TANZIA Mwanamuziki Waziri Sonyo afariki dunia

kitonsa

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2011
Posts
1,211
Reaction score
2,649


Mwanamuziki aliyewahi kuimba kwenye bendi ya Chuchu sound na TOT Plus, Waziri Sonyo ameaga dunia jana tarehe 23 Februari saa moja usiku maeneo ya Kibaha.

Chanzo cha kifo hakijawekwa wazi ingawa kuna taarifa kuwa alikwenda kutazama mechi ya mpira wa miguu na aliporudi alijipumzisha hadi mauti yalipomkuta



Taarifa nimezipata katika kipindi cha afro tizi cha Rajabu Zomboko radio one, usiku huu
 
Mwanamuziki aliyewai kuimba chuchu sound na tot plus waziri sonyo ameaga dunia Leo SAA moja usiku maeneo ya kibaha

Chanzo cha kifo hakijawekwa wazi

Taarifa nimezipata katika kipindi cha afro tizi cha rajabu zomboko radio one, usiku huu

Duuh kumbe unasikiliza kipindi, ndo Zomboko anaaga hapa na wana Tukunyema kibao cha Sophia. Nami nimesikia hapa
 
Duuh kumbe unasikiliza kipindi, ndo Zomboko anaaga hapa na wana Tukunyema kibao cha Sophia. Nami nimesikia hapa
sikosagi mkuu nyimbo za zomboko nilivyo kuwa mdogo wazazi na mabro walikuwa wakizisikiliza nilikuwa sizipendi,
Nashangaa nimeanza kuzipenda kipindi hiki kinoma,,,,sijui nimekuwa mzee?
 
Huo mpira uliishaje? Labda timu yake haikufanya vizuri.
Nakumbuka huyu dogo alipokua na Komba na Banza stone walivyokua wanajitutumua kujilinganisha na African stars miaka Ile ya 2002 2006 lkn African stars walikua wamewaacha TOT kwa mbaali sana.
 
Basi mijitu itaanza, ooh, tuchukue tahadhari, ni mwaka upi watu hawakufa?
Huwa ninahisi na najiuliza hivi misiba ndio inayokupa hela? Au biashara unayofanya inahusika na misiba? Mfano, biashara ya majeneza, misalaba ya makaburi, granite za makaburini, maua ya msibani, mabasi ya msibani, magari ya kubeba majeneza,n.k. Maana yaani vifo kwako wewe fresh tu maana unaingiza hela ndefu. Ila daah basi tu!
 
Poleni ndugu,jamaa na marafiki.

Taratibu ni zile zile hazijabadilika ,tufuate miongozo iliyotolewa na wataalamu.
Huyu jamaa alikuwaga jambazi aliiba pikipiki.

Kina Joti walimuigiza kwenye kile kipindi chao amefulia. Wakuvanga alimuigiza kama yeye ameva 'kauwoshii' huku akikimbia na 'kuruka ukuta' joti akimdhihaki vibaya sana.
 
Huyu jamaa alikuwaga jambazi aliiba pikipiki.

Kina Joti walimuigiza kwenye kile kipindi chao amefulia. Wakuvanga alimuigiza kama yeye ameva 'kauwoshii' huku akikimbia na 'kuruka ukuta' joti akimdhihaki vibaya sana.

Noma sana kweli kweli.
 
Huyu Rajab Zomboko ana uhusiano wowote na miss zomboko wa JF?
 
R.I.P tuwasaidie kujikinga na kuwakinga wote waliopo kwenye kundi hatarishi :NB nani anakumbuka sigara ya sonyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…