DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

DOKEZO Mwanangu ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inazungushwa

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Tatizo sio limempata nani? Suala ni uhalisia wa jambo husika. Je, ungekuwa wewe ni huyo Mwalimu unapewa tuhuma zisizo na uhalisia na kuhukumiwa na jamii ungejisikiaje?
Unajua hili suala hata mm linaniuma pande zote, iwapo mwalimu angekuwa ndugu yangu lazima ningekuwa katka kuomba yasimkute mabaya yoyote juu yake, hivyo hivyo huyo mtoto bila kuwa ngugu yangu inaniuma pia,
Ila wewe unashanikia kwa kusema eti mambo ya kizungu, hivyo kwako ni sahihi kabisa mtoto wa miaka saba kuchapwa kwasababu amechelewa namba? Dah!
Ndio maana watu wanasema kwasababu ya huyo mtoto hayajatokea kwako,
Mm simuhukumu mwalimu, na ninakuwa uoande wake kwasababu mtoto hatarudi, ila tuangalie namna ya kuwaadhibu watoto, mm nilisoma Shule ya Msingi kisutu, nikiwa darasa la Kwanza na la pili mwalimu wangu alikuwa Mrs Lukindo, ( muimba kwaya pale Azania Front) alitufanya kama watoto wake tu, hakuwa natumia vimbo bali anatugomveza tu na tunaogopa, 1979.
 
Naitwa Janeth Shayo, mkazi wa Uru, Moshi. Naomba unisaidie kupaza sauti mwanangu Jonathan Makanyaga (07) mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mrupanga, ameuawa kwa kupigwa na Mwalimu lakini kesi inataka kupindishwa.

Tar.28/02/2024 mwanangu alienda shuleni akiwa mzima. Alipofika aliadhibiwa kwa kuchelewa "namba". Alipoingia darasani alianza kutokwa damu puani na mdomoni. Akarudishwa nyumbani. Nilipomkagua nikamkuta na majeraha yaliyovilia damu mgongoni, kwenye mbavu na mguuni.

Kesho yake nikaenda nae shuleni kutaka kuoneshwa mwalimu aliyemfanyia ukatili mwanangu. Lakini Mwalimu mkuu akaomba nibaki nje. Akaingia na mwanangu ofisi ya walimu na kumtaka amtambue Mwalimu aliyemuadhibu. Mwanangu akamtanbua. Mwalimu Mkuu akaniambia wameshamfahamu ni mwalimu wa "Field" hivyo atazungumza nae.

Wakanipa 20,000/= za matibabu. Nikampeleka mwanangu zahanati. Kesho yake akazidi kutoka damu, na kulalamikia maumivu sehemu za mbavu. Nikampeleka hospitali ya masista. Daktari akaniambia bandama imejeruhika ndio sababu ya kutoka damu mdomoni. Mtoto alidai pamoja na viboko alivyochapwa, Mwalimu pia alimpiga ngumi tumboni. Huenda ndiyo iliyopasua bandama.

Hali yake ilizidi kuwa mbaya tukapewa rufaa kwenda KCMC. Akatakiwa kufanyiwa upasuaji. Gharama 350,000/= lakini sikuwa nayo. Nikapiga simu shuleni wakasema tuombe afanyiwe halafu watalipa baadae. Hata hivyo kabla hajafanyiwa hali yake ikazidi kuzorota, akashindwa kupumua, akawekwa kwenye Oxygen. Akashindwa kula, akawekewa mpira wa chakula. Baada ya siku chache akafariki 😭.

Lakini ripoti ya hospitali inasema mwanangu amekufa kwa kansa ya damu. Kansa gani ya damu inayomuua mtoto kwa wiki mbili? Na kwanini hiyo kansa itokee baada ya kuadhibiwa shuleni? Kwanini Mwalimu aliyemuadhibu mwanangu anafichwa, na sipewi haki ya kumfahamu?

Nalazimishwa nichukue maiti nikazike lakini nimekataa. Nataka uchunguzi huru. Nimeenda dawati la jinsia kulalamika nikapuuzwa. Nimepiga simu kwa Waziri Dkt. Gwajima D akanipa namba ya mtu wa kunisaidia. Nilipopiga kumbe ni yuleyule Mkuu wa dawati la jinsia aliyenipuuza. Nikamrudia Gwajima akasema niwasiliane nae huyohuyo. Nimekosa pa kulilia haki ya mwanangu Jonathan

Pia, Soma: Madai ya Janeth Shayo, Mkazi wa Uru, Moshi, kutosikilizwa
Inasikitisha sana, hawa walimu jamani
 
Bahati mbaya wadau,hakuna mwalimu mwenye Nia ya kumuua mtoto. Mara ngapi watoto wanafia mikononi mwa wazazi?Ni bahati mbaya ndugu yangu,siamini kama yupo binadamu wa kunuwia kumuua mtoto
Na yule aliyebaka mtoto kule Mara kisha akamnywesha sumu ili afe na ushahidi upotee hakuwa mwalimu? Kuwa makini na unachokisema
 
Bahati mbaya wadau,hakuna mwalimu mwenye Nia ya kumuua mtoto. Mara ngapi watoto wanafia mikononi mwa wazazi?Ni bahati mbaya ndugu yangu,siamini kama yupo binadamu wa kunuwia kumuua mtoto
Na yule aliyehukumiwa kunyongwa juzi juzi tu kwa kumpiga mwanafunzi hadi kumwua.

