Mwanangu Ana E Zote na F 1 ya Hesabu, Je Anaweza Kupata Nafasi za Nursing?

SENGATI

Senior Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
127
Reaction score
26
mwanangu ana matokeo ya F4 ambapo amepata E zote na F moja, nataka nimpeleke nursing je ana sifa? naomba ushauri wenu wana jf........... mkoa wowote
 
Agh pole, ningekusaidia lakini mfumo wa sasahivi wa ufaulu hata mi siuelewi kabisa...!!i wa Hovyohovyo sana.
 
mwanangu ana matokeo ya F4 ambapo amepata E zote na F moja, nataka nimpeleke nursing je ana sifa? naomba ushauri wenu wana jf........... mkoa wowote

Hawezi kupata Nursing labda welding veta. Nursing inahitaji ufaulu. Hiyo ni sawa na Zero kwa maneno rahisi. Arudie mtihani au anza nae levels za chini za VETA alafu aendelee kujiongeza.
 
Sasa hapo si ana zero mwambie akalime kwa umesikia nursing ndo wanahitaji mazezeta.
 
mwanangu ana matokeo ya F4 ambapo amepata E zote na F moja, nataka nimpeleke nursing je ana sifa? naomba ushauri wenu wana jf........... mkoa wowote
UKIPATA F umefeli, pia ukipata E umefeli. kwa utaratibu wa sasa E na F zote zinamaanisha mwanafunzi amefeli, kwa maana hiyo mdogo wetu hajafaulu hata somo moja na hivyo hawezi kupata chochote kama ni kwa mfumo wa elimu. NDIO MAANA MIMI NILISEMA NI BORA WANGEANDIKA F tu badala ya E mana wanachanya watu. hiyo E haina msaada wowote. ila angepata D mbili hapo sawa.
 
kwa ufaulu huo atapata nafasi kwa nursing wa mirembe. nenda ka apply.
 
jamani taratibu na lugha zetu!
mwanao hawezi kupata nursing kwa alama hizo...labda veta.lakini kama yupo serious arudie mitihani yake,vinginevyo sijui.
 
Mmh, hebu hurumieni wagonjwa, huyu si atakuchoma fenegani badala ya PNV?

Bora aende u-polisi, akiwa trafiki, wampengie Tazara au moroco.

Si bora apatie route sasa!!!!!!
Atakutwikapo Quinine I/v push ukutwe na orbituary mapemaaaa!!!!!

Huyu nursing hapana kwa kweli akafanye mengine ya kipaji chake!!!!!
Muangalizie baking and decorations kama una mtaji akimaliza unamfungulia goli lake unamuunganisha na watu anafanya kazi zake for good!!!!!
 
Mpe nafasi nyingine,mrudishe form 2.maana naamin kiumri bado ni mdogo sana.kwa matokeo hayo,hawezi kuchaguliwa chuo chochote ndani ya mipaka ya tanzania.over
 
Aje hapa roman's college tunatoa kozi za nyingi lakini yeye atasoma
Nursery teaching na atapata cheti toka VETA.
kwa maelezo zaidi wasiliana na 0768298180
 
Mh jamani kwa matokeo ya mwanao yanatia Huruma kwa ushauri arudie mtihani ,mi ni mmoja wa waliofeligi kwa kupata four ya 30 ya mwaka 2006 nikarisiti 2007 na saba nikapata 3 ya 25 Leo hii nimeshamaliza chuo nimeshaajiriwa kwa vyeti vyangu visivyo na mawaa mwambie Mdogo wetu arudie maisha sio marahisi kwa matokeo yake haendi popote labda upishi
 
Ataua watu tu....
huyo mtafutie fani inayohitaji nguvu kuliko akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…