DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Jana Oktoba 2,,2025 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea vituo vya mabasi ya Mwendokasi vya Kivukoni na Kimara kukagua utoaji wa huduma na kuzungumza na wananchi.
Akiwa Kivukoni, alikutana na changamoto ya wafanyabiashara wa samaki waliodai wamezuiwa kupakia bidhaa zao kwenye mabasi mapya. Walisema hali hiyo inawapa ugumu wa kufikisha samaki sokoni.
Majaliwa alimuelekeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, akae na wafanyabiashara hao ili kutafuta suluhu, ikiwemo kuangalia njia ya kufunga mizigo yao au kutumia utaratibu mwingine. Alisisitiza kuwa changamoto hiyo lazima ipatiwe ufumbuzi mapema.
Ziara hiyo ilihitimishwa Kimara, ambapo Waziri Mkuu alitaka mabasi mapya yaendelee kutoa huduma bora na salama kwa wananchi.
Pia Soma: Mabasi mapya ya Mwendokasi ya MOFAT yaanza kubeba Abiria Gerezani–Mbezi