Kisa: kumsingizia kaiba pochi ya Mwalimu mwenzake wa kike.
Baadae huyo Mwalimu wa kike akaletewa pochi yake na bodaboda ambaye alipanda na kuisahau.

Hiyo kesi hukuisikia?
Jisemee nafsi yako ndugu, wako baadhi ya walimu ni chinjachinja kwa watoto wasio na hatia.

Tutaenda kuelewana tu hapo baadae kidogo na hawa wapumbavu wanaojiita walimu.
 
Bahati mbaya wadau,hakuna mwalimu mwenye Nia ya kumuua mtoto. Mara ngapi watoto wanafia mikononi mwa wazazi?Ni bahati mbaya ndugu yangu,siamini kama yupo binadamu wa kunuwia kumuua mtoto
Hapa nakubaliana na wewe,
Unajua una utoto mwingi? Mtoto mwenye kansa hawezi kupigwa kikatili? Tuseme tu alikuwa nayo hiyo kansa, inazuia vipi kupigwa? Hapa tunachojadili ni nini? Madai ya mtoto kupigwa. Umeshathibitisha kuwa mtoto hakupigwa kwa kiwango ambacho si sahihi?

Tena kupiga mtoto mgonjwa ilitakiwa ndo uwe aggressive zaidi kuwa kama alikuwa na kansa walimu hawakujua hali yake? Mzazi hakujua hali ya mtoto? Hiyo kansa ilijificha mpaka siku ya kipigo ndo iibuke kumuua? Ulipaswa kujiuliza maswali kabla ya kumtetea huyo mwalimu kuwa hausiki kabisa.

Hakuna mtu anataka mwalimu ahukumiwe bila makosa, ila tukio limetokea, kuna tuhuma, huwezi zipuuza tu bila kusikia upande wa mtuhumiwa.
Hapa ndipo nakubaliana na wewe

Hakuna mtu anataka mwalimu ahukumiwe bila makosa, ila tukio limetokea, kuna tuhuma, huwezi zipuuza tu bila kusikia upande wa mtuhumiwa.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Sorry madame mtoto wakati yupo hai hukumuuliza jina la mwalimu aliyempiga? Kama ulimuuliza unapata pa kumjua huyo muuaji. pole sana ndugu duniani saivi haki imepotea (alisema mdau mmoja wa JF saivi hakuna haki kuna sheria.
 
Kuna wavuta bange wanapewa cheo cha ualimu, na wengine stress za kukosa kizazi wanahamishia kwa watoto wa watu
Na yule aliyehukumiwa kunyongwa juzi juzi tu kwa kumpiga mwanafunzi hadi kumwua.

Kisa: kumsingizia kaiba pochi ya Mwalimu mwenzake wa kike.
Baadae huyo Mwalimu wa kike akaletewa pochi yake na bodaboda ambaye alipanda na kuisahau.

Hiyo kesi hukuisikia?
Jisemee nafsi yako ndugu, wako baadhi ya walimu ni chinjachinja kwa watoto wasio na hatia.

Tutaenda kuelewana tu hapo baadae kidogo na hawa wapumbavu wanaojiita walimu.
 
Kosa limeanza mwalimu wa field kupewa darasa la kwanza kufundisha. Watt wa darasa la kwanza wanataka walimu tena hasa wawe wa wamama wary wazima wenye huruma na upendo kwa wtt. Sasa mtt wa darasa la kwanza unamuachia mwalimu wa field kweli!!!? Ukute kaingia kwenye fani ya ualimu hio hana budi tu alimradi maisha yaende.
RIP mtt usie na hatia.
mama madhal umepaza sauti yako itasikika na haki yako utaipata very soon...Pole sn
 
Hapa nakubaliana na wewe,

Hapa ndipo nakubaliana na wewe

Hakuna mtu anataka mwalimu ahukumiwe bila makosa, ila tukio limetokea, kuna tuhuma, huwezi zipuuza tu bila kusikia upande wa mtuhumiwa.
Kabisa mkuu na limefanyika hilo. Wameshikiliwa na polisi.
 
Hii ya kupiga piga watto ovyo ni mbaya saa wegine wana ma sikoseli uko unamuua kizembe mtot wa watu, mi mtott namchapa makalio au mkononi tu basi na si ovyo ovyo
 
Na ukweli ni kuwa, hii Hadith imetungwa, hakunipigia na wala mm utaratibu wangu huwa siyo wa kuongea Bali SMS (kuandika ujumbe), tangu nitangaze simu. Kwenye mawasiliano yake na mm hakuna kitu kama hicho na yy anajua. Na kilichopo ni kuwa, watuhumiwa 5 wako ndani na Jeshi limethibitisha.

Kwa mema machache niliyofanya, yatakumbukwa baadae, nature ni nzuri, inatabia ya kukumbuka. Tuendelee kushirikiana [emoji1666]View attachment 2935519View attachment 2935520

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
Huenda pia kitete cha kufiwa aliongea na mtu sio sahihi akidhani ni wewe,,unaeza msaidia kutoka hapa kwenda mbele kuliko kukomalia alipiganau hakupiga
 
Huenda pia kitete cha kufiwa aliongea na mtu sio sahihi akidhani ni wewe,,unaeza msaidia kutoka hapa kwenda mbele kuliko kukomalia alipiganau hakupiga
Bahati nzuri huwa sina moyo wa kushikilia jambo, Nina moyo tu wa kuweka kumbukumbu sahihi. Tulishaenda mbele sisi na yeye zamani sana. Hii tu ilikuwa rejea ya kumbukumbu.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom