Mwanamke mzuri wa kuoa ni mwalimu.

Mwanamke mzuri wa kuoa ni mwalimu.

Kinachozungumzwa ni tabia za jumla za makundi ya watu katika jamii. Mfano kuna makundi kama walimu, wanasheria, askari, mama lishe, madaktari, wanasiasa n.k. Watu wa kundi moja huwa na tabia zinazowatofautisha na wengine katika makundi tofauti. Hata hivyo si ajabu baadhi ya watu wa kundi moja kuwa na tabia fulani za walio katika kundi jingine. Sasa kilichopo hapa ni mapendekezo kutokana na kundi la walimu. Watu wanaowafahamu walimu (kwa ujumla wao) wanatoa changamoto ambazo kwa sasa ni kupendekeza sifa chanya na hata hasi za wanawake katika kundi hili.
Mtoa mada ameanza na sentensi hii"ukitaka kuoa oa mwalimu" kwa sentensi kama hii we umeelewaje? Ndo maana nikasema kazi ya mtu haina uhusiano na maisha ya ndoa! Maisha ya ndoa ni kupendana,kuvumilana!na kuheshimiana!
 
Ukitaka kuoa oa mwanamke ambaye ni mwalimu.
Huwa ni watu wenye hekima, wanaweza malezi kwasababu huwa wanakutana na watoto wengi wa tabia tofauti so wa kwake hawatomshinda.
Ni watu ambao hawawi overworked mara nyingi hivyo anapata muda wa kuwa na familia yake.
Na inasemekana wanaume wengi wenye hela huoa walimu.
Hiyo ni kweli wadau?
Wenye taaluma zingine mbona kazi tunayo.

hilo tu? Basi na mabar maid wachange fani wawe waalimu! Hukufafanua mwalimu wa stage gani pia, kwani mwalimu ni mwalimu awe wa chekechea au chuo! Au umepata mwalimu huko unatafuta support hujiamini? Acha hizo, kama kuoa oa mtu si fani yake hazina correlation
 
Ukitaka kuoa oa mwanamke ambaye ni mwalimu.
Huwa ni watu wenye hekima, wanaweza malezi kwasababu huwa wanakutana na watoto wengi wa tabia tofauti so wa kwake hawatomshinda.
Ni watu ambao hawawi overworked mara nyingi hivyo anapata muda wa kuwa na familia yake.
Na inasemekana wanaume wengi wenye hela huoa walimu.
Hiyo ni kweli wadau?
Wenye taaluma zingine mbona kazi tunayo.

Mke/mume mwema anatoka kwa Mungu.Period
 
Kwa hiyo sisi mamessenger tusiolewe jamani nyie watu mna balaa nyie. Mwanamke mzuri wa kuoa ni yule mwenye tabia na maadili mema, mwenye heshima, adabu, uvumilivu bila kusahau upendo. Hiyo ni taaluma tu hakuna uhusiano na kuolewa

hapana dena, kila mtu ataolewa bila kujali taaluma yake ila hiyo ni tabia ya kiujumla ya kundi la walimu.
 
hapana dena, kila mtu ataolewa bila kujali taaluma yake ila hiyo ni tabia ya kiujumla ya kundi la walimu.
Badilisha basi maneno yako kwenye thread ili watu wakuelewe vizuri!
 
Nafikiri kazi zote ni nzuri tu. Ila mwalimu anapewa kipaumbele pengine na watu wengi kwa kuwa kazi yake inampa angalau muda wa kurudi nyumbani mapema na kuhudumia familia. Na pia anayo saikolojia ya malezi. Baadhi ya kazi zina changamoto sana, kama nesi. Niliwahi kuwa na gf nesi, basi siku nyingine ana zamu ya usiku inabidi mtu ukae roho juu, huna uhakika kama yupo kweli hospitali au yuko mahali pengine. Mtu anayefanya kazi benk kwa mfano, unakuja kuona siku nyingine anafunga mahesabu saa nne usiku, siku nyingine anafika home saa sita, mara amekwenda kutembelea matawi mikoani wiki tatu, amani inaanza kukosekana.

Lakini pia changamoto ya mke mwalimu ni kwamba mchango wake wa kifedha ndani ya nyumba ni almost zero. Maana mshahara anaolipwa unatosha nauli tu ya kumpeleka na kumrudisha kutoka kazini. Ila kama mme ni mtu ambaye muda mwingi yupo busy na kazi, mke mwenye taaluma ya ualimu anaweza kuwa ni chaguo zuri kwake, though mke siku zote huwa anapatikana by coincidence sidhani kama huwa inawezekana kuziweka sifa za mke unayemtaka na ukaweza kweli kumpata yule uliyetaka. Mara nyingi mke wa kuoa huwa anatokana na available possibilities.
 
Siku hizi uzuri wa ndoa ni Pesa tu.Kama huna pesa au mna mapunfuku katika mapato ya kyuendesha familia hata ukiolewa/kuoa nani upendo kwenye familia ni sifuri.
 
Ukitaka kuoa oa mwanamke ambaye ni mwalimu.
Huwa ni watu wenye hekima, wanaweza malezi kwasababu huwa wanakutana na watoto wengi wa tabia tofauti so wa kwake hawatomshinda.
Ni watu ambao hawawi overworked mara nyingi hivyo anapata muda wa kuwa na familia yake.
Na inasemekana wanaume wengi wenye hela huoa walimu.
Hiyo ni kweli wadau?
Wenye taaluma zingine mbona kazi tunayo.


Mh........,hapo bado hujanishawishi,maana kwa mimi ambaye first appointment yangu ya kazi ilikuwa ni ualimu kabla ya kujiendeleza kielimu nawajua vizuri sana hawa viumbe.Nimefanya nao kazi na nimeshuhudia tofauti kubwa sana kati ya kizazi hiki na walimu wa zamani maana wale wa zamani kweli walikuwa wanajiheshimu na mpaka leo wanatunza heshima yao,lakini hawa walimu wa leo sijui MMEM sijui wanawaitaje ukitaka kumuweka ndani kwanza jiandae kupata mtu ambaye ni dataless,pili jiandae kupata watoto ambao watakuwa na uwezo mdogo darasani na hii ni kutokana na asilimia kubwa ya walimu wa leo kuwa failures katika masomo yao. nasema hivyo kwa kuwa mama anachangia akili ya mtoto 80% .Yapo mengine mengi tu lakini kwa kuanzia naona inatosha.
 
Mke mwema anatoka kwa mungu. Si lazima awe mwalimu, kwani ualimu ni wito na wengine wamesomea tu ili afanye kazi walimu jina. So anakua hana wito wala nini hata watoto hanampango nao anachojali salary yake tu. Mke mwema anaombwa kwa mungu.
 
Ila Walimu wa Kizazi hiki cha Dot Com aka Voda Fasta nasikia wanamegwa sana na Ma Head Teacher na Maafisa Elemu ha ha ha
 
Id yangu ni utata nini? Mimi ni mwanamke. Sawa nitamwita mme wangu kwa cheo chake. Cjui atakuwa mwalimu..!!

Hapana sijachanganywa na ID yako. Nimejibu kwa mtazamo wa wanaume kwa kuwa post yako imesema ... "Ukitaka kuoa........." Najua kuwa Husninyo inaundwa na "Husna" hiyo "...nyo" ni kama Ronaldinho, by the way kwa Brazil ikiongezwa "...nyo" katika jina inamaanisha "mdogo." Hivyo Ronaldinho ni "Ronaldo mdogo." Wadau watanisahihisha kama nimekosea.
 
Back
Top Bottom