DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Naitwa Janeth Shayo, mkazi wa Uru, Moshi. Naomba unisaidie kupaza sauti mwanangu Jonathan Makanyaga (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mrupanga, ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inataka kupindishwa.

Tar.28/02/2024 mwanangu alienda shuleni akiwa mzima. Alipofika aliadhibiwa kwa kuchelewa "namba". Alipoingia darasani alianza kutokwa damu puani na mdomoni. Akarudishwa nyumbani. Nilipomkagua nikamkuta na majeraha yaliyovilia damu mgongoni, kwenye mbavu na mguuni.

Kesho yake nikaenda nae shuleni kutaka kuoneshwa mwalimu aliyemfanyia ukatili mwanangu. Lakini Mwalimu mkuu akaomba nibaki nje. Akaingia na mwanangu ofisi ya walimu na kumtaka amtambue Mwalimu aliyemuadhibu. Mwanangu akamtanbua. Mwalimu Mkuu akaniambia wameshamfahamu ni mwalimu wa "Field" hivyo atazungumza nae.

Wakanipa 20,000/= za matibabu. Nikampeleka mwanangu zahanati. Kesho yake akazidi kutoka damu, na kulalamikia maumivu sehemu za mbavu. Nikampeleka hospitali ya masista. Daktari akaniambia bandama imejeruhika ndio sababu ya kutoka damu mdomoni. Mtoto alidai pamoja na viboko alivyochapwa, Mwalimu pia alimpiga ngumi tumboni. Huenda ndiyo iliyopasua bandama.

Hali yake ilizidi kuwa mbaya tukapewa rufaa kwenda KCMC. Akatakiwa kufanyiwa upasuaji. Gharama 350,000/= lakini sikuwa nayo. Nikapiga simu shuleni wakasema tuombe afanyiwe halafu watalipa baadae. Hata hivyo kabla hajafanyiwa hali yake ikazidi kuzorota, akashindwa kupumua, akawekwa kwenye Oxygen. Akashindwa kula, akawekewa mpira wa chakula. Baada ya siku chache akafariki 😭.

Lakini ripoti ya hospitali inasema mwanangu amekufa kwa kansa ya damu. Kansa gani ya damu inayomuua mtoto kwa wiki mbili? Na kwanini hiyo kansa itokee baada ya kuadhibiwa shuleni? Kwanini Mwalimu aliyemuadhibu mwanangu anafichwa, na sipewi haki ya kumfahamu?

Nalazimishwa nichukue maiti nikazike lakini nimekataa. Nataka uchunguzi huru. Nimeenda dawati la jinsia kulalamika nikapuuzwa. Nimepiga simu kwa Waziri Dkt. Gwajima D akanipa namba ya mtu wa kunisaidia. Nilipopiga kumbe ni yuleyule Mkuu wa dawati la jinsia aliyenipuuza. Nikamrudia Gwajima akasema niwasiliane nae huyohuyo. Nimekosa pa kulilia haki ya mwanangu Jonathan
Aisee pole sana... jamani inasikitisha sana.
 
mnapoelimishwa mpende kuelemika , KCMC wajibu nini wakat walitoa majibu na majibu yao yanafanana na majibu ya hatua ya kwanza , ukisoma bandiko hilo lipo wazi kabisa na hilo bandiko ni kwa mujibu wa huyo mama na sio mwl , kinachowachanganya wengi ni BANDAMA KUHARIBIKA ILA SIDHAN KAMA UNAJUWA HATA BANDAMA INAPATIKANA WAPI MWILINI UHUSIANO WA FIMBO NA BANDAMA , PIA UHUSIANO WA NGUMI NA BANDAMA

WAJINGA KAMA WW MPO WENGI SANA , MNAPINGANA NA TAARIFA ZA VIPIMO MNAENDA AMINI MANENO YA MDOMONI

KWENYE SIMULIZI YOTE INAONESHA KABISA MWL ALIISHIA KUMPA ELF 20 na Sidhani kama mwl alijuwa lolote linaloendelea , je kwann hospitali zote hawajatoa taarifa ya uhusiano wa ngumi na matatizo aliyokuwa nayo mtoto na badala yake wakasema mtoto ana kansa ya damu

HII INFERIORITY INAWASUMBUA SANA , UNAFIKIA HATUA UNAMTISHA MTU AWAACHE MUENDELEE KUWATIA HOFU WALIMU ILI WASHINDWE KUTIMIZA WAJIBU WAO WA KITAIFA , KWA AKILI HIZO MIAKA KADHAA MBELE TUTAKUWA NA KIZAZI GANI KAMA WAELIMISHAJ WATAAMUA KUIFANYA KAMA SEHEM YA KIPATO NA SIO UJENZI WA TAIFA LE KESHO

