Mwananchi: Sisi hatujui kabisa Kondomu na hatujui maana yake

Mwananchi: Sisi hatujui kabisa Kondomu na hatujui maana yake

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
418
Reaction score
550
Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Kondomu jana Februari 13, 2026, imebainika kuwa bado kuna changamoto ya uelewa kuhusu matumizi sahihi ya kondomu, huku takwimu zikionesha kushuka kwa matumizi kwa asilimia tano nchini.

Licha ya jitihada zinazoendelea za Serikali ya kuimarisha utoaji wa elimu ya kinga, hususan kwa Vijana ili kuzuia kuingia kwenye ngono katika umri mdogo na kupunguza maambukizi mapya ya VVU, bado wadau wa afya wanasema elimu zaidi inahitajika, hasa katika maeneo ya vijijini.

Akizungumza, mmoja wa Wananchi wa Jamii ya Wamaasai ambaye ni Mkazi wa Dodoma, amesema pamoja na kampeni mbalimbali zinazoendelea, bado hawatumii kondomu na wanaamini kwamba kwa kutumia kondomu ndio watapata maambukizi ya magonjwa

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NASHCoP), Dkt. Boniface Silvan, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali katika maadhimisho hayo, amewataka Watanzania kuzingatia matumizi sahihi na endelevu ya kondomu pamoja na njia nyingine za kinga, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu katika kulinda afya binafsi na jamii kwa ujumla.

Aidha Mratibu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Kanda ya Kati, Eriko Kawanga, amesema Tume inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya ili kuhakikisha maambukizi mapya ya VVU, homa ya ini pamoja na mimba zisizotarajiwa yanapungua kwa kiwango kikubwa.


 
Wamerekani watu wabaya sana wametuletea ugonjwa wa ukimwi Ili wafanye biashara ya kutuuzia kondom na ARV
 
Back
Top Bottom