Dada yangu pretty, mimi na mwenza wangu tunaishi kama marafiki, tunataniana na hakuna ubabe ndani ya nyumba. mwanzoni kabisa wakati wa uchumba tulikaa chini nikamweleza mimi nini nataka kwenye relationship yetu na yeye aniambie ni nini anataka kwenye uhusiano wetu. Mipaka ipi isivukwe na vitu gani vya kufanya.Kitu ambacho nilimsisitizia sana ni Kunisikiliza nachosema/nachotaka na kuwa muwazi kwa kila jambo analofanya yaanikusiwe na siri baina yetu. km ni pesa ajue kila kitu mshahara wangu na wake nijue ili kusiwe na mmoja awe na matumaini ya juu sana kwa mwenzie kifedha kumbe si hali ilivyo, tuishi maisha ya kweli na si kupeana ahadi za uongo. Nakushauri sana kuwa muwazi kwa mwenzi wako, usipende kuweka kitu moyoni na kwenda kwa shosti kumueleza au ndugu yako, kila tatizo mueleze mmeo, na yeye msisitize awe huru, asifiche matatizo yake.Sio kwamba hatugombani tunagombana ila ikitokea kutoelewana huwa tunakwenda room tunafunga mlango tunapashana kila kitu kwa uwazi hata 2 hrs zinaweza isha baadaye tutafikia muafaka, kama mmoja kakosa itabainika na huwezi amini tunaishia KUMEGANA, tukitoka hapo hasira zimekwisha. Kuwa na mashosti kazini, jichanganye nao kwa sana lkn usiwaamini sana mashost, hakikisha huna shosti wa kumleta leta nyumbani kila wakati, mara ooh kakupigia simu kidogo naenda kwa amina, au amina njoo nyumbani, mmeo yuko sebuleni wewe kutwa nje na amina story tu unamwacha mmeo peke yake na yeye ataboreka idoo utasikia naenda kupiga story na John anaishia bar. hakikisha kama huko kazini au ni weekend mmeo ndo awe company yako, kama kuna vitu mlipanga yeye kasahau, mkumbushe onyesha concern kwenye mipango ya family yenu, usiishie kudai mitoko kila siku ilhali hata kiwanja hamna, au watoto hawana school fees, au hawana maendeleo mazuri shuleni. kuwa mbunifu kidogo kama mwanaume kwenye ngono ni wadhaifu sana km ukiwahi rudi toka kazini mmeo hajarudi, au weekend upo nyumbani mzee hayupo , ikifika time anarudi usikaae tu sebuleni akirudi umenuna akisema habari za hapa hata usoni humwangalii unanuna unajibu kwa kutafuna tafuna, hata km uko sebuleni mpokee kwa bashasha, mpeleke room, mpe mabusu moto moto, km ulijifunga kanga moja idondoshe kwa makusudi mkumbatie, utaona jamaa linavyochanganyikiwa, damu itaenda mbio, halafu unasepa zako kumwandalia msosi wakati jamaa kishapanda mshawasha, kwa mwanaume hapo atakuahidi hata mtoko ili mradi umpe MCHEZO, hujaweka AMANI NYUMBANI hapo? Naumbuka wakati wife kajifungua our first kid, nilichukua likizo ya mwezi mzima, Maids wetu alipoona kuna mtoto pale akasingizia mama yake anaumwa akasepa, Ngoma ikawa hakuna msaidizi, nilfua nepi za mtoto na kupika na shuguki karibu zote for the whole month na baada ya likizo km miezi 8 zaidi niliendelea kufanya kitchen chaos zile, wife alikuwa na shosti yake ambaye alikuwa akija pale mara kwa mara, alishangaa sana mwanaume huyu anafanya hizikazi za nyumbani mwanzo alisifia sifia lkn kilimuuma sana kumbe kuona mwanamke mwenzie ana enziwa namna ile, mimi sikuwa na mazoea naye na sikupenda kuzoeana naye kupita kiasi coz nilishajua hapa nini kitatokea, nikamkanya wife lkn yeye hakuweza ona mbali sana akaona km nna chuki binafsi na shosti yake, baada ya mtoto kufika mwaka, nika notice changes kwa wife, kwa vile nilipenda sana kukaa na kid wangu nikitoka job, basi yeye ataaga naenda saloon kidogo kumbe anaenda kwa shosti yake, atakaa hata 2 hrs ukimpigia simu anakuwa mkali huniamini atampa na yule shoga yake simu utasikia shemeji wala usiwe na wasi wasi niko naye, Yule shosti kwa kiasi fulani alifanikiwa kumteka wife tukawa tuangombana daily, mtoto sasa haangaliwi tena, kwa 3 months hakuna amani nyumbani, Mungu mkubwa siku ya siku ilipofika shosti yake alikuwa anamtumia mtu sms akakosea akanitumia mie sms, aliandika hivi, Yule pusi anayejidai kupendwa na mmewe akafuliwa mpaka chupi za ndani sasa kwisha, kazi nimeifanya, sasa bwana anaachiwa mtoto, mwanamke nashinda naye mtaani, kazi iliyobaki ni kumwingilia yule bwana kwa maneno makali juu ya mkewe, mwisho akasema pale ndani lazima niingie, nimempa kazi Mathias adili na akataja jina la wife in full ili amlubuni walale nae tumalize mchezo. nilipoipata sms ile nikacheka sana huyo mathias alikuwa kila akija yule shosti na yeye aatajipitisha pale home kujidai anamsalimia mtoto, kumbe wana yao, sikuwa na hasira coz nilishajua mbaya ni nani. Nikamwita wife nikajifanya mnyenyekevu kweli kweli, mabusu ya hapa na pale akajifanya kachoka, nikamwambia nataka nikutoe out leo, akakubali baadaye kwa shingo upande, tukaenda coco beach. Nilimuuliza unamwamini sana yule shosti yako akaja tena juu, nikampa ile sms asome, na presha ikapanda juu ikawa sasa nauguza mgonjwa after 2 days akarudi normal. wife alilia tena kwa kwikwi, na siri zote za yule shosti nikapewa, alikuwa akimwambia wanaume mbwa kabisa hapo anajifanya kukupenda lkn HAKUNA MWANAUME MWENYE MWANAMKE MMOJA, LAZIMA ANA MWANAMKE HUKO KAZINI, ETI WIFE ALIPOKUWA KAJIFUNGUA LAZIMA NILILALA NJE YA NDOA, ETI MWANAUME HAWEZI KAA BILA KUFANYA MAPENZI. tokea hapo sasa heshima na adabu mbele na anaogopa mashosti km ukoma. So kuwa mwangalifu sana na ma shosti, Msikilize mmeo, Kingine Kama umedhamilia kuingia kwenye ndoa usibadili msimamo ukiwa ndani ya NDOA, sipendi sana huu usemi watu wanapenda kuusema eti NDOA NGUMU, ukimsikiliza mmeo na kumshauri vizuri mtafurahia ndo yenu.