JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Getrude akizungumza na GADI TV amesema yeye na ndugu zake waliitwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo na walipofika alishurutishwa atoe cheti hicho mbele ya dada yake ambaye anadaiwa alihusika na mauaji ya mama huyo kwa tamaa za kutaka eneo la ardhi kwa muda mrefu.
Aidha, Getrude amesema baada ya kukosa maelezo ya kutosha kuhusiana na cheti hicho aligoma kukitoa akiwa na hofu na dada yake hali iliyopelekea mkuu huyo kusimama na kumzaba kofi sehemu ya begani huku akimtolea lugha zisizo za staha.
Katika mahojiano ya mkuu wa wilaya hiyo ndugu Kaji na moja ya chombo cha habari akijibu tuhuma hizo amesema kutokana na kesi inayoendelea kuhusiana tuhuma za mauaji hayo ilihitajika cheti hicho na kuhusu kumpiga mwananchi huyo kofi ameshauri aende mahakamani.
Chanzo: GADI TV