Drone Camera
JF-Expert Member
- Jul 25, 2017
- 14,041
- 13,907
Mwanamke mmoja raia wa Tanzania
alikamatwa wikendi iliopita kufuatia
madai ya mauaji ya jirani yake
kutoka Kenya katika eneo la
Chhattapur kusini mwa jimbo la
Delhi kufuatia mgogoro kati yao
kuhusu chupa ya pombe.
Kulingana na gazeti la The Citizen
nchini Tanzania mtuhumiwa
amedaiwa kuwa mkaazi wa jiji la Dar
es salaam.
Maafisa wa polisi wanasema
kwamba mwili wa marehemu
uliopatikana nyumbani kwake
ulikuwa na majereha ya kisu kifuani.
Wakati wa uchunguzi, watu kadhaa
raia wa Kenya na Watanzania
pamoja na wale wa Nigeria
walihojiwa na maafisa wa polisi.
"Tulipokea simu mwendo wa saa
mbili na dakika kumi usiku kutoka
kwa mwanamke mmoja raia wa
Kenya akidai kwamba dadake
ameuwawa'', alisema kamishna wa
polisi wa wilaya ya kusini Vijay
Kumar akinukuliwa na gazeti la The
Nation nchini Kenya baada ya
kuzungumza na gazeti la India
Express nchini humo.
"Tulikimbia katika eneo la mkasa na
kumpeleka mwanamke huyo
hospitalini ambapo daktari alisema
kwamba tayari alikuwa amefariki."
Rekodi za mawasiliano ya simu na
kanda za video za CCT zilitathminiwa
ambapo mtuhumiwa ambaye alikuwa
akiishi katika nyumba moja ilio
mkabala na jumba ambalo
marehemu alikua akiishi alikamatwa
kulingana na naibu huyo wa
kamishna wa polisi .
Akihojiwa na polisi mtuhumiwa
aliambia maafisa hao kwamba sku
mbili zilizopita alikuwa amemtaka
marehemu kumpatia pombe swala
ambalo alikataa.
Ni wakati huo ambapo walirushiana
maneno kabla ya mshukiwa
kumdunga kisu marehemu, alisema
afisa huyo wa polisi wa eneo la
Delhi.
Kisu pamoja na nguo ambazo
mshukiwa huyo alikuwa amevaa
wakati wa kisa hicho zilipatikana
nyumbani kwake.
Kulingana na gazeti la Nation nchini
Kenya, mtuhumiwa na mpenzi waake
walikua katika nyumba hiyo wakati
wa mgogoro huo.
Gazeti hilo limedai kwamba wawili
hao walitoroka lakini walipatikana na
kushirikishwa katika uchunguzi ,
afisa aliyekuwa akifanya uchunguzi
huo aliambia gazeti la Hindustan
Times
Mwanamume huyo alikiri kwamba
mpenzi wake alikosana na
marehemu kuhusu chupa ya pombe.
source BBC
alikamatwa wikendi iliopita kufuatia
madai ya mauaji ya jirani yake
kutoka Kenya katika eneo la
Chhattapur kusini mwa jimbo la
Delhi kufuatia mgogoro kati yao
kuhusu chupa ya pombe.
Kulingana na gazeti la The Citizen
nchini Tanzania mtuhumiwa
amedaiwa kuwa mkaazi wa jiji la Dar
es salaam.
Maafisa wa polisi wanasema
kwamba mwili wa marehemu
uliopatikana nyumbani kwake
ulikuwa na majereha ya kisu kifuani.
Wakati wa uchunguzi, watu kadhaa
raia wa Kenya na Watanzania
pamoja na wale wa Nigeria
walihojiwa na maafisa wa polisi.
"Tulipokea simu mwendo wa saa
mbili na dakika kumi usiku kutoka
kwa mwanamke mmoja raia wa
Kenya akidai kwamba dadake
ameuwawa'', alisema kamishna wa
polisi wa wilaya ya kusini Vijay
Kumar akinukuliwa na gazeti la The
Nation nchini Kenya baada ya
kuzungumza na gazeti la India
Express nchini humo.
"Tulikimbia katika eneo la mkasa na
kumpeleka mwanamke huyo
hospitalini ambapo daktari alisema
kwamba tayari alikuwa amefariki."
Rekodi za mawasiliano ya simu na
kanda za video za CCT zilitathminiwa
ambapo mtuhumiwa ambaye alikuwa
akiishi katika nyumba moja ilio
mkabala na jumba ambalo
marehemu alikua akiishi alikamatwa
kulingana na naibu huyo wa
kamishna wa polisi .
Akihojiwa na polisi mtuhumiwa
aliambia maafisa hao kwamba sku
mbili zilizopita alikuwa amemtaka
marehemu kumpatia pombe swala
ambalo alikataa.
Ni wakati huo ambapo walirushiana
maneno kabla ya mshukiwa
kumdunga kisu marehemu, alisema
afisa huyo wa polisi wa eneo la
Delhi.
Kisu pamoja na nguo ambazo
mshukiwa huyo alikuwa amevaa
wakati wa kisa hicho zilipatikana
nyumbani kwake.
Kulingana na gazeti la Nation nchini
Kenya, mtuhumiwa na mpenzi waake
walikua katika nyumba hiyo wakati
wa mgogoro huo.
Gazeti hilo limedai kwamba wawili
hao walitoroka lakini walipatikana na
kushirikishwa katika uchunguzi ,
afisa aliyekuwa akifanya uchunguzi
huo aliambia gazeti la Hindustan
Times
Mwanamume huyo alikiri kwamba
mpenzi wake alikosana na
marehemu kuhusu chupa ya pombe.
source BBC