Mwananchi waomba radhi, wasema mchakato zabuni uuzaji mradi wa Dege waendelea

Mwananchi waomba radhi, wasema mchakato zabuni uuzaji mradi wa Dege waendelea

MwaikamboN

Member
Joined
Sep 21, 2020
Posts
38
Reaction score
23

Muktasari:​

  • Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Masha Mshomba amesema thamani ya mfuko huo imeongezeka na kwamba, fedha za wanachama ziko salama.
Dar es Salaam. Mchakato wa kumsaka mzabuni kwa ajili ya uuzaji wa mradi wa Dege Eco Village uliopo Kigamboni, Dar es Salaam uliogharimu Sh330 bilioni, bado unaendelea.

Mradi huo ulianzishwa na NSSF mwaka 2014 unahusisha majengo ya hoteli, kumbi za mikutano, eneo la wazi la mapumziko, shule, hospitali na nyumba za kifahari.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Masha Mshomba amesema mradi huo uliamuliwa uuzwe baada ya kufanyika tathmini mwaka 2020 na kwamba uamuzi huo unalenga kurudisha gharama zilizotumika.

"Hivi sasa tulitangaza zabuni ambayo bado ipo katika mchakato na endapo ikatokea kwamba hatujapata mtu, ambaye amefika bei ya kurudisha ile gharama maana yake ni kuwa tutatangaza tena kwa mara nyingine," amesema Masha.

Amesema kwa namna ambavyo wawekezaji wanaongezeka nchini, kuna uhakika kwamba wataweza kununua mradi huo katika kiwango kitakachokuwa na manufaa kwa NSSF.

Ameongeza kuwa kuuzwa kwa mradi huo kutakuwa na faida kubwa kwa wanachama wa mfuko na Taifa kwa kuwa kutaepusha hasara ambazo zingeweza kupatikana iwapo wangeendelea na mradi huo.

Mshomba ametumia nafasi hiyo pia kuwahakikishia wanachama kuwa mfuko huo upo salama na kwamba, thamani yake imeongezeka hadi kufikia Sh6.6 trilioni Desemba, mwaka jana. Hilo ni ongezeko la asilimia 36 kwani hadi kufikia Machi 2021 thamani ya mfuko ilikuwa Sh4.7 trilioni.

“Ongezeko hili linatokana na michango ya wanachama na mapato yatokanayo na uwekezaji, hivyo ukuaji huu wa mfuko unathibitisha kuwa NSSF ipo imara na endelevu kwa ajili ya utoaji huduma kwa wanachama wake,” ameongeza Mshomba.

Kauli hiyo ya Mshomba kuhusu michango inatokana na ukweli kwamba, katika mwaka wa fedha unaoishia Juni 2023, mfuko unatarajia kukusanya michango ya Sh1.6 trilioni ikiwa ni ongezeko la asilimia 14 ukilinganisha na Sh1.4 trilioni zilizokusanywa kwa mwaka 2021/22.

Kuhusu mapato yatokanayo na uwekezaji nayo yanatarajiwa kupanda kutoka Sh500 bilioni hadi Sh700 bilioni kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita.



SAHIHISHO/UFAFANUZI:Jana katika ukurasa wetu wa Instagram tuliandika kichwa cha habari kuwa: NSSF yakosa tena mteja mradi wa Dege. Sahihi ni kuwa mchakato bado unaendelea ili kumpata mzabuni atakayefikia kiwango cha fedha kilichopangwa na mfuko huo kuuza mradi husika.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Mhariri


Pia soma

- NSSF yakosa tena Mnunuzi wa Mradi wa Dege Kigamboni Mji Mpya
 
Hii ni laana ya kudhurumu pesa za michango ya wafanyakazi na kuanzisha miradi ya kifisadi, kuwatesa wastaafu na kuwasumbuwa wafanyakazi wanaopoteza ajila wanapotaka kulipwa pesa zao

Suluhisho Serikali iamke usingizini Sasa itaifishe huu mradi Kwa maslahi ya umma.

Ni wizi mtupu uliofanyika hapo, pesa nyingi amechukuwa Ramadhani Dau na wahuni wenzake.
 
Hili SAKATA la NSSF ,Upinzani,(isomeke CHADEMA) wakilitumia vizuri 2025,watapata kura nyingi,kikubwa walifanyie utafiti na waje na lugha rahisi ambayo itaeleweka kwa wapiga kura wa vijijini..

Hakika Ufisadi huu,ni mfano hai wa ubadhirifu na kulindana wa CCM na Serikali yake. Licha ya taarifa za CAG kueleza kinagaubaga huu ufisadi,hakuna hatua nzito zilizochukuliwa kwa wahusika,sana sana eti,ni kufukuzwa tu kazi kwa Mameneja

Inawezekana vipi mseme eti Azimio moja ya mtaji wake ni acres 28,000,kumbe ni chini ya acres 4000,hao wapimaji walikuwa "wamelewa"?
Mambo ya AIBU kabisa..
 
Back
Top Bottom