Mwananchi ungeambiwa kuchapa kiongozi kiboko, ungemchapa nani na kwa sababu zipi?

Mwananchi ungeambiwa kuchapa kiongozi kiboko, ungemchapa nani na kwa sababu zipi?

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2020
Posts
1,809
Reaction score
1,692
Wanabodi, Heri ya mwaka mpya wa 2021!

Nimekaa kwa muda nikitafakali, kujiuliza na kutafuta majawabu kuhusu mienendo ya viongozi kuwachapa bakora wananchi kufuatia tuhuma mbalimbali dhidi ya wachapwaji.

Huenda viongozi hao wana sababu za msingi au hawana - wengine huwachapa bakora wakosaji kwa provocation, wengine hufanya hivyo waonekane miamba, na wengine wameenda mbali mpaka wanaadhibu kwa push-ups watumishi jeshini kama Dkt Kigwangala nk.

SASA
Wewe mwananchi kama ungekuwa na mamlaka ya kuwachapa bakora viongozi au watawala ungemchapa nani na kwa sababu zipi?

= Ungemchapa kiongozi kwa kuwa ameshindwa kukufikishia maji kijijini?

= Ungemchapa kwa kuwa ameshindwa kuwa mbunifu wa vyanzo vya mapato ya Halmashauri / Wilaya?

= Ungemchapa kwa kuwa kijana wako kakosa mikopo ya elimu ya juu?

= Ungemchapa yupi sababu ya vijana wetu kukosa ajira katika vijiji, kata na wilaya?

Mwisho, nashauri viongozi wauweke pembeni utamaduni wa kuwachapa watu bakora na baada yake wajielekeze kwenye Sheria.

******** **********
Nimegundua kuwa wengi wetu hatuna sababu mahususi za kulaumu wale wanaochapa bakora - lkn pia wengi wetu tunasukumwa na kasumba ya visasi - kwa nini umcharaze mwenzako bakora?
 
Nashauri viongozi waendelee kucharaza viboko maana huu uzi machadema wote wamesema watachapa viongozi bakora HAKUNA hata mmoja anayesema ni kinyume na Sheria.
 
Ninge mchapa Lukuvi kwa kunivunjia nyumba bila kulipa fidia pale kibamba

Ningemchapa Dr .Sheni kwa kutoifanya Zanzibar kuwa Dubai kama alivyo ahidi.
 
Back
Top Bottom