DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mheshimiwa Waziri kwanza nikupongeze kwa kujibu haya maswali, ila si jambo sahihi kuanza kutoa lawama kwa huyo mama elewa yupo katika kipindi kigumu sana.
Nimeepuka Sana lawama na badala yake angle niliyotumia ni kuelimisha waliokuwa Wananilaumu mimi kuhusu uhalisia ulivyokuwa. Sasa iwapo tafsiri zimekuwa tofauti, ni mapokeo tu.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Hakika, na hili ndiyo muhimu zaidi

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Muhimu zaidi ni haki kupatikana kwa wakati, maana huchelewi kusikia kuwa washitakiwa wameachiwa huru kutokana na poor investigation, au hati ya mashitaka ilikosewa! Hongera sana Muheshimiwa kwa kua karibu na Jamii, Mungu akutangulie kwa kila jambo!!
 
Safi Sana, mimi kwa kuwa nimeona identity yake ni hiyo ndiyo maana nikaandika hivyo hivyo. Hata hivyo, nimepongeza na kutoa wito kuwa, basi taarifa ziwe balanced Ili kuepusha hizi taharuki za kuanza kufafanua Kila ukurasa badala ya mimi kujikita na mambo mengine. Anyway, nadhani mjadala huu pia umekuwa na faida nyingi za elimu.

Shukrani

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Aya mama kapumzike kwanza
 
Katika page za Malisa GJ kuna habari hii leo.

Naitwa Janeth Shayo, mkazi wa Uru, Moshi. Naomba unisaidie kupaza sauti mwanangu Jonathan Makanyaga (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mrupanga, ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inataka kupindishwa.

Tar.28/02/2024 mwanangu alienda shuleni akiwa mzima. Alipofika aliadhibiwa kwa kuchelewa "namba". Alipoingia darasani alianza kutokwa damu puani na mdomoni. Akarudishwa nyumbani. Nilipomkagua nikamkuta na majeraha yaliyovilia damu mgongoni, kwenye mbavu na mguuni.

Kesho yake nikaenda nae shuleni kutaka kuoneshwa mwalimu aliyemfanyia ukatili mwanangu. Lakini Mwalimu mkuu akaomba nibaki nje. Akaingia na mwanangu ofisi ya walimu na kumtaka amtambue Mwalimu aliyemuadhibu. Mwanangu akamtanbua. Mwalimu Mkuu akaniambia wameshamfahamu ni mwalimu wa "Field" hivyo atazungumza nae.

Wakanipa 20,000/= za matibabu. Nikampeleka mwanangu zahanati. Kesho yake akazidi kutoka damu, na kulalamikia maumivu sehemu za mbavu. Nikampeleka hospitali ya masista. Daktari akaniambia bandama imejeruhika ndio sababu ya kutoka damu mdomoni. Mtoto alidai pamoja na viboko alivyochapwa, Mwalimu pia alimpiga ngumi tumboni. Huenda ndiyo iliyopasua bandama.

Hali yake ilizidi kuwa mbaya tukapewa rufaa kwenda KCMC. Akatakiwa kufanyiwa upasuaji. Gharama 350,000/= lakini sikuwa nayo. Nikapiga simu shuleni wakasema tuombe afanyiwe halafu watalipa baadae. Hata hivyo kabla hajafanyiwa hali yake ikazidi kuzorota, akashindwa kupumua, akawekwa kwenye Oxygen. Akashindwa kula, akawekewa mpira wa chakula. Baada ya siku chache akafariki [emoji24].

Lakini ripoti ya hospitali inasema mwanangu amekufa kwa kansa ya damu. Kansa gani ya damu inayomuua mtoto kwa wiki mbili? Na kwanini hiyo kansa itokee baada ya kuadhibiwa shuleni? Kwanini Mwalimu aliyemuadhibu mwanangu anafichwa, na sipewi haki ya kumfahamu?

