Mwananchi: Kashfa nzito "michoro ya ZOMBI amesahau viatu & Mess"

Mwananchi: Kashfa nzito "michoro ya ZOMBI amesahau viatu & Mess"

Mfumo wa elimu ni wa kiboya sana...... Shule za kata zifutwe zifundishe ufundi stadi labda itawasaidia wadogo zetu or else ni majanga juu ya majanga kwenye sekta ya elimu Tanzania.
 
hali ni ngumu... ila inahitaji kuwa na mjadala wakuangalia elimu yetu.. kwa ushauri wangu pia hasa kwa shule za kata hizi ni wazazi na kata husika kuzimiliki kwa maana kuziangalia kwa makini na kujitolea kuangalia maslahi ya walimu wao.

Kabisa.
Inatakiwa hili suala la elimu ya taifa letu iwe mjadala wa kitaifa, tutafute utatuzi wa kudumu wa shida hii. Porojo za akina Kawambwa bungeni haziwezi kutupeleka popote kwenye utatuzi wa matatizo yanayoikabili sekta hii muhimu!
 
watoto wa siku hizi mazuzu pia au hlo hamlioni?

Nakubaliana nawe, yaani sijui nitumie neno gani badala ya hilo ulowaita. Yaani watoto hata commitment na shule hamna, shughuli za nyumbani wazito, udadisi ndo hivyo! Wazazi kazi ipo.
 
Nina uhakika wangeeambiwa wachore Bunsen Burner wangeishia kuchora viungo vyao vya Uzazi....
CC: zumbemkuu
MANI

Mpwa hiyo bunsen burner mbona uanawapa neno gumu sana na sidhani kama wameshaiona kwa shule zetu hizi za sasa!
 
Wazazi bongofleva na vizazi vya kiduku tukubali, mmomonyoko wa maadili na malezi finyu vinapelekea usinyaa wa akili na fikra finyu! HATUJITAMBUI SISI, WATOTO WETU WATAJITAMBUA VIPI?
 
Mkuu sio watoto, hata wazazi mazuzu, ndani ya daladala utakutana na tubinti tuchafu twa maadili utafikiri hatukai na wazazi. Hivi mtoto wa shule ameweka nywele dawa, mkononi ana gazeti la UDAKU (hapa najua namuudhi EMT) na ana simu mbili. Wazazi utafikiri hawamuoni.

Yea, halafu wakati huo huo "Kuna baadhi ya shule unakuta darasa zima watoto hawajajibu somo fulani kwa mfano Biolojia, wanaingia tu na kuandika namba. Tuliamua kuwapigia simu walimu wao, majibu waliyokuwa wakitupa ni kuwa hawajawahi kuwa na walimu wa somo husika kwa hiyo watoto hawakuwa na cha kujaza." - source Ndalichako

Kama huko mashuleni hawana hata walimu wala vitabu kwa nini wasiishie kusoma magazeti ya udaku, kuweka nywele dawa na kuchati kwenye simu?
 
Na wazazi/ walezi hatuna muda wa kufuatilia maendeleo ya watoto wetu. Hata mimi shule niliyosoma hatukuwa na walimu wa kutosha, lakini tulifanya vizuri kupitia discussion na wanafunzi waliokua wana walimu. Watoto wetu wanahitaji msaada wetu wa kimalezi pia. Kuandika bongo fleva inahusiana nini na kukosa walimu wa kutosha?
 
watoto wa siku hizi mazuzu pia au hlo hamlioni?
napingana na wewe kabisa !si mazuzu -wamendika vikaragosi,mashairi na upuuzi mwingine kwa kuwa wameletewa mitihani juu ya mambo ambayo HAWAJAWAHI KUFUNDISHWA!!!!!
Tena vitoto vya siku hizi ni vijanja kuliko unavyofikiri wala hawachezi michezo yetu ya zamani-" kariri utaelewa baadaye"
 
Mimi bado siamini. Najua mimi na wewe tumepita huko, na wala sio jambo la ajabu kwenye mtihani kukutana na jambo ambalo ama ulijui au umesahau ndio maana ukaitwa mtihani. Je kwenye hali hiyo ulikua unaandika matusi au bongo fleva kwenye answer sheet? Kuna shida nyingine kubwa tu na watoto wa siku hizi
 
Kashfa nzito

“Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu anaandika… nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua, wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au viwanjani…” alisema.

................denti huyu anayoakili sema mfumo tu umemuharibia maisha

Siyo utani dogo ana uewelewa wa hali ya juu kabisa, kama anaweza kuliona hilo yupo juu.
 
“Kuna baadhi ya shule unakuta darasa zima watoto hawajajibu somo fulani kwa mfano Biolojia, wanaingia tu na kuandika namba. Tuliamua kuwapigia simu walimu wao, majibu waliyokuwa wakitupa ni kuwa hawajawahi kuwa na walimu wa somo husika kwa hiyo watoto hawakuwa na cha kujaza.”

Duuh!

Halafu unataka vipi kulaumu wanafunzi hawasomi hapo?
 
602031_10151434863309339_167670344_n.jpg

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako akionyesha karatasi ya majibu ya mmoja wa watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2012, Dar es Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
 
Kuna Zombie wimbo/ album ya Fela Anikulapo Kuti alipokuwa akikebehi uongozi wa kijeshi/kisiasa pamoja na wanajeshi wa Nigeria.

Labda wanafunzi wana hasira na uongozi kwa kutowapatia walimu na kuwafanya wajue cha kujaza kwenye mtihani.

Wanabaki kuubeza uongozi wetu kuwa ni "Zombies". Unapelekwa pelekwa tu bila kujielewa.

Lyrics http://www.lyricsmania.com/zombie_lyrics_fela_kuti.html

Last edited by a moderator:
Mimi bado siamini. Najua mimi na wewe tumepita huko, na wala sio jambo la ajabu kwenye mtihani kukutana na jambo ambalo ama ulijui au umesahau ndio maana ukaitwa mtihani. Je kwenye hali hiyo ulikua unaandika matusi au bongo fleva kwenye answer sheet? Kuna shida nyingine kubwa tu na watoto wa siku hizi

Ndugu yangu hilo nalo neno!i am taking back my earlier post versus yours.
 
tatizo siasa zinazofanywa kwenye matokeo ya darasa la saba na form 2 wakati wenzao wa necta wapo kikazi zaidi na hawataki masihara, kuna watu ambao hawakustahili kufika huko form4 sioni ajabu kwa majibu hayo,kama mtu anaingia form1 hajui kusoma na kuandika unatarajia nini, kama wanafunzi wangekuwa wanajiweza huo muda wa kusoma mashairi wangekuwa wanasoma kiswahili walau wapate c wasingepata ziro
yani utashangaa form six wa saivi hajui chchte mpk aibu. Unabaki kujiuliza kafikaje apo alipo
 
Back
Top Bottom