mjingamimi
JF-Expert Member
- Aug 3, 2015
- 42,209
- 51,004
Naamini watu wa serikali wameona.hawatamsubiri tena makonda aende ndo wachukue hatua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeandika ujinga mtupu..!!!Pumba tupuBila kuchangia kwa mihemko na bila kujaji kwa nini unapuuzwa ebu tuanzie hapa;
1) Ilikuwaje hizo hospitali zikubali kumtibu mtoto bila PF3 ya police wakati uliwaeleza na kuwaonesha makovu ya vipigo kutoka kwa mwalimu.
2) Kwa nini hujaenda police kutoa taarifa au kwa afisa elimu wake hata wa kata.
3) Mtoto wa darasa la kwanza ni mdogo sn iweje mwalimu afikie hatua ya kumpiga hovyo hovyo hivyo tena kwa sababu ya kuchelewa. Angekuwa mkubwa km sekondari tungesema kulikuwa na majibizano mwalimu akashikwa hasira akampiga hovyo. (NB: Vyovyote mwanafunzi atakavyojibu na kumuudhi Mwalimu, Mwalimu haruhusiwi kumuadhibu hovyo).
4) Unasema mkuu alikataa kukuonesha Mwalimu mhusika. Ulitaka kumuona ili iweje. Km ungemuona ndo angepona. Hapa ndo wazazi wengi wasio na upeo hukurupuka na kutanguliza hasira mbele maarifa kubaki nyuma. Muhimu ulitakiwa ufuate taratib za kisheria ili afahamike na kukamatwa. Na nikuhakikishie hata km angekamatwa iwapo usingekuwepo wakati wa ukamataji usingemuona hata ungelia machozi ya damu police hawawezi kukupa ruhusa ya kuonana na mbaya wako kwa wakati huo labda mkifika mahakamani. Hivyo hivyo Mwalimu mkuu siyo mjinga eti akuoneshe Mwalimu mhusika. Angejuaj lengo llako, je km ulitaka kumdhuru. Kamwe hilo haliwezi kutokea kwenye taasisi kienyeji hivyo.
5) Kwanini hutaki kuamini majibu ya daktari. Je kwanini tusiamini kuwa mtoto alikuwa mgonjwa kweli na wewe tatizo hilo ulikuwa unalifahamu Ila fimbo za Mwalimu zimekuwa sababu tu.
6) Je ni mwanao tu alipigwa hivyo? Km wengine nao waliadhibiwa lakini kwa utaratibu na kuathirika kwa nini awe mwanao tu. Km waliadhibiwa kwa pamoja umeshindwa kuuliza wenzake kilichoprlekea mwanao kupigwa kiasi cha kupasuka bandama.?
7) Unasema ulazamishwa kuzika mwanao. Nani anaekushinikiza kufanya hivyo wakati kwenye bandiko lako hakuna ulikotaja police kuhusika.
Mwisho: Nakupa Pole kwa yaliyokukuta na fuata taratib za kisheria kupata haki yako kuliko kuja humu kulia. Pili, ulitakiwa utaje shule aliyokuwa anasoma.
Kuna jambo nitaeleza hapa kwa ufupi ambalo liliwahi kumtokea Mwalimu flani baada ya kumuadhibu mwanafunzi wa sekondari viboko 2 mkononi tena mbele ya kaka yake waliekuwa darasa moja lakini baada ya muda mfupi alifariki. Lakini alipopewa mzazi taarifa huku mwalimu akitafuta kukimbia, baba wa marehem alisema huyo mwalimu hana hatia aachwe. It means kulikuwa na jambo la kifamilia nyuma ya pazia. Naskia takribani miaka 6 sasa huyo mwalimu yupo hapohapo na maisha yanaendelea.
Nimemaliza; BANDOKITITA
Ebu jifunze kitu hapa.
Walimu 5 wameshikikiwa na polisi wanahojiwa. Hili ndo lilikuwa linalohitajika, mtuhumiwa ahojiwe na limefanyika na hilo ndo la muhimu.Unadhan mpaka waziri na mtu wa Dawati la jinsia kuanza kumpuuza mzazi hawakulifanyia Kazi Hilo? Lazima Mwl amehojiwa na Daktari amehojiwa. Lazima mkurugenzi amelifatilia analijua Hilo, lazima mkuu wa wilaya amelifatilia analijua Hilo, DSEO Lazma amelifatilia analijua Hilo, ocd lazma analijua hilo Maana waziri hawezi kwenda mwenyewe Ana vyanzo vyake vya habari na viongozi wa chini hujitahid sana kufatilia jambo na kulifahamu Kwa kina, asije kupigiwa Simu akampotosha waziri Au akajibu hajui Maana ni kuchezea kitumbua chake.
Habari Mdusi!yaaan humu kuna wajinga wengi , ukisoma story ya huyo mtoto mpk mauti ni kama huyo mama anataka tumia mauti ya mwanae iwe mtaji wake kiuchumi , anampa presha mwl mkuu amuweke wazi mwl wa field ( hii ni kosa pia ) ili mwl wa field aje ampooze huyo mama , ila ukwel anaujuwa kuwa mwanae alikufa kwa KANSA YA DAMU na dalili alikuwa nazo .
Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Sio wote wana uwezo wa kumpiga mtoto Ngumi ila wapo wanaweza kufanya hivyo...kupiga ngumi na kuchapa vinafanana ? hoja ya mama bandama imeharibika kisa kapigwa ngumi na michirizi mgongoni , je WEWE UNAWEZA mpiga ngumi mtoto wa drs la kwanza NGUMI ? Ebu onesha utimamu wako
Sent from my HUAWEI NXT-L29 using JamiiForums mobile app
Dkt. Gwajima D aliyetoa taarifa sio 'mtoa habari wa kujitegemea au mwaandishi wa habari wa kujitegemea' ama 'unknown' kama ulivyomuita.... hapa JF kuna kitu kinaitwa 'Fichua Uovu' tool inayokuwezesha kuripoti jambo bila utambulisho wako kujulikana, hata wewe ikiwa una jambo ambalo umekosa msaada na unahofia kujulikana ukiweka hapo taarifa ID yako itasoma 'Anonymous', ujumbe utafika bila utambulisho wako kuwa compromised.Mimi sina neno na huyu mama wala. Na sitakiwi kuwa na neno lolote kama kiongozi. Hoja yangu ni hawa watoa habari wa kujitegemea akina unknown ambao, hawazingatii maadili na miiko ya habari, ama kwa kutojua au kujua yaani makusudi na kutumika kwa faida zao. Ili tu, kazi yote ninayofanya na wadau wazuri kwenye jamii kwa maslahi ya jamii ionekane ya hovyo.
Anyway, Mungu ana macho.
Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Asante sana kwa matusi yako. Mungu akupe heri.Umeandika ujinga mtupu..!!!Pumba tupu
Heshima kwako chief Kuna watu wanadhalilisha sana taaluma ya udaktari.Habari Mdusi!
Nimeona mara nyingi ukirudia Hili swala Kwamba mtoto alikuwa na kansa na kadha wa kadha..
Naweza kukubaliana na wwe kwamba Kweli mtoto huenda mtoto alikuwa na cancer na huenda mama yake hakuitambua..
Ila kuna swali moja Unashindwa kuliaddress kwa watu wanaouliza..
How Leukemia inaweza kuwa triggered (Aggreviated) After Kipigo kutoka kwa mwalimu?
lakini usisahau pia kuwa Dalili zote Za leukemia alizo nazo huyo mtoto zinafanana na Traumatic injury inayotokana na blunt injury..
Petachiae inaweza kufanana na Bruises only Unautofautisha kwa R/O kuwa Una uhakika hakukuwa na tukio la injury..
Na hata Spleenomegaly (Au rupture) inaweza kusababishwa na Kipigo pia, Na hata Visceral organs zikiwa injured inaweza kupelekea Kupata Bleeding
hili swala nimeliongea kama Mzazi kwa sababu najua michezo yetu Madaktari...
INaweza ikawa kwa nia njema lakini tafsiri ya mpokeaji ikawa tofauti kabisa...
Kuna kipindi kulikuwa na mchezo wa utoaji saja wa mimba lakini ukisoma Report unakuta Ni inevitable abortion, Missed abortion ,na incomplete abortion nyingi..
Unajua ni kwanini? Madaktari walikuaa wanajiprotect kwa ajili ya Kutokutwa na hatia...
Watu wakiuliza na kulalamika haina maana kuwa ni wajinga, ina maana kwamba huenda wanajua mchezo ila hawajui kitaalamu unachezajwe...
UNAFIKIRI KWANINI WAMEKAMATWA WATU WATANO WAKATI MTOTO ALIKUWA NA ONLY SHIDA YA CANCER???
NAFIKIRI TANZANIA SASA KUPITIA KITIVO CHA SHERIA KUNA HAJA YA KUANZISHA KOZI YA TABIBU/DAKTARI MWANASHERIA (Medical lawyer)....Inaweza ikasaidia kutatua Sintofahamu zilizo ndani ya kidaktari maana Daktari itabidi aende kusomea Sheria ili kumuwezesha kutunza Heshima ua udaktari kwenye jami..
Shukrani
Kama ingekuwa kweli yaani mara moja ningewaambia kuwa, kweli nami nilimwambia hivi na chats zake ninazo. Sasa siyo kweli, hatukuongea, kumbe mimi nisemeje ndugu zangu? Maana kwanza nawasiliana na kutoa maelekezo kwa sms lengo nibaki na kumbukumbu sababu ya rejea.Hii kazi ya ualimu Kwa Africa ni laana baada ya kusoma kisa hiki nikakumbuka jinsi nlivyokuwa nazabuliwa na walimu,wengine wakinishindilia Kwa miguu huku nimeshika chini.Kuna mmoja alinipiga Hadi nkasema mwalimu sikubali najirudishia japo nilisema tu maana nakumbuka baada ya kauli Ile nlijikuta asembo kengele imegongwa na wanafunzi wakinishangaa.Kifupi mm ni shuhuda wa kipigo hevi Cha walimu waliolaaniwa na nikwambie tu japo nlikuwa ni mtundu kiasi bt vipigo vingine vilikuwa ni for no good reason at all.Huyo boya aliyempiga mtoto kama Rika lake asakwe ajibie,na tena Nashangaa waziri Gwajima kwanini anarusha mpira kwenye jambo hili kama ni kweli.?
Hakika, na hili ndiyo muhimu zaidiKwa kuwa walimu wamekamatwa, tuache police wafanye Kazi yao
Safi Sana, mimi kwa kuwa nimeona identity yake ni hiyo ndiyo maana nikaandika hivyo hivyo. Hata hivyo, nimepongeza na kutoa wito kuwa, basi taarifa ziwe balanced Ili kuepusha hizi taharuki za kuanza kufafanua Kila ukurasa badala ya mimi kujikita na mambo mengine. Anyway, nadhani mjadala huu pia umekuwa na faida nyingi za elimu.Dkt. Gwajima D aliyetoa taarifa sio 'mtoa habari wa kujitegemea au mwaandishi wa habari wa kujitegemea' ama 'unknown' kama ulivyomuita.... hapa JF kuna kitu kinaitwa 'Fichua Uovu' tool inayokuwezesha kuripoti jambo bila utambulisho wako kujulikana, hata wewe ikiwa una jambo ambalo umekosa msaada na unahofia kujulikana ukiweka hapo taarifa ID yako itasoma 'Anonymous', ujumbe utafika bila utambulisho wako kuwa compromised.
Hii hapa na kwa wanaJF wote ambao hamjui kuna hiki kitu humu[emoji116][emoji116]
View attachment 2935907