sikuwa na wazo lolote kuhusu mapenzi nilijua labda ni mambo ya kazi kwa sababu wasichana wengi walikuwa wanakuja kuulizia nafasi za kazi.

Basi yule dada akaanza kuongea, akaniambia ametokea kunipenda sana anaomba niwe mpenzi wake live bila chenga, mara akaanza kulia ananiambia nisimuelewe vibaya, basi ili kuua soo nikambembeleza nikamwambia tutawasiliana baadae ili aondoke.

In short hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kutongozwa na msichana japo baaadae iliwahi kunitokea tena mara kadhaa, nikaja kugundua kuwa ni mambo ya kawaida, mwanamke kumtongoza mwanaume haimaanishi ni malaya au vinginevyo, wana haki ya kueleza hisia zao japo kwa tamaduni za ki Afrika inaweza isiwe kitu cha kawaida.
 

Kuna shemales, kuweni makini, unamuona ni mwanamke kwa nje ila kumbe dumejike..!!
 
Mwisho wa thread maelezo umeyaweka uzuuuri sana. Ni kawaida mno (japo ni nadra ) kwa mwanamke kumtongoza mwanaume directly kwa kusema wao, hutumia indirect way.. matendo zaidi mwanaume ajiongeze. Atakuchekea mara ajipitishe mara salama nyingi ..
N.k
Sure
 
Im sorry, bado sijajiandaa kisaikolojia kupokea mtihani wa sampuli hiyo, na kama ukitokea ataniacha na maswali elfu moja najiuliza nikose majibu, japo najua nao wana haki ya kupenda na kufunguka, lakini....
 
Mbona hakuna shida? Ukimpenda mtu kwa tabia au sura na ukatamani awe mtu wako wa karibu au mchumba wako, ukimwambia shida Iko wapi? Kwa upande wangu sioni shida kwa sababu hata mimi nimewahi kuambiwa hivyo mara kadhaa.
 
Kakuona wewe mlaini, ikiwa sura ya kazi ataanzia wapi, huwa wanaishia kusema tu nimekumis, mara huwa unanifurahisha mjuba unaunganisha tu doti hapo unaelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…