Mwanamke mpumbavu hupiga kelele

"A man says one word ,She says five words.!
"A man says five words, She says a hundred words...!" Lucky Dube R.I.P
 
Wanaume wengi kituo bar baada ya kutoka kazini, nyumbani mida mibovu kukimbia kelele na asubui uwahi kazini wikiendi awakai nyumbani.
Kelele ni negative energy
 
Tatizo la ndoa za Tanzania siyo kwamba wanawake walioolewa wote wanakelele siyo kweli ni asilimia ndogo tu, ila kinachosumbua ndoa nyingi za kitanzania ni umasikini, ujinga na malezi mabaya hasa kwa watoto wa kiume tena tunakoelekea wanaume wasipobadilika watapata tabu sana maana kizazi cha baadaye kitakuwa tofauti sana na kizazi kilichopita cha kuishi Bora liende hata ukiwa na watoto mia moja watajilea tu tofauti na kizazi cha Sasa cha kuishi kwa bajeti kama watu wanaojielewa.

Kijana anaanzisha maisha ya ndoa katika Hali ya kushindwa hata yeye kujua anakula nini, Hana makazi, Hana akiba yoyote tena na mwanamke asiye na uelewa wowote wa kujenga familia kwa bajeti baada ya kuanzisha maisha hayo kwa michango ya harusi pia wanatumia vibaya au hela zote bila kuweka sawa mambo muhimu hapo hapo kijana anatoka kwao hajui hata kufua nguo zake, kupika hajui na bajeti ya jikoni.

Vitu vidogo vidogo vya maisha ya nyumbani hajui anategemea msaidizi wake ambaye ni mke wakati yeye alitakiwa kuwa kichwa akiwa anajua Kila kitu kiasi cha huyo mke kumuheshimu Sasa mtu hata kukata matunda ya kujenga afya ya mwili wake hajui anategemea mke Sasa hapo kama siyo kutafuta kelele ni nini?

Somo kwa wanaume wote wanaotaka kuishi kwenye kizazi hichi cha kileo kabla ya kuoa unatakiwa ujitathimini je wewe kama wewe unajiweza na kujielewa? Unaweza kupika? Kufua nguo, kuosha vyombo, kudeki nyumba, kwenda sokoni na bajeti zote za nyumbani, unahitaji kuwa na wake wangapi? Watoto wangapi?

Ukishakuwa umeweza hayo unaangalia eneo linalokushinda unakwenda kujifunza iwe mapishi jifunze iwe kufua kama huwezi nunua mashine ya kufua, weka mpango wa maisha yako kiasi ukioa huyo mwanamke atakuheshimu na kelele hutazisikia na utapewa huduma kwa Upendo tena kwa kutetemeka maana anayehudumiwa anajielewa na alikutwa akiwa ametengeneza maisha yake imagine mwanaume anaoa hata vifaa vya kupika chakula chake Hana anategemea hoteli na mama ntilie.

Sasa akioa na mwanamke akakuta yeye mwenyewe hakujithamini alafu analamika chakula na kwavile hajui hicho chakula mpaka kiive kinatumia muda gani na gharama yake na hata vyombo vya kusaidia kukipikia kikaiva haraka yule anayemwambia watapigiana kelele hivyo ni muhimu sana kichwa cha nyumba kujiandaa kuwa kichwa na heshima inakuja yenyewe tena kijue Kila kitu kiasi cha mke akifika akifanyiwa kuelekezwa mpango wa nyumba anajipanga mwenyewe na mwanaume asiwe mgeni nyumbani kwake kiasi cha kutokujua hata friji imebeba nini siku hiyo.
 
Tilte iliivutia Sana. Nime subuskraibu.

Nimerudi...lkn ulivyoweka hizi {®©% 2:16)
Nikaishia hapo hapo
 
Tunaweza kulalamika sana kuhusu waume zetu wanaochelewa sana kurudi nyumbani ila ukweli ni kwamba, kelele zetu ndio zinawafanya waume zetu waone ni heri kuchelewa nyumbani, kuliko kuwahi nyumbani ukakutana na kelele zisizo na mwisho.
Umenikuna sana hapa, nawezaje kukupata nikupe zawadi yangu
 
Hio paragraph ya kwanza [emoji108][emoji108][emoji108][emoji108][emoji108][emoji419][emoji419][emoji419]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…