Sonko Bibo
JF-Expert Member
- May 24, 2019
- 957
- 1,493
Nilichogundua ni kwamba watu wanadhani tunaosema kataa ndoa ni tunamaanisha kataa kuoa..Mimeoa na nina mtoto mmoja. Hakuna siku ambayo nimekataza watu kuoa. Kuoa sawa ila ule mkataba wa kitapeli uliopewa jina la ndoa siwezi kusaini
Ukweli ni kwamba ndoa ni tofauti na kuoa
Kuoa ni kwamba mnatambulishana pande zote mbili na kama mahari unalipa accordingly yaani hapa hakuna mtu anakulazimisha kuwa lazima utoe kiasi kadhaa ndio uishi na binti yetu..
Ukiona mama au baba wa binti anajikita kwenye kukusopoa fedha nyingi na wanafanya lazima basi hiyo ni big redflag kabisa ya mwanzo ambayo haihitaji kusubiri hadi uanze kuishi na binti yao.
Kwanini??
Wazazi wa binti hawatakiwi kuwa na power juu yako hata siku moja hata kwa kuteleza tu haitakiwi..
Wewe ndio unatakiwa uwe na power kila sehemu sio mtu mwingine yeyote yule awe anatoka upande wa binti au wa kwenu wewe mwanaume.. maana muoaji ni wewe..
Wazazi wakiwa na power juu yenu maana yake ni kuwa mtaishi chini ya misingi yao jambo ambalo litakupelekea mwanaume ukose mamlaka kamili kwa familia yako
Like wanaweza kuamua muda wowote binti aende kwao wanapojisikia na binti akaenda hata kama wewe hutaki jambo hilo litokee so unashindwa kuoppose hilo jambo.. Hii inaweza ikaja siku ukashangaa unaulizwa maswali ambayo utaona kabisa mbona ni kama navuliwa nguo na wakwe zangu? Kwanini?
Kwasababu hujaseti standards na limits zako so wanakuona vulnerable sana..
Kiasi hata shemeji yako mdogo kiumri akawa anakukoromea akihisi kuwa anakumudu.
Vijana kabla hawajaoa ni lazima watake total control juu ya binti na familia yake wakati wote wa uchumba..