Mtambuzi mbona umeelekeza kwa wadada tu ilihali wapo wakaka abao wanaweza fanya the same?
to me mtu anayemkataa mtu pasi ustaarabu na kwa kashfa huyu si bnadam wa kawaida. kumbukwe kabisa kwamba kila mwanamke ana haki ya kutongozwa na mwanaume na si jambo baya ila si kila akutongozaye basi wamkubalia na kutoka naye neva.
lakinai pia unapotaka kumkataa mtu tumia hekima sana ili badala ya kauwa adui muwe good friends ambaye waweza kumsaidia ama yeye aweza kukusaidia baadae. ina pendeza sana kwa mwanamke kutokuwa na maneno ya kashfa na matusi ingawa waswhili husema asiye kujua hakuthamini. Pia usimdharau mtu katika maisha yako.
Kiukweli jamani hakuna kitu kibaya kama dharau kwa mtu mwingine yawe mdogo ama mkubwa kwani hujui yeye kesho yake itakuwaje. Unapomtolea mwanaume kashfa ujue kabisa wajipandia laana. Kuna mfano wa dada mmoja niliwah kupanga nae nyumba moja mwenzangu alikuwa na bahati sana ya kupata wakaka yaani wapenzi ila alikuwa anawananga sana. aliwah hadi kumuita mmoja tumbo kama anakunya humohumo tulijaribu kumshauri sana juu ya tabia yake ila kwakua anajijua yeyey ni mzuri sana alikuwa anasema yeye hadi atoke nyumbani kufika posta kila kituo atapakiza na kushusha mwanaume. tulichoka tukaamua kumuacha aendelee.
cha ajabu wenzie wote wa mule ndani ndoa zilipita akabaki yeye tu, leo hii bado yupo kapanga nyumba mitaa fulan kaishia kuzaa mtoto na mume wa mtu, hana mbele waa nyuma uzuri wake wote umeishia kapuni. huyu ni mtu wa kweli niliyeshuhudia so nakubaliana kabisa na haya ayasemayo
Mtambuzi