Nalazimishwa nichukue maiti nikazike lakini nimekataa. Nataka uchunguzi huru. Nimeenda dawati la jinsia kulalamika nikapuuzwa. Nimepiga simu kwa Waziri @gwajimad akanipa namba ya mtu wa kunisaidia. Nilipopiga kumbe ni yuleyule Mkuu wa dawati la jinsia aliyenipuuza. Nikamrudia Gwajima akasema niwasiliane nae huyohuyo. Nimekosa pa kulilia haki ya mwanangu. Naomba Rais Samia Suluhu Hassan anisaidie.!

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Yaani wakuu kama una mtoto shule za kayumba, usipochukua action unaweza kupoteza mtoto, kuna mwalimu mmoja hapa mwanza, shule x, alimwazibu mwanangu kinyume na taratibu za kanuni za ualimu,bint akarudi nyumbani yuko hoi, aisee niliwasha moto kwa mkuu wa shule mpaka aliitwa muhusika, niliwaambia nikinua hapa mguu, tusilaumiane, tangu siku hiyo, hakuna mwalimu anacheza na mwanangu, hizi shule za kayumba wakijua mzazi ni mkakix hawamgusi mwanao, ye ye DED ansongea muharo maana ajui maumivu watoto wanayopitia mashule ya serekali..
 
Inauma sana aisee huyo , mpaka machozi yanatoka kama mwanangu, huyo mtu ashughulikiwe ipasavyo
 
Tunapaswa kumrudia Mungu kusema kweli hivi vifo vya ajabu ajabu vimeshamiri mno!?
 
Yaani aliona viboko havitoshi akaongeza na ngumi???
Huyu Mwalimu atakuwa na mapepo si bure! [emoji848][emoji848] Sheria ichukuwe mkondo wake mara moja na waache kumzungusha huyu mama!!
 
Si ndiyo taarifa imetolewa kuhusu maendeleo ya shauri ndugu yangu? Mm nilichokanusha ni kuwa sijaongea kwa simu na kutoa hayo maelekezo kama ilivyosemwa. Kisha nikatoa na update ya hatua zilizochukuliwa kumbe tena ndugu yangu sijafanya vema? Niwie radhi basi tusonge mbele.
You're correct na Asante kama unalifanyia kazi ili haki itendeke.

Jambo la msingi Uhai wa binadamu umetoweshwa kwa makusudi hivyo basi wahusika wapewe haki yako.
 
Hawa walimu tarajali huwa hawapewi tahadhari ya kuadhibu wanafunzi. Vitoto vya siku hizi havina uwezo wa kuhimili adhabu hata ndogo huwa tunaviacha na kuvichekea tu, maana hata ukivifinya alama ya kifinyo itaonekana miilini mwao. Ishu ni kufundisha tu, wale wa dararasa la tano, sita na saba pamoja na ndugu zao wa sekondari huwa tunawaziria kipindi wakileta za kuleta watajifundisha wenyewe shida kuadhibu watoto wa watu hatutaki, wengine ni wagonjwa ukimgusa unammalizia
 
Naitwa Janeth Shayo, mkazi wa Uru, Moshi. Naomba unisaidie kupaza sauti mwanangu Jonathan Makanyaga (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mrupanga, ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inataka kupindishwa.

Tar.28/02/2024 mwanangu alienda shuleni akiwa mzima. Alipofika aliadhibiwa kwa kuchelewa "namba". Alipoingia darasani alianza kutokwa damu puani na mdomoni. Akarudishwa nyumbani. Nilipomkagua nikamkuta na majeraha yaliyovilia damu mgongoni, kwenye mbavu na mguuni.

Kesho yake nikaenda nae shuleni kutaka kuoneshwa mwalimu aliyemfanyia ukatili mwanangu. Lakini Mwalimu mkuu akaomba nibaki nje. Akaingia na mwanangu ofisi ya walimu na kumtaka amtambue Mwalimu aliyemuadhibu. Mwanangu akamtanbua. Mwalimu Mkuu akaniambia wameshamfahamu ni mwalimu wa "Field" hivyo atazungumza nae.

