Yeah,hii inawezekana sana.Sema inategemea sana na malezi na mazingira uliyokulia.Nachukulia mfano wangu nimekulia kwenye familia kubwa,i mean extended familly,ambapo nimekua na watoto wa kike watatu,wanne,na tulikuwa close sana,nimesoma co-education halafu day.Nimeenda JKT na Chuo ambako ni mchanganyiko na bahati nzuri nilikutana na mdada wakati nipo chuo tukawa kwenye group study moja pia.
Huyu mdada akatokea kuwa rafiki yangu sana,hakuwa na bf na mimi nilikuwa na gf anasoma chuo kingine lakini alikuwa mtu ambae hata love life yangu alikuwa anaijua.Baada ya kumaliza chuo miaka hiyo,tulipangia kazi mikoa tofauti lakini tulikuwa tunatembeleana na alikuwa akija kwangu wakati huo naanza maisha nilikuwa na chumba kimoja "fullsuite",yaani chumba,unapika humo humo,makochi yako humo,yaani kila kitu basi tulikuwa tunalala pamoja,yeye kitandani mimi kwenye kochi
Acha hiyo hata dadangu ninae mfuata ambae kulikuwa close pia wakati naanza maisha alikuwa akinitembelea tulikuwa tunalala chumba kimoja.
Hii nafikiri inategemea kama nilivyosema mwanzo na malezi na mazingira uliyokulia