Hili jambo la loliondo lilishawahi kujadiliwa sana hapa JF. Waziri alikanusha kuwa hakuna unyanywasaji uliofanyika na pia watu waliochomewa maboma hawakuwa watanzania, swali ninalojiuliza: ikidhibitika kuwa kulikuwepo na vitendo vya unyanyasaji na waliochomewa maboma walikuwa watanzania,Je waziri atawajibika kivipi kufuta kauli yake ya hawali kuwa hakuna madhara yeyote yaliyo tokea?
Mkuu Ulimbo tatizo ni pana zaidi: hata wangekuwa wakenya kama serikali hii isiyo na uwezo wa kufikiri inavyotaka kutuaminisha, ni sheria gani inayosema wageni wa nchi fulani wachomewe nyumba zao, wabakwe na kuteswa? Jumuia ya kimataifa na hususan nchi ya Kenya ikiamua kudai haki za "wakenya" Tanzania itajibu nini? Kati ya majibu ya mawaziri wa JK yaliyo wahi kunichefua ni hili la kuwapa wananchi wa Loliondo "Ukenya" baada ya kuwatesa na kuwabaka. What a lame minister!