TANZIA Mwanamuziki mkongwe, Said Mabera afariki dunia

TANZIA Mwanamuziki mkongwe, Said Mabera afariki dunia

Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.


Hii ni safu iliyokoga mioyo ya wapenzi wa muziki asilia wa kitanzania, Mungu amlaze pema SM
 
Mebera ndiye aliyemleta Hassan Rehan Bitchuka kweye band ya NUTA wakati huo Bitchuka alikuwa bado mdogo sana kiumri na wote wakawa wanamwita "bwana mdogo"
Nakubaliana na wewe kuwa Marehemu Mabera ndio aliemleta Bitchuka Nuta. Sawa kabisa!!! Nuta pia kulikuwa na kijana mwingine mpiga gitaa la Rhythm akiitwa Abdallah "Dulla" Omar ambaye kwenye nyimbo kadhaa utamsikia Bitchuka akimwita, hususan wimbo wa Mume Wangu utamsikia Bitchuka akisema ahsante sana Bwana Mdogo kwa jinsi kijana yule alivyokuwa analicharaza gitaa la Rhythm. Nyimbo nyingi za wakati ule mfano mzuri ule wa Nidhamu ya Kazi ukiusikiliza utasikia kazi ya bwana mdogo huyo.
Tuwa Enzi hawa wazee wetu walifanyakazi nzuri sana. Pia nimeona kwenye mitandao Mzee Kikumbi Mwanza Mpango "Kikki" mgonjwa tumwombee Mzee wetu huyu mwingine afya njema.
 
Miongoni mwa binadamu mlioletwa duniani kwa kusudi la kutoa huduma.
Hukupenda kunyenyekewa bali mwenyewe ulikuwa myenyekevu.
Ulikuja duniani kwa lengo la kuburudisha waliochoka na walio na msongo wa mawazo, lakini ukajipa wajibu mwingine wa kuonya, kufundisha na kutahadharisha.
Nenda Mabera, nenda baada ya kutekeleza vema ulichojaliwa na Mungu. Wafuate wenzio waliozitendea haki karama zao za burudani;
Gerry Nashon "Dudumizi",
Hemed Manet " Chiriku",
Moshi William "Tx"
Mbaraka Mwinshehe,
Abdalla Gama,
Remmy Ongalla "Dr"
Mohamed Kipande,
Abdalla Mgonahazelu,
Muhidin Ngurumo "Maalimu"
Seleman Mbwembwe,
Athman Momba,

Amen!!!!
 
Daah imeniuma sana sana!! Mm nipo mkoana huja Dar Mara kwa Mara
Nikija lazima niwaone hawa wakongwe wenye tungo muruwaaa kweli msondo famili tumeumia sana
Kwaheri Dr
 
Ameitumikia Msondo kwa miaka 47
Kuanzia
NUTA
JUWATA
OTTU
Kwa mtindo ule ule wa Msondo
 
Naomba mwenye kujua jina la wimbo alioimba Selemani Mbembwe wenye kibwagizo kifuatacho; bwana ee e hali hii mpaka lini nasema, ukiamka na shida za leo na za kesho zinakungoja'"
 
Joseph Lusungu,huyu ndie Mwanzilishi wa Msondo Ngoma.
Bishuu
Mnenge Ramadhan
Said Mabera
Kitambi
Makosa
Maasadi
Ridhiwani Mpangamawe "Totoo"
Zahoro Bangwe
Selemani Mwanyiro "Internet"
Roman Mng'ande "Romario"
Hamis Said Mnyupe
Ally Rashid "Marashi ya Zanzibar"
Muhidin Gurumo "Kamanda"
Moshi William "TX Moshi"
Joseph Maina
Othman Momba
Rehan Bitchuka
Seleman Mbwembwe
Buyungwa
 
Naomba mwenye kujua jina la wimbo alioimba Selemani Mbembwe wenye kibwagizo kifuatacho; bwana ee e hali hii mpaka lini nasema, ukiamka na shida za leo na za kesho zinakungoja'"
Yeyote mwenye kujua huu wimbo alioimba Selemani Mbwembwe anisaidie jina lake jamani. nimejaribu kutafuta jina la huo wimbo muda mrefu kidogo na sehemu mbali mbali bila mafanikio.
 
Back
Top Bottom