Mwanamke ninayempenda humu jf kumbe yupo ujerumani anakula maisha, japo ni ndoto ila nimeumia sana.

Mwanamke ninayempenda humu jf kumbe yupo ujerumani anakula maisha, japo ni ndoto ila nimeumia sana.

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
8,252
Reaction score
18,335
Mapenzi hayazuiliki na kamwe huwezi kuyaficha.

Usiku wa leo umekuwa ni usiku ambao nimeota ndoto nyingi ambazo zinabeba uhalisia wa maisha yangu kwa kiasi kikubwa. Moja wapo ni hii ambayo inamhusu mwanamke ninayemzimikia sana humu jf.

Iko hivi,

Leo nimeota nikiwa geto naperuzi jf kwenye jukwaa la chitchat, nikafungua uzi ulioanzishwa na member (simkumbuki ni nani), kwenye uzi huo aliomba kila member aelezee ni umbali gani mrefu aliowahi kuusafiri kwa gari yeye mwenyewe akiwa anaendesha. Basi kila mmoja akaanza kuflow experience yake, wengine wakisema dar-tunduma, wengine dar-mwanza, nakadhalika nakadhalika.

Sasa kwenye ile page ya kwanza nikaona comment ya yule mwanamke ninayemzimikia kabisa humu jf na yeye akitoa mchango wake, alikuwa ameorodhesha miji aliyokuwa amesafiri. Miji yote ilikuwa ni ya mbele (ujerumani). Alikuwa anaeleza na nini alikifanya kwenye safari husika; mara ni tour, mara kufatilia docs fulani fulani.

Kilichokuja kuniua ni pale alipoambatanisha na picha kwenye hiyo comment hiyo. Picha ya kwanza ilipigwa kutoka ndani ya gari ikionyesha gari lilikuwa katika mwendo. Picha zilizofuata hazikuwa na uhusiano na post, ila nadhani alitaka kukazia ili tuone ni kweli yupo ulaya.
Picha ya pili ilionekana akiwa amesimama akiwa ameshika camera ndogo huku akiwa ameachia tabasamu mwanana. Nyuma yake alikuwa amesimama mwanamke mwingine wa kizungu naye akiwa anatabasamu.

Picha nyingine ambayo ilikuwa ni selfie alikuwa yupo na mtoto mdogo wa kike ambaye naweza kusema ni mwanae maana wanafanana sana. Wote walikuwa na tumasikio twa mbwa tule tunakopatikana snapchat.
Picha mwisho ilipigwa sebuleni, yaani mwonekano wa ile sebule umekaa kimambele kabisa aisee, sio kama kwetu huku.
Nakupenda sana M...., ila naumia kwamba ni vigumu kukupata kwa kuwa mwenzangu uko ujerumani, uko na maisha poa na una mtoto pia wakati huo mimi nipo naganga njaa. Ndoto hii imeniumiza, hope sio kweli.

Nimependa, nimekufilia mbali na kuozeamo.
 
Dah..ndoto nzuri....ubaya wa ndoto huwa pale unapoona mlango wa choo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom