DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mh Waziri nimekuelewa sana pengine kuna sehemu amekosea naomba usamehe na ujue kuwa ambacho unaweza msaidia ni yeye kupata haki yake ya kujua ukweli na kupata fursa ya kuongea nae na kumfariji maana kwa hali aliyonayo lazima kuna kuchanganyikiwa…Mtoto amefariki cha kumsaidia ni kuhakikisha anapata msaada na unaongea nae….! Tunaomba unsaidie wewe ni Mama na unajua mtoto anavyo uma wengi huvurugwq!
 
Kifupi sijaongea naye naye anashangaa. Nisaidie kumuuliza ameongea na nani maana mm nasubiri hiyo namba tangu asubuhi. Ukweli uko kwenye tamko la Polisi kuwa watuhumiwa wako ndani.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Tunashukuru kwa kuja kujibu hapa chamsingi tunaomba ufatilie hili jambo hadi mwisho ujue limefikia wapi na ikiwezekana uonane na mfiwa ujue na umfariji! Kwenye hizi kazi kuna kusingiziwa kwa hiyo usichoke ndio kazi ya Umma! Tunaomba umsaidie
 
Nilitaka kushangaa hizi tuhuma juu yako maana nakujua vizuri.Binafsi mwaka jana nilikuwa na shida nikakutumia sms usiku saa nne usiku nilishangaa kuona unanijibu.Upo vizuri sana kufatilia mambo yanayohusu wizara yako maana ni nadra sana kumuona Waziri anajibizana na wananchi tena kwa sms .Big up sana dada.
 
Toa ripoti hii kwenye vyombo vya juu; ni ukatili sanba kukatisha maisha ya mtoto wa miaka saba ambaye bado alikuwa na dunia yite mbele yake. \
 
Shikamoo Dr. gwajima nimefarijika kumbe umekuwa mtu wa watu kiasi hiki hadi unachati na sisi huku..Naomba tu kubali salamu yangu najua inaenda kubadili ktu kwenye maisha yangu kitakacho acha alama🙏🙏
 
Nafikiri kashatoa majibu kwenye post za nyuma na ametoa maelezo mengi tuu unapaswa kusoma na amesema ana fatilia na ana subiri majibu ya mtoa taarifa na atamtafuta!
 
Inasikitisha sana huyo mwalimu achukuliwe sheria.
 

Ficha ujinga wako basi.
 
Umeongea vizuri, ila kusema hutaki mwanao asipigwe nimebaki mdomo wazi. Basi wewe ni tofauti na mimi, mimi nina watoto wanasoma hizi kayumba zilizochangamka (English medium) tena ya dini . Wakati nampeleka wa kwanza wakaniambia kuna wazaz walisema hawataki watoto wao wachapwe. Mimi nilisema wa kwangu akikosea achapwe la sivyo ntamhamisha. Mimi sina imani ya kulea mtoto km mayayi. Muhimu "aadhibiwe siyo kupigwa". Mimi mwenyewe hata nyumbani wanakula makofi kila wakifanya upuuzi achilia mbali fimbo.

Ila ktk malezi kila mtu na style yake bwana hamuwezi kufanana wote. Ni sawa tu na kuendesha maisha ya ndo, kila mwanaume ana mfumo wake.
 
Tukisoma taarifa ya Jeshi la Polisi kipenge cha 3, tutaona kwa uwazi hatua zote. Kuwa uchunguzi umefanyika hospitali gani na watuhumiwa 5 wako ndani na upelelezi unaendelea. Na kwamba, tukio lilitokea 28 Feb 2024 taarifa ikatolewa 11 Machi, 2024. Hapa Pana maswali ngazi ya wazazi napo. Hivyo lazima upelelezi ufanyike chini ya wizara ya mambo ya ndani Jeshi la Polisi, kisha mwendesha mashtaka (wizara ya Katiba na Sheria) aone itifaki yake kuhusu kwenda mahakamani.

Nadhani wananchi wengi hawajui hizi itifaki za kisheria, wao wanajua, ustawi akipokea taarifa mambo yote anamaliza yy. Siyo hivyo ndugu zangu wapendwa.

Kuna Sheria, taratibu na kanuni za vyombo vya taasisi za wizara mbalimbali kwa mujibu wa Sheria kuu yaani Katiba ya nchi yetu. Mbarikiwe.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Mimi sina neno na huyu mama wala. Na sitakiwi kuwa na neno lolote kama kiongozi. Hoja yangu ni hawa watoa habari wa kujitegemea akina unknown ambao, hawazingatii maadili na miiko ya habari, ama kwa kutojua au kujua yaani makusudi na kutumika kwa faida zao. Ili tu, kazi yote ninayofanya na wadau wazuri kwenye jamii kwa maslahi ya jamii ionekane ya hovyo.

Anyway, Mungu ana macho.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Ukienda nchi zilizostaarabika kama za Ulaya utapata shida kweli kweli na watakunyang'anya watoto. Kupiga hakusaidii bali kunaharibu. Hii ni research siyo mimi. Unaweza kumfundisha mtoto bila kumchapa. Hata mimi nyumbani sikupigwa na wazazi wangu. Hivi unajua mtoto aliyekulia Ulaya ana tofauti kubwa na mtoto aliyekulia Tanzania? Unajiuliza ni kwa sababu gani?
 
Tunashukuru kwa kuja kujibu hapa chamsingi tunaomba ufatilie hili jambo hadi mwisho ujue limefikia wapi na ikiwezekana uonane na mfiwa ujue na umfariji! Kwenye hizi kazi kuna kusingiziwa kwa hiyo usichoke ndio kazi ya Umma! Tunaomba umsaidie
Kila kitu Kiko sawa, shauri linaendelea, soma taarifa ya Polisi, Moshi kuna serikali ya mkoa na wilaya pia, hapa kikubwa wala siyo huyu mama Bali watoa taarifa wasiozingatia weledi wa kubalance habari. Hawa ndiyo shida.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Hata mm nimeshangaa kuwa, inawezekanaje baadhi ya watu wakipokea taarifa tu wanaondoka nayo hata kusema kuwa, mbona haina upande wa pili? Yaani nashangaa kuwa zama hizi mtu anaweza kuibuka na habari mfano nime R...P, basi baadhi wakaanza kabisa kuchimba na ka...ri hata dea.... cert..... haipo[emoji3060]

Wito wangu jamani, watoa taarifa watafute taarifa kwa bidii lakini wafanye balance, na wasomaji nao wasome kwa bidii ila wakumbuke kuangalia balance...

Kwenye mambo ya kijamii wote tunategemeana .. [emoji7]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Shikamoo Dr. gwajima nimefarijika kumbe umekuwa mtu wa watu kiasi hiki hadi unachati na sisi huku..Naomba tu kubali salamu yangu najua inaenda kubadili ktu kwenye maisha yangu kitakacho acha alama[emoji120][emoji120]
Ubarikiwe, Kila la heri. Ndiyo Dunia ilivyo, Hadi vitabu vimeandika, kumbukumbu nzuri hutolewa ukisha fumba macho na mdomo. Ndiyo kanuni ya Dunia. Kwa kuwa tunaishi kimwili na kiroho, tuimarishe zaidi misuli ya Imani, ndiyo faraja yetu....[emoji7]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Uzi ufungwe Sasa kweli katika mawaziri nchi hii wewe Mama upo active kwenye sector yako

Ubarikiwe sana Mheshimiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…