Mwananchi: Kashfa nzito "michoro ya ZOMBI amesahau viatu & Mess"

Mwananchi: Kashfa nzito "michoro ya ZOMBI amesahau viatu & Mess"

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
Kashfa nzito

"wanafunzi walichora vekaragosi, yakiwemo matusi, mashairi ya bongo fleva, na wengine kuandika kuhusu mapenzi"
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweza kukumbwa na kashfa kubwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya 2012 yaliyotangazwa juzi na Waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa.

Kashfa hiyo inatokana na aina ya majibu yaliyoandikwa na baadhi ya watahiniwa katika mitihani hiyo, huku wengine wakikusanya vitabu vya majibu bila kujibu chochote, hali inayohusishwa na uhaba mkubwa wa walimu katika baadhi ya shule za sekondari nchini.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako alisema wasahihishaji walikutana na mambo ya ajabu yakiwamo matusi, michoro ya vitu visivyoeleweka, mashairi na nyimbo za muziki wa kizazi kipya (bongo fleva).

“Mwaka jana tulikutana na ‘single’ yaani waliandika mashairi kwa uchache, lakini mwaka huu tumepata albamu nzima… ni vituko vitupu, wengine wanaandika mapenzi, mwanafunzi anatumia ukurasa mzima kumlalamikia mpenzi wake. Miongoni mwa yaliyoandikwa ni mpenzi, umeniacha, natamani kunywa sumu, usiku silali nakuwaza wewe…” alisema Dk Ndalichako.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Ndalichako alisema wanafunzi wengine waliandika malalamiko dhidi ya wabunge na uendeshaji wa Bunge.

“Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu anaandika… nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua, wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au viwanjani…” alisema.

Alisema wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka walikuwa ni wengi na walichangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya.

Dk Ndalichako alionyesha baadhi ya michoro hiyo ambayo inaonyesha vikaragosi ambavyo wanafunzi hao waliviita Messi (Lionel, mchezaji wa Barcelona) na zombi (ni picha za kutisha) ambazo huonyeshwa kwenye televisheni.

Sababu za kufeli
Dk Ndalichako alisema hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja juu ya kwa nini matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya, lakini akadokeza kuwa huenda yametokana na wanafunzi wengi kukosa maarifa.

Anasema mbali na waliojaza matusi na michoro, wanafunzi wengine waliofanya vibaya ni wale ambao hawakujaza chochote kwenye karatasi zao za majibu.

“Kuna baadhi ya shule unakuta darasa zima watoto hawajajibu somo fulani kwa mfano Biolojia, wanaingia tu na kuandika namba. Tuliamua kuwapigia simu walimu wao, majibu waliyokuwa wakitupa ni kuwa hawajawahi kuwa na walimu wa somo husika kwa hiyo watoto hawakuwa na cha kujaza.”

Dk Ndalichako alisema kwa ku mbukumbu zake, hakuna matokeo mabaya kama ilivyo kwa mwaka huu yaliyowahi kutokea.

“Tukiangalia tu kuanzia 2000, hakujawahi kutokea matokeo mabaya kama haya, kwa kweli hali haipendezi. Hata kabla ya kuyatangaza nilikuwa nayaangalia mara tatu tatu, sikuyapenda na inasikitisha kwa kweli,” alisema Dk Ndalichako.

by: Mwananchi: mwanzo - Gazeti la habari za kiswahili la kila siku Tanzania, linaongoza
 
Hii ibaweza kuwa trela kama serikali itaendeleza siasa na hasa kutoshughukikia madai ya walimu na kuwapa motivationi walimu wanaoishi katika mazingira magumu ili waende mpaka vijijini na kufundisha hatimaye elimu kupanda.
 
mitaala tu hamna

walimu hamna

waliopo mshahara kiduchu

mnajisifia kujenga shule zisizo na walimu......

 
Kwa kweli hii ni mwisho kabisa ya kuididimiza serikali mbaya legelege ya jk na kabinet yake yote!
 
sasa mtoto hajui biology ,hajawai kusikia toka form one hilo neno leo unamletea mtihani ajibu nini?
aote ?



Smile;

Nakwambia kuwa mpole na majibu utayapata na hii serikali inayojilimbikiza trilioni moja kila mwezi na watajutia!
 
