Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Poleni sana wanafamikia ya muziki Tanzania.Wapenzi wa muziki wa dansi, wana Twanga pepeta tutakukumbuka kwa mchango wako mkubwa katika utunzi na nidhamu ya kazi wakati wote wa utumishi wako.
Utunzi wako katika wimbo wa “Kisa cha Mpemba” utabaki kumbukumbu ya wakati wote.
Mwenyezi Mungu aiweke roho yako mahali pema peponi, Amina.
Mbinga alikuwa ni mmoja wa wachalaza magitaa nguli hapa nchini kuwahi kutoke, na ni mzaliwa wa mkoa wa Lindi na ndiko alikoanzia masuala haya ya muziki wa dansi.
Alianza kujulikana kimuziki kwenye miaka ya 2000 akiwa na bendi ya African Sound' "Twanga Pepeta" akiwa na akina Hamisi Amigolas.
Lwiza Mbutu, Victor Mkambi na Ally Choki na hao ni baadhi tu.
Na baadae alijiunga na bendi ya Mchinga Sound ambayo ilikuwa inamilikiwa na mheshimiwa Mohamed Mudhihir-na aling' ara pale akiwa na akina Prince Muumin Mwinjuma, Joseph Watuguru, Roshi Mselela na Michael Riloko.
View attachment 2659192
mpiga solo Adolf Mbinga
Kuna taarifa zinasema marehemu alikuwa anaumwa na akazidiwa akarejeshwa nyumbani.
Ni jambo jema tukafahamu, wasanii wengi wanakuwa wahanga kijamii kwa sababu hakuna sheria nzuri zinazolinda maslahi yao pindi wanapokuwa nje ya game. Wengi wanakufa masikini na dhalili kabisa.
Inawezekana ndugu yetu angepata matibabu sahihi endapo angekikuwa na fedha ya kutosha. Kuna wakati tusimsingizie Mungu kwa mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu.
Mungu ampokee mja wake