TANZIA Mwanamuziki Adolf Mbinga, aka Chinga One afariki Dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wapenzi wa muziki wa dansi, wana Twanga pepeta tutakukumbuka kwa mchango wako mkubwa katika utunzi na nidhamu ya kazi wakati wote wa utumishi wako.

Utunzi wako katika wimbo wa “Kisa cha Mpemba” utabaki kumbukumbu ya wakati wote.

Mwenyezi Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi, Amina.

Mbinga alikuwa ni mmoja wa wachalaza magitaa nguli hapa nchini kuwahi kutoke, na ni mzaliwa wa mkoa wa Lindi na ndiko alikoanzia masuala haya ya muziki wa dansi.

Alianza kujulikana kimuziki kwenye miaka ya 2000 akiwa na bendi ya African Sound' "Twanga Pepeta" akiwa na akina Hamisi Amigolas.

Lwiza Mbutu, Victor Mkambi na Ally Choki na hao ni baadhi tu.

Na baadae alijiunga na bendi ya Mchinga Sound ambayo ilikuwa inamilikiwa na mheshimiwa Mohamed Mudhihir-na aling' ara pale akiwa na akina Prince Muumin Mwinjuma, Joseph Watuguru, Roshi Mselela na Michael Riloko.
IMG_20230616_044303_359.jpg

mpiga solo Adolf Mbinga
 
Kisa cha mpemba.. dah, utunzi mzuri saana.. wimbo umeanza kutiririka kichwani,nimemkumbuka na mwalimu wa walimu, ramadhani masanja.. kwenye aina ya mziki wao, bwana banza kwangu alikuwa hatati zaidi..

Wapumzike kwa amani.
 
Wapenzi wa muziki wa dansi, wana Twanga pepeta tutakukumbuka kwa mchango wako mkubwa katika utunzi na nidhamu ya kazi wakati wote wa utumishi wako.

Utunzi wako katika wimbo wa “Kisa cha Mpemba” utabaki kumbukumbu ya wakati wote.

Mwenyezi Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi, Amina.

Mbinga alikuwa ni mmoja wa wachalaza magitaa nguli hapa nchini kuwahi kutoke, na ni mzaliwa wa mkoa wa Lindi na ndiko alikoanzia masuala haya ya muziki wa dansi.

Alianza kujulikana kimuziki kwenye miaka ya 2000 akiwa na bendi ya African Sound' "Twanga Pepeta" akiwa na akina Hamisi Amigolas.

Lwiza Mbutu, Victor Mkambi na Ally Choki na hao ni baadhi tu.

Na baadae alijiunga na bendi ya Mchinga Sound ambayo ilikuwa inamilikiwa na mheshimiwa Mohamed Mudhihir-na aling' ara pale akiwa na akina Prince Muumin Mwinjuma, Joseph Watuguru, Roshi Mselela na Michael Riloko.
View attachment 2659192
mpiga solo Adolf Mbinga
Namkumbuka sana enzi za mango garden akiwa bado kijana kiasi, apumzike kwa amani
 
Tunaomba ma-manju wamuziki humu watuorodheshee nyimbo alizotunga na zile alizopiga solo guitar
 
Adolf Mbingaaaa, wapi Joseph Watuguruu maamaaa!
..atanishauri Nani mie eeh
.. atanishauri Nani miee eeeh

Roshi Msela eeh, na Kocha wa Dunia tunahudhunikaa
.. atanishauri Nani mie eeh
.. atanishauri Nani mie eeh
[emoji106]
 
Back
Top Bottom