Wananchi katika kikao kilichofanyika Septemba 4, 2026 cha ushauri Wilaya ya Mpanda (DCC) wamehoji sababu ya umeme ndani ya Manispaa ya Mpanda kila inapofika Saa 11 Jioni na Saa mbili usiku umeme hukatika na kukaa gizani ili hali Mkoa wa Katavi hivi sasa umeunganishwa na Gridi ya Taifa.
Afisa Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Katavi, Mary Ngole akijibu hoja hiyo amesema ongezeko la matumizi ya umeme husababisha transfoma kuzidiwa wakati huo wa Saa 11 Jioni na Saa 2 Usiku, hivyo TANESCO hulazimika kufanya mgao kwa maelekezo kutoka makao makuu ya TANESCO.