Mwanangu akilia anakauka mpaka anazimia, jamani hii ni hali ya kawaida?

Muwekee ugoro atatulia mbona.

Muhimu: muache alie tu akiwa mkubwa atakuwa mpole kupitiliza hadi mwenyewe utakuwa unamshangaa.
 
Mkuu namfahamu mtoto mwenye hilo tatizo. Hospitali aliambiwa ni kawaida. Mtoto anavyolia anakuwa anabana pumzi yake na kwa watoto wengine hupelekea kupoteza fahamu . Ila aliambiwa kama mtoto ana dalili nyingine kama kifafa ndio hatari ila kama ni hivo hivo ayakuwa sawa.

Nyongeza.
Watoto wanatofautiana na dalili zinaweza kuwa zinatofautiana hata kama zinaonekana zinafanana. Kaonane na mtaalamu.
 
Acha msihara mkuu,toa maoni!
Ndo ukweli huo wala si utani. mimi nilikuwa silali.Hospital waliniambia baada ya muda ataacha tu ngoma ikaenda hadi miezi8 ndipo mama akaja kushuhudia mtanange na kbadilishwa jina saivi akilia ni ile kulia kawaida tu kama wengine
 
Wana jukwaa, naomba ushauri.

Mwanangu wa mwaka 1 na nusu kila akilia anakauka mpaka anazimia, na hali hii imekuwa ikijirudia kila anapolia kabla ya kurudi katika hali ya kawaida. Kwa kifupi, inanitisha sana kwani sijui shida ni nini.

Je, hii ni hali ya kawaida kwa watoto au inahitaji matibabu ya haraka?
Aiseee kama anazimia ile ya kiukweli kweli kabisaa na sio kujifanyisha basi pelekeni huyo Mtoto Hospitali. Inawezekana Mfumo wake wa kuhandle kilio kwenye Ubongo haupo sawa jamani
 
Mkuu namfahamu mtoto mwenye hilo tatizo. Hospitali aliambiwa ni kawaida. Mtoto anavyolia anakuwa anabana pumzi yake na kwa watoto wengine hupelekea kupoteza fahamu . Ila aliambiwa kama mtoto ana dalili nyingine kama kifafa ndio hatari ila kama ni hivo hivo ayakuwa sawa.

Nyongeza.
Watoto wanatofautiana na dalili zinaweza kuwa zinatofautiana hata kama zinaonekana zinafanana. Kaonane na mtaalamu.
Asante kwa ushauri wako
 
Aiseee kama anazimia ile ya kiukweli kweli kabisaa na sio kujifanyisha basi pelekeni huyo Mtoto Hospitali. Inawezekana Mfumo wake wa kuhandle kilio kwenye Ubongo haupo sawa jamani
Shukrani, nachukua hatua za haraka za kitabibu
 
Baba kimbiza mtoto hospital ndugu yangu, labda kama unapiga story. Hiv mambo ya afya mbona mi nayaogopa sana halaf nyoe naona kama mnayapimia kawaida?? Mimi hapo ningekua mpaka MRI ashafanya aisee
 
Wana jukwaa, naomba ushauri.

Mwanangu wa mwaka 1 na nusu kila akilia anakauka mpaka anazimia, na hali hii imekuwa ikijirudia kila anapolia kabla ya kurudi katika hali ya kawaida. Kwa kifupi, inanitisha sana kwani sijui shida ni nini.

Je, hii ni hali ya kawaida kwa watoto au inahitaji matibabu ya haraka?
mpeleke kwenye makanisa ya upako
 
Wana jukwaa, naomba ushauri.

Mwanangu wa mwaka 1 na nusu kila akilia anakauka mpaka anazimia, na hali hii imekuwa ikijirudia kila anapolia kabla ya kurudi katika hali ya kawaida. Kwa kifupi, inanitisha sana kwani sijui shida ni nini.

Je, hii ni hali ya kawaida kwa watoto au inahitaji matibabu ya haraka?

Kwa nini analia mda wote huo? Tuanzie hapo?!?
 
Back
Top Bottom