Last edited by a moderator:
Smile;

Nakwambia kuwa mpole na majibu utayapata na hii serikali inayojilimbikiza trilioni moja kila mwezi na watajutia!
hakuna majibu hapa,watoto wenyewe hawajui kusoma wala kuandika ,hawana walimu hawajawai kufundishwa lolote.jinsi walivowafaulisha la saba bila kujua kusoma na kuandika basi wawapitishe kwenda a level kwa jinsi ile ile
 
Ushauri wangu kwa hii Serikali ni bora ya kuwa na watu wachache wenye elimu inayowasaidia kukabiliana na changamoto za maisha kulikuwa kuwa na kundi kubwa linalojiona wamesoma wasiokuwa na mbinu za kukabiliana na changamoto za maisha.
 
sasa mtoto hajui biology ,hajawai kusikia toka form one hilo neno leo unamletea mtihani ajibu nini?
aote ?
Tatizo siasa zinazofanywa kwenye matokeo ya darasa la saba na form 2 wakati wenzao wa NECTA wapo kikazi zaidi na hawataki masihara, kuna watu ambao hawakustahili kufika huko form4 sioni ajabu kwa majibu hayo,kama mtu anaingia form1 hajui kusoma na kuandika unatarajia nini, kama wanafunzi wangekuwa wanajiweza huo muda wa kusoma mashairi wangekuwa wanasoma kiswahili walau wapate C wasingepata ziro
 
Yaani leo nimechaka hadi basi, baada ya kusikia baadhi ya wanafunzi wameuliza maswali badala ya kujibu. 'eti unaniuliza mimi swali la historia ya mwaka 1800 au 1902 wakati mimi nimezaliwa mwaka 1993? Mimi natajuaje?'
Wataalamu wa histori hebu jibuni hoja ya watoto wenu.
 
matokeo mabaya ya message kwa serikali. Nayo ni kupiga marufuku tuition. uhaba wa wawalimu mikoani unatokana na walimu wengi kuja Dar kufundisha tuition.
 
Waalimu wana mazingira magumu kiufundishaji, wanafunzi wenyewe nao tatizo pia.... Serikali yaweza kua chanzo kikubwa cha kufeli kwa wanafunzi wa kidato cha nne, ila naamini na hao wanafunzi nao ni tatizo maradufu.

Watoto hawaoni shida kuandika mambo ya ajabu kwenye mtihani, nidhamu ya kiuanafunzi imeenda wapi? kuchora vikatuni imekua kama fashion sasa? nalo hili ni sera za serikali au wadogo zetu elimu hawaitilii maanani?

Sio mara moja nimekutana na watoto wa sekondari au msingi wakibishana kuhusu ELIMU na PESA, ujasiri wa kubishania hivi vitu viwili nakumbuka haukuwepo miaka ya nyuma. utawasikia wakiambiana kwani wasoma ili nini? tatizo haliko kwenye serikali tu, wadogo zetu hawaoni maana ya elimu kama hapo miaka ya 90.
 
Hao ndio CCM bana, wanahakikisha kila mwanafunzi anaenda shule na kila mwanafunzi anatoka bila kitu kichwani. Ndio maana wahitimu wa vyuo wa miaka hii kichwani hovyo kabisa.

Leo wamechora vikaragosi, wanapenya kimtindo kesho wanavuvia madesa, mwisho wa mwaka majoho, wako kazini.
 
watoto wa siku hizi mazuzu pia au hlo hamlioni?

Mkuu sio watoto, hata wazazi mazuzu, ndani ya daladala utakutana na tubinti tuchafu twa maadili utafikiri hatukai na wazazi. Hivi mtoto wa shule ameweka nywele dawa, mkononi ana gazeti la UDAKU (hapa najua namuudhi EMT) na ana simu mbili. Wazazi utafikiri hawamuoni.
 
Last edited by a moderator:
hali ni ngumu... ila inahitaji kuwa na mjadala wakuangalia elimu yetu.. kwa ushauri wangu pia hasa kwa shule za kata hizi ni wazazi na kata husika kuzimiliki kwa maana kuziangalia kwa makini na kujitolea kuangalia maslahi ya walimu wao.
 
matokeo mabaya ya message kwa serikali. Nayo ni kupiga marufuku tuition. uhaba wa wawalimu mikoani unatokana na walimu wengi kuja Dar kufundisha tuition.
Hao wanafunzi wa kusoma hizo tuition miaka hii wako wapi wangekuwa wanazisoma hizo tuition wasiandika habari za mashairi ya mapenzi, tena kutokana na uhaba wa walimu wangezitumia hizo tuition vizuri zingewasaidia sana ili kupata angalau cha kujibu, kuliko kuchora messi kwenye mtihani, ila ukianzisha tuition za facebook,bongofleva na mapenzi utapata wengi sn
 
Back
Top Bottom