Wakanipa 20,000/= za matibabu. Nikampeleka mwanangu zahanati. Kesho yake akazidi kutoka damu, na kulalamikia maumivu sehemu za mbavu. Nikampeleka hospitali ya masista. Daktari akaniambia bandama imejeruhika ndio sababu ya kutoka damu mdomoni. Mtoto alidai pamoja na viboko alivyochapwa, Mwalimu pia alimpiga ngumi tumboni. Huenda ndiyo iliyopasua bandama.

Hali yake ilizidi kuwa mbaya tukapewa rufaa kwenda KCMC. Akatakiwa kufanyiwa upasuaji. Gharama 350,000/= lakini sikuwa nayo. Nikapiga simu shuleni wakasema tuombe afanyiwe halafu watalipa baadae. Hata hivyo kabla hajafanyiwa hali yake ikazidi kuzorota, akashindwa kupumua, akawekwa kwenye Oxygen. Akashindwa kula, akawekewa mpira wa chakula. Baada ya siku chache akafariki 😭.

Lakini ripoti ya hospitali inasema mwanangu amekufa kwa kansa ya damu. Kansa gani ya damu inayomuua mtoto kwa wiki mbili? Na kwanini hiyo kansa itokee baada ya kuadhibiwa shuleni? Kwanini Mwalimu aliyemuadhibu mwanangu anafichwa, na sipewi haki ya kumfahamu?

Nalazimishwa nichukue maiti nikazike lakini nimekataa. Nataka uchunguzi huru. Nimeenda dawati la jinsia kulalamika nikapuuzwa. Nimepiga simu kwa Waziri Dkt. Gwajima D akanipa namba ya mtu wa kunisaidia. Nilipopiga kumbe ni yuleyule Mkuu wa dawati la jinsia aliyenipuuza. Nikamrudia Gwajima akasema niwasiliane nae huyohuyo. Nimekosa pa kulilia haki ya mwanangu Jonathan

Pia, Soma: Madai ya Janeth Shayo, Mkazi wa Uru, Moshi, kutosikilizwa

Ila dunia Ina watu katili kuliko hata shetani. Mtoto was miaka?!

Serikali inasubiri nini kufuta adhabu za viboko mashuleni?
 
Walimu tuache ukatili ,yaani mpk sasa kuna walimu wakatili mnooo
Fundisha ,rudi nyumbani subiri mshahara
Ukijifanya mpigaji utakutana nacho
 
pole sana mama Kwa kuondokewa na kijana wako. mpendwa ngoja tusubiri uchunguzi Uhuru...
 
Mwalimu yoyote akibainika kuanzia Leo anampiga viboko mtoto wa dalasa la Kwanza au la Pili ashtakiwe na ikibainika ametenda Hilo kosa na anyongwe tu.
Wananchi hatuna huruma naye tena.

Unakapigaje viboko katoto kadogo ka dalasa la Kwanza kenye miaka 6 ?
Kanaelewa nini.
Tumesha choka na ukatili wenu, na
Hili ni Onyo la Mwisho

Ulaya na Marekani watoto wa shule ya msingi hawapigwi kabisa na wanafulahia maisha ya shule.
Na wanafaulu vizuri masomo kushinda wa kwetu.

Kama Kuna walimu mabondia wenye hamu ya kupigana mjiandikishe, tukutane rasmi ulingoni.
Na sio kuvitesa vitoto vichanga.
 
Katika moja ya sababu itakayosababisha nije kuua mtu, ni kwa kosa la kumpiga mtoto wangu kwa namna iliyopitiliza, hata kama ni mama yake, sitajali..
 
Bahati mbaya wadau,hakuna mwalimu mwenye Nia ya kumuua mtoto. Mara ngapi watoto wanafia mikononi mwa wazazi?Ni bahati mbaya ndugu yangu,siamini kama yupo binadamu wa kunuwia kumuua mtoto
 
Back
Top Bottom