MUDA MWINGINE MJUE NA ATHARI ZA MAMBO MNAYOYASHABIKIA

HII MIKASA INAPENDWA NA WANASIASA NA MTAONA HUYO KIJANA ATHARIBIWA MAISHA YAKE NA ATAKUWA KAFARA YA MWAASIASA X KUPATA UMAARUFU WKT ILIKUWA JAMBO LA KUWASISITIZIA MUPIME WATOTO ZENU AFYA KABLA YA KUWAPELEKA MASHULENI

Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Takataka 🚮
 
Hapo tu kwenye alipiga simu kwangu ndiyo ninaposema kuwa siyo kweli. Mm nawasiliana na watu wote kwa SMS. Akipiga nasema tafadhali tuma ujumbe. Kumbukumbu za kwenye ukurasa wa mawasiliano yangu mm na yy hazioneshi kuwa kulikuwa na mazungumzo aina hiyo kati yake na mm. Naomba kuweka kumbukumbu sahihi.

Aidha, nimeongea naye na kumuuliza je niliongea na ww? Amekanusha yy mwenyewe kuwa hajaongea na mm. Badala yake, amethibitisha kufahamu kuwa, watuhumiwa 5 wako ndani.

Sijajua lengo la hii taarifa kuwa niliongea naye lilikuwa nn hasa.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa taarifa pia najaribu kupandisha hapa sn 3.

WITO wangu; wanahabari wa kijamii tushirikiane ila tuepuke kutoa taarifa za upande mmoja. Vita ni yetu wote, ushirikiano wa dhati ni muhimu.

Ahsanteni sana.
IMG_20240315_140850_094.jpg
IMG_20240315_140850_164.jpg

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
IMG_20240315_140725_830.jpg

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Duuu mkuu pole sana bila shaka Dkt. Gwajima D atakuja hapa kutoa majibu …aisee inauma sana sana yani mwalimu anampiga ngumi mtoto hapa hii haikubalika kabisa kabisa!

Nafikiri kwenye hili Mwl Mkuu anapaswa kuchukuliwa hatua kabisa na huyo mwalimu anapaswa kufikishwa kwenye vyombo vya kisheria hii ni hatari!

Halafu Dkt. Gwajima D unapaswa kutwambia huyo mtumishi wako wa dawati la jinsia anaye lalamikiwa kupuuza watu unapaswa kumuondoa pale hapamfai kabisa!

IMG-20240315-WA0159.jpg

Changamoto ni yy mwenyewe mama huyu nimemuomba hiyo namba ya simu ya mtu ambaye waliongea naye Ili nimhoji, naisubiri tangu asubuhi.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Mama yangu Mhe Dkt Mwijuma
Ninapenda kukushauri uliangalie hili jambo kwa jicho pevu.

Kilio cha mama kimetugusa wengi. Inaamsha hisia
Tayari nimetoa ufafanuzi kuhusu taarifa ya yy kuongea na mm kuwa siyo sahihi. Unaweza kusoma tafadhali. Ahsante Sana. Na nimeabatisha na taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu hatua iliko hiyo kesi

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Lakini si anasema alimwambia hadi waziri na akapewa namba ya dawati lakini kakosa msaada!
Halafu hakurudi kwangu, kwamba alipiga akaniambia nikasema Rudi tena huko, siyo kweli. Unaweza kusoma maelezo yangu tafadhali na baada ya mm kushangazwa na taarifa hizi nikamtafuta. Uzuri mm nawasiliana na wote kwa sms Ili kutunza Kumbukumbu zisaidie baadae.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Unaweza tu kinibeza upendavyo, ndiyo uongozi wenyewe huo. Ila hiyo taarifa siyo sahihi. Maana mm nawasiliana na wanitafutao kwa sms Ili kutunza kumbukumbu. Kwangu hakupiga tena, na nimeongea naye hata hizo namba zilizompigia au alizopiga akaongea akajibiwa hivyo nimeomba anitumie, nasubiri tangu asubuhi. Uzuri mitambo ya simu hutunza rekodi siku ngapi tena?

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kama imefikia hatua Waziri anarusha mpira kwa mtu aliye chini yake kwa tukio la kikatili na kupelekea mauaji kwa namna hii basi nchi haina uongozi.

