Mwanangu ananyonya sana!

Ntakasi

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2013
Posts
1,428
Reaction score
456
Hellow.....
Nina kabinti cha one week,nilijifungua week iliyopita....sasa since day one amekuwa ananyonya balaa....maziwa yalipochanganya akawa ananyonya mpaka yanakauka kisha anaanza kulia sababu hashibi....nakunywa uji wa pilipili manga like 24/7 na yanajaa kweli but hashibi....sasa naombeni ushauri kama kuna kitu cha ziada nifanye maziwa yamtoshe ......anything that can be helpful!

Thanks in advance,
Ntakasi.
 
Peleka huu uzi Jf Doctors utatendewa haki, nami ninakuja hukohuko kutoa mchango wangu,.
 
Una watu wazima waliokaribu nawe haswa wakina mama
Tafadhari tafuta hao alaka ili usipate michango ya kumpa mtoto maziwa ya kopo au kemikali nyengine
Mpende mwanao kama ulivyo pendwa wewe
 
Mimi ningekushauri ukazane hivyo hivyo kumnyonyesha bila kumpa kitu kingine.

Ongeza intake yako ya fluids and proteins ili maziwa yaongezeke.

Doctors hawashauri mtoto apewe chochote zaidi ya maziwa ya mama mpaka atakapo timiza miezi sita.

God Bless.
 
Una watu wazima waliokaribu nawe haswa wakina mama
Tafadhari tafuta hao alaka ili usipate michango ya kumpa mtoto maziwa ya kopo au kemikali nyengine
Mpende mwanao kama ulivyo pendwa wewe

Its not clear umemuambia nini.

Assuming umemshauri anyonyeshewe mtoto, wewe utampa mtoto mtu akunyonyeshee just like that?

Achilia mbali maradhi ya siku hizi, personal hygiene?

Sometimes tukitoa ushauri tuwe tunajiuliza what if ni sisi, tungefuata ushauri huo?
 
maziwa yako hayana virutubisho vyote .....mpe uji laini wamhogo
 
Una watu wazima waliokaribu nawe haswa wakina mama
Tafadhari tafuta hao alaka ili usipate michango ya kumpa mtoto maziwa ya kopo au kemikali nyengine
Mpende mwanao kama ulivyo pendwa wewe

Nipo na my mom nyumbani na wote tunajaribu kutafuta kitachowork huku tukiulizauliza kama hivi sababu tunakesha wote akicharuka usiku.....
 

Ahsante K But This Baby Ana Demand Aiseee....What Can