Mwanamke si rafiki

Mwanamke si rafiki

Six Man

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
253
Reaction score
892
FRANK NA NESTO WAPO KANISANI...

Frank: Nesto Kwa Nini Mwanamke Yule Ananitazama Hivi?

Nesto: Mwanamke Yupi?
Frank: Yule Pale Kavaa Gauni Ya Bluu.
Nestor: Usimtazame Kamwe achana nae.

Baada Ya Dakika Chache Frank Akasema Tena lakini Nesto Anani Konyezea Jicho!
Nesto: nimeshakwambia Usimtizame wewe sikiliza mahubiri.

Baada Ya Misa Frank Akapotea Na Nesto Akaja Kumuona Saa 5 Usiku.

Nesto: Frank Ulipitia Wapi Tangu Mchana Saa 6 Mpaka Hivi?

Frank: Ndugu yangu Ni Story Ndefu Nimechoka sana hapa nilipo,yaani niko hoi!!!

Nesto: story Ndefu Kulikoni?

Frank: Tulipotoka Kanisani Yule Mwanamke Akaniita Tukaongea vizuri tu halafu Tukaenda Kwake Tukala chakula Ila Alipotaka Kunikumbatia Tu Mumewe Askari Akaja Yule Mama Akasema Mumewe Ni Mkali Sana Ataniua Kwa Hiyo Akanipa Nguo Nyingi Sana Zilizo Kuwa Kabatini Nikajifanya Mpiga Pasi Nguo.

Nesto: Yaani Toka Mchana Mpaka Hivi Saa 5 Usiku umekuwa unapiga Pasi Tu?

Frank: Ndio Kaka, na vyombo juu nimeosha na kusugua masufuria.

Nestor: Nilikwambia Usimuangalie Hukusikia Unatakiwa unisikilize ninapo Kwambia Kitu. Unaona Zile Nguo Ulizo Piga Pasi Mimi Ndio Nilizifua Jumapili Iliyopita.
Na Mimi Kanifanyia Hivyo Hivyo Kaka na nimeambiwa ni mpango wao na mumewe ndio maana hawaajiri wafanyakazi wa ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana. Mnaokonyeza malaya ndo adhabu yenu hiyooo. Mpaka mshikishwe adabu zenyu ndo mtakoma.
 
Hao akina Frank ni wanaume wa Dar. Wa mikoani huwa tunapigana mpaka kieleweke.
 
Nestor: Nilikwambia Usimuangalie Hukusikia Unatakiwa unisikilize ninapo Kwambia Kitu. Unaona Zile Nguo Ulizo Piga Pasi Mimi Ndio Nilizifua Jumapili Iliyopita
🤣
Lakini Nestor angefunguka zaidi na si kumwambia tu Frank kua usimuangalie! Besti wao wa tatu atapewa kazi ya kuzipanga kabatini.
 
Back
Top Bottom