Inaumiza sana kuuliwa mwanao alafu walioshika mpini wanalindana, haki mzazi achana na hiyo maiti hadi haki ipatikane vinginevyo ukiibeba umeruhusu jinai kuwa haki.
Uzuri ni kuwa, hakukuwa na mazungumzo kati yangu na yy kama ilivyoandikwa hapo juu. Sijui haya katunga nani

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Unaweza tu kinibeza upendavyo, ndiyo uongozi wenyewe huo. Ila hiyo taarifa siyo sahihi. Maana mm nawasiliana na wanitafutao kwa sms Ili kutunza kumbukumbu. Kwangu hakupiga tena, na nimeongea naye hata hizo namba zilizompigia au alizopiga akaongea akajibiwa hivyo nimeomba anitumie, nasubiri tangu asubuhi. Uzuri mitambo ya simu hutunza rekodi siku ngapi tena?

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Kwa hili mh...nakutetea ujue hata Mimi binafsi huwa nikipata muda nakutumiaga msg na huwa unajibu.

Kwenye ufuatiliaji wa masuala upo vizuri Nina Imani KunA step Moja huyu mama aliiruka...!

Mh Dkt. Gwajima D mwenyezi Mungu akupe nguvu busara na hekima. You deserve a Gold medals​
 
Hapo tu kwenye alipiga simu kwangu ndiyo ninaposema kuwa siyo kweli. Mm nawasiliana na watu wote kwa SMS. Akipiga nasema tafadhali tuma ujumbe. Kumbukumbu za kwenye ukurasa wa mawasiliano yangu mm na yy hazioneshi kuwa kulikuwa na mazungumzo aina hiyo kati yake na mm. Naomba kuweka kumbukumbu sahihi.

Aidha, nimeongea naye na kumuuliza je niliongea na ww? Amekanusha yy mwenyewe kuwa hajaongea na mm. Badala yake, amethibitisha kufahamu kuwa, watuhumiwa 5 wako ndani.

Sijajua lengo la hii taarifa kuwa niliongea naye lilikuwa nn hasa.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetoa taarifa pia najaribu kupandisha hapa sn 3.

WITO wangu; wanahabari wa kijamii tushirikiane ila tuepuke kutoa taarifa za upande mmoja. Vita ni yetu wote, ushirikiano wa dhati ni muhimu.

Ahsanteni sana. View attachment 2935509View attachment 2935510

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Vizuri sana Mh Waziri, endelea na kazi yako nzuri. Mungu akuongoze.
 
Kimsingi siwezi kutoa lawama sana kwa waziri kwa sababu kimsingi awezi fanya kila kazi mwenyewe anapaswa kusaidiwa lakini anachotakiwa kuhakikisha wanao msaidia wawe active na wawe ni wenye uelewa na utu sio wajinga wajinga,jeuri ,kibri na dharau …dawati linapaswa liwe na watu wenye utu!

Kimsingi hao watu watamuharibia sana Dkt. Gwajima D sifa zake na juhudi zake maana kila mwana jf anajua anavyo jitahidi kujibu na kutolea ufafanuzi na kushughuliakia matatizo ya watu na ni kati ya mawaziri walio active sana hapa na hawaogopi mijadala…
Bila shaka atakuja kulijibu hili swala maana watu kama hawa wanao puuza watu hawapaswi kumzunguka wana muharibia sana sana!
Na ukweli ni kuwa, hii Hadith imetungwa, hakunipigia na wala mm utaratibu wangu huwa siyo wa kuongea Bali SMS (kuandika ujumbe), tangu nitangaze simu. Kwenye mawasiliano yake na mm hakuna kitu kama hicho na yy anajua. Na kilichopo ni kuwa, watuhumiwa 5 wako ndani na Jeshi limethibitisha.

Kwa mema machache niliyofanya, yatakumbukwa baadae, nature ni nzuri, inatabia ya kukumbuka. Tuendelee kushirikiana [emoji1666]
IMG_20240315_140850_094.jpg
IMG_20240315_140850_164.jpg

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Mheshimiwa Dkt. Gwajima D hizi ni shutuma nzito unapaswa uzifanyie kazi wewe mwenyewe bila kumtumia huyo afisa dawati kwani mlalamikaji hana imani naye vinginevyo atakupaka matope na wewe una sifa kubwa ya kuwa mtetezi wa wanyonge.
Hapa ni shutuma za kutengenezwa kwa makusudi. Kwanza, sijawahi ongea naye, mawasiliano yangu ni sms , kwenye ukurasa wake hakuna maneno aina hiyo, naye anajua kuwa, watuhumiwa 5 wako ndani. Na baada ya kumpigia kuongea naye imekuwaje, naye anashangaa, nimeomba simu aliyopiga au kupigiwa anipe, tangu asubuhi hajanipa. Humu duniani, tuvumiliane tu...
IMG_20240315_140850_094.jpg
IMG_20240315_140850_164.jpg

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom