Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Mambo ambayo huja baadae kusababisha kuiona ndoa ni chungu ni kuwa na matarajio makubwa kwa mwenza wako,,hii sio sawa hata kidogo,hatuna budi kutafuta namna ya kutafuta raha katika nafsi zetu wenyewe.
Kuna wakati hutaambiwa unapendwa kama zamani lkn hii isikufanye ukose furaha na amani katika ndoa yako,bali amini unapendwa hata kama hutaambiwa,,ukiikubali hali hiyo utapata amani ndani ya ndoa yako
Kuna nyakati huenda kutatokea kutoelewana kutokana na hili au lile,basi tambua maisha ya ndoa ndiyo yalivyo hakuna good time kila siku katika ndoa ila kuna nyakati mbaya pia,ukilijua hilo utakuwa na amani na hautapaniki kwakuwa ni sehemu ya maisha ya ndoa
Kuna wakati tendo la ndoa linaweza kukosekana kutokana na sababu moja au nyingine,basi usipaniki saana na kuona hupendwi au ukawaza labda mwenzako ana sehemu anapumzika huko,tambua tendo hilo lahitaji utulivu wa akili na hisia pia,fahamu kwamba sio siku zote utulivu wa akili na hisia unakuwa sawa bali kuna siku mambo hubadilika.
Kikubwa ni kutambua kuwa furaha haipatikani kwa kupata mambo mazuri peke yake bali hupatikana kwa kukubali kukubaliana na mazingira yoyote ambayo utakutana nayo katika maisha yetu
Kuna nyakati huenda kipato kikawa ni tatizo na mkashindwa kufanya yale mambo ambayo mmezoea kuyapata basi ili uwe na amani huna budi kukubali ukweli kwamba hali imebadilika na tuishi kutokana na hali halisi.
Kuna nyakati huenda ukakosa mda wa kuwa na mwenza wako labda kutokana na majukumu ya hapa na pale basi huna budi kuikubali hiyo hali na fahamu kwamba itapita tu
Ninachotaka kusema hapa matarajio makubwa ndio chanzo kikubwa cha ndoa nyingi kukumbwa na misukosuko,,wakati mwingine tuna ahadiana mambo mengi lakini ukija katika uhalisia mambo hayapo hivyo kabisa,,sio kwamba tuliahidi ili kufurahishana laa,ila tuliahidi tukiwa na matumaini kwamba mambo yataenda sawa kama tulivyopanga lakini kunatokea mazinngira mengine ambayo yanabadilisha kila kitu.
Hivyo kukubaliana na yasiyo tarajiwa ni njia moja kubwa sana ya kuponya ndoa zetu,,na hapa ndipo furaha ya kweli hupatikana kwasababu haibebwi na sababu yoyote ile bali inabebwa na kuyakubali mambo kama ambavyo yanakuja au kutufikia katika nyakati fulani katika maisha yetu.
Kingine jitahidi sana kuwa na mawazo mazuri juu ya mwenza wako, usiwe na mawazo hasi juu yake maadam amekuonyesha heshima ndani ya ndoa yenu,,kitendo cha kutaka kujua anawasiliana na nani au kutaka kupekua simu yake basi ujue hauna hisia nzuri na mwenza wako na hali hiyo itakutesa sana na ni chanzo cha kukosa amani.
Ukifahamu kwamba mwenza wako anaweza kufanya uchafu bila hata kuacha alama katika simu yake itakusaidia kujua kwamba kumbe hata nikiifuatilia simu yake hakuna kitacho saidia itakupa amani ya kutofatilia simu yake.
Kikubwa ni kuheshimiana ndani ya ndoa,,kila mmoja ajitahidi asimfanye mwenza wake akawa na mashaka nae,,haya mambo ya kusema huyu fulani ananisumbua sana kwa kunitumia msg zake au kwa simu zake,swali linakuja kwanini husimblock?
Kama hujamblock ina maana unafurahia usumbufu wake na mawasiliano yake ila mbele yangu unaniletea drama zisizo na sababu
Kingine wanawake mtambue kwamba mnapendwa kwasababu mko katika ndoa lkn mkiachika hao ambao wanajifanya wanajua kupenda kuliko waume zenu ujue watawakimbia chap,,unavutia kwao kwasababu hawana Majukumu ya kukuhudumia sana sana watalipia lodge na nauli na vihela vidogo vidogo lkn utakapokuwa umeachwa hawataweza kukugharamia kwa mahitaji yako yote,kwahiyo mfikirie mara mbili kabla hamjaingia katik huo mtego.
Kikubwa kumbuka furaha ya kweli haipatikani kwa kupata mambo mazuri tu kila siku bali ni pamoja na kukubaliana na mapungufu ambayo yatajitokeza pia.
Gracias / asante
Ni hayo tu!