King Jody
JF-Expert Member
- Oct 8, 2022
- 1,834
- 3,456
Nimekumbuka miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nafanya kazi kwenye kiwanda fulani maeneo ya A-town.
Mida ya 'lunch break' tumekaa nje ya kiwanda tunapunga upepo na kupiga stori mabalimbali,
mara akatokea msichana mmoja akaniita, akaniambia ana maongezi na mimi kama sitajali,
Basi nikamwambia hakuna shida, wakati huo sikuwa na wazo lolote kuhusu mapenzi nilijua labda ni mambo ya kazi kwa sababu wasichana wengi walikuwa wanakuja kuulizia nafasi za kazi.
Basi yule dada akaanza kuongea, akaniambia ametokea kunipenda sana anaomba niwe mpenzi wake live bila chenga, mara akaanza kulia ananiambia nisimuelewe vibaya, basi ili kuua soo nikambembeleza nikamwambia tutawasiliana baadae ili aondoke.
In short hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kutongozwa na msichana japo baaadae iliwahi kunitokea tena mara kadhaa, nikaja kugundua kuwa ni mambo ya kawaida, mwanamke kumtongoza mwanaume haimaanishi ni malaya au vinginevyo, wana haki ya kueleza hisia zao japo kwa tamaduni za ki Afrika inaweza isiwe kitu cha kawaida.