Habari zenu wana jamvi. Niko na mke wangu karibuni mwaka sasa tangu tuoane na kufunga ndoa lakini bado hatujabahatika kupata mtoto. Kuna wakati mke wangu huhisi dalili zote za ujauzito ikiwemo kuchefuchefu, kupatwa na kizunguzungu, maumivu ya tumbo chini ya kitovu, na pia huweza kupitisha tarehe zake hata kwa muda wa siku 5 au zaidi, lakini baadae huziona siku zake kama kawaida. Sasa naomba msaada wenu kwa wanaojua je tatizo ninini, na pia je mimba huchukua muda gani kuonekana kupitia kipimo cha mkojo? Msaada please I get scared.