Mwanamuziki Msami akiri kuwa mpenzi wa Uwoya, azungumzia tofauti ya umri na mipango yao

Mwanamuziki Msami akiri kuwa mpenzi wa Uwoya, azungumzia tofauti ya umri na mipango yao

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
qw1.JPG

Mkali wa Sound Track ambaye pia ni mkali wa kuvunja (dancer) amezungumzia uhusiano wake na muigizaji mrembo wa Bongo Movies, Irene Uwoya.

Akiongea na tovuti ya Times Fm, Msami alizunguka sana mbuyu kutaka kutoa maelezo kuhusu ukweli wa mambo kati ya wawili hao lakini kwa mara ya kwanza aliamua kuiambia tovuti ya Times Fm kauli yake kutokana na jinsi alivyoulizwa.

"Kaongea kwa upole huyu jamaa, kaapproach ili apate jibu. Ni kweli (kicheko)…nimekuridhisha lakini, nimeamua kukuridhisha." Amesema Msami..

Muonekano wa Irene Uwoya na Msami kwa muonekano uliwafanya wengi wazungumze kwenye mitandao ya kijamii kuwa Msami amegeuka Serengeti Boy kwa Uwoya ambaye wanaamini anamzidi sana umri. Lakini ukweli ni kwamba Msami ni mkubwa kwa Uwoya. Chukua hiyo!

"Unajua mimi mwanzo, Serengeti Boy nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani. Yaani ile deeply nilikuwa sina tafsiri yake kabisa yaani. Kwa hiyo leo ndio nimepata tafsiri yake ‘Serengeti Boy' kumbe ni mtu ambaye amezidiwa umri. Tofauti na mimi nilivyokuwa nawaza kuhusu Serengeti Boy.

"Lakini mbona nikasema kama ni hivyo, as we are best friends lakini (joke), lakini mbona mimi nimemzidi umri Uwoya. Lakini mimi ni mkubwa kwake sema yeye ananizidi umri. Mimi ni mkubwa kwake nimemzidi miezi mingi…yaani wewe jua nimemzidi miezi mingi. Mimi ni mkubwa kwa Uwoya." Alisisitiza Msami

Katika hatua nyingine, Msami ameeleza mpango wake na Uwoya kutoa filamu ya pamoja na jinsi filamu itakavyokuwa.

Amesema katika filamu hiyo yeye ndiye mhusika kuu na kwamba ni filamu ambayo itahusisha dance na muziki. Filamu hiyo itatoka mwaka huu lakini bado haijapata jina rasmi na tarehe ya kutoka.

"Movie inakuja very soon, watu wakae tayari." Amesisitiza.

Chanzo: bongomovies.com
 
Wewe uliyeleta hii habari wa kike au wakiume?
Never mind ....................................:A S-eek::A S-eek:
 
Mtu na mutoto yakeeeee ukishangaa ya Nuhu utayaona ya Msamii
 
Eeeh Dida leo kasema angekuwa mtoto mbona akienda chooni anafunga mlango?
Mbona hasemi ataka jojoaaaa.....hahahaaa nimecheka sana leo...

Hhhhhhaaaa timu dogo dogo lazima atetee
 
"Lakini mbona nikasema kama ni hivyo, as we are best friends lakini (joke), lakini mbona mimi nimemzidi umri Uwoya. Lakini mimi ni mkubwa kwake sema yeye ananizidi umri. Mimi ni mkubwa kwake nimemzidi miezi mingi…yaani wewe jua nimemzidi miezi mingi. Mimi ni mkubwa kwa Uwoya." Alisisitiza Msami
Ukitaka ku-anticipate umri wa wasanii wetu basi waambie wanamegwa na vibabu! Bi Shost atakuambia... hamna bwana, maneno ya watu tu hayo; wala hatujapishana sana... yule ana miaka 38 mimi n'na miaka 32... yaani keshasahau kwamba alikuwa anadai she's 26!
 
Eeeh Dida leo kasema angekuwa mtoto mbona akienda chooni anafunga mlango?
Mbona hasemi ataka jojoaaaa.....hahahaaa nimecheka sana leo...
Sio mambo ya kulilia manyonyo tena?!!? Kwa mbaaaaaaaaaali naona kama wanaelekea kwenye swali la msingi: "Ka mtoto mbona akiiiona hafumbi macho kuiogopa?"
 
Sio mambo ya kulilia manyonyo tena?!!? Kwa mbaaaaaaaaaali naona kama wanaelekea kwenye swali la msingi: "Ka mtoto mbona akiiiona hafumbi macho kuiogopa?"

Hahahaa tena kasema kama mtoto angekuwa anasoma primary au bado angekuwa anaenda clinic, kama kote huko kapita basi mtu mzima huyooo....

Akasema mtu akidate mtu mzima utasikia oooh mzee, babu, Mtu mzima kwani anavunja nazi kwa ugoko? anapiga danadana kwa kisu, au anaoga katikati ya ikuluuu???? Hahahaaa mzee kwani namshikia mkongojo....

Kasema waacheni watu wapendane....
 
Back
Top Bottom