Nitakwenda na naani msondo ngooma, nitacheza na nani magoma kitakita.
Kalale mahali pema .
Athumani Momba,
Selemani Mbwembwe,
Maina,
TX Moshi William,
Muhidin Maalim Ngurumo na leo
Said Mabera.
Nakubaliana na wewe kuwa Marehemu Mabera ndio aliemleta Bitchuka Nuta. Sawa kabisa!!! Nuta pia kulikuwa na kijana mwingine mpiga gitaa la Rhythm akiitwa Abdallah "Dulla" Omar ambaye kwenye nyimbo kadhaa utamsikia Bitchuka akimwita, hususan wimbo wa Mume Wangu utamsikia Bitchuka akisema ahsante sana Bwana Mdogo kwa jinsi kijana yule alivyokuwa analicharaza gitaa la Rhythm. Nyimbo nyingi za wakati ule mfano mzuri ule wa Nidhamu ya Kazi ukiusikiliza utasikia kazi ya bwana mdogo huyo.Mebera ndiye aliyemleta Hassan Rehan Bitchuka kweye band ya NUTA wakati huo Bitchuka alikuwa bado mdogo sana kiumri na wote wakawa wanamwita "bwana mdogo"
Miongoni mwa binadamu mlioletwa duniani kwa kusudi la kutoa huduma.
Hukupenda kunyenyekewa bali mwenyewe ulikuwa myenyekevu.
Ulikuja duniani kwa lengo la kuburudisha waliochoka na walio na msongo wa mawazo, lakini ukajipa wajibu mwingine wa kuonya, kufundisha na kutahadharisha.
Nenda Mabera, nenda baada ya kutekeleza vema ulichojaliwa na Mungu. Wafuate wenzio waliozitendea haki karama zao za burudani;
Gerry Nashon "Dudumizi",
Hemed Manet " Chiriku",
Moshi William "Tx"
Mbaraka Mwinshehe,
Abdalla Gama,
Remmy Ongalla "Dr"
Mohamed Kipande,
Abdalla Mgonahazelu,
Muhidin Ngurumo "Maalimu"
Seleman Mbwembwe,
Athman Momba,
Pangamawe RidhiwaniDuh, nikijaga bongo huwa sikosi Msondo Kisuma.
Sijui brotherman gani atarithi mikoba.
Rest in Peace Said Mabera.
Ametutoka alfajiri ya kuamkia leo kwa Maradhi ya muda mfupi
Alikuwa Kiongozi wa bendi ya Msondo Ngoma na atapumzishwa leo saa 10 Maeneo ya GobaView attachment 1584342
Romariiiii mzee wa bazeeee!!Mabeee mabeee mabela yaani jamaa mvumilivu sana amekaa msondo miaka mingi sana
Yeyote mwenye kujua huu wimbo alioimba Selemani Mbwembwe anisaidie jina lake jamani. nimejaribu kutafuta jina la huo wimbo muda mrefu kidogo na sehemu mbali mbali bila mafanikio.Naomba mwenye kujua jina la wimbo alioimba Selemani Mbembwe wenye kibwagizo kifuatacho; bwana ee e hali hii mpaka lini nasema, ukiamka na shida za leo na za kesho zinakungoja'"