Mwanamke zingatia haya ni kwa faida yako

Mwanamke zingatia haya ni kwa faida yako

Makamee

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2013
Posts
2,029
Reaction score
1,194
Akina dada naomba niwajuze machache huenda yakawa msaada kwenu.

1.Usitumie sabuni yeyote yenye chemical kujisafishia sehemu za siri(hupelekea kuu walinzi wa maeneo hayo na kukusabishia fungus na muasho ukeni.

2.Usitumie ndoo ya kudekia kwa kwenda kuogea(hubeba vimelea na vijidudu vitakavyokusabishia UTI na fungus.

3.Wakati wa kujisafisha baada ya haja kubwa nawa kwa kutoka mbele kuelekea nyuma(hii itasaidia vijidudu vya kinyesi visiingie ukeni na kukuletea madhara.
 
Asante,pia zingatia kuwa na mpezi mmoja au tumia kinga ufanyapo mapenzi nje ya ndoa.
 
Hivi na kujisafisha kwa namna ya kujiingiza vidole kuna tatizo?
 
Nimeelimika na mengi sana ktk safu hii jf doctor nikaamua nami nijiunge ili niwe na mwanachama halali, with thanks; nikaribishen!
 
Hivi na kujisafisha kwa namna ya kujiingiza vidole kuna tatizo?

Tatizo lipo tena kubwa tu. Ikumbukwe kinachoruhusiwa kuingia ktk uke wako ni uume tu.
OSHA sehemu za nje(clitoris and vagina lips) sio ndani kwasababu uke unajisafisha wenyewe kwa kujiosha(self cleaning oven).
Haifai kuingiza vidole vyaweza kua na uchafu ukasababisha kuwaua Walinzi(Lactobacilli) na kukuletea Chain Reaction.
 
Unajua kuna imani potofu kua,
1.Uke ni sehemu chafuchafu inayohitaji kusafishwa kwa sabuni,marashi,detol kila mara nje na mpaka ndani.

2.Uke unahitajika uwe mkavu wakati wote.

3.Uke unahitajika uwe hauna harufu hata kidogo .
Dhana hizi na mafundisho ya kitchen party na elimu vijiweni ndo hupelekea wanawake wengi kujirundikia maradhi sehemu zao za siri.
 
Back
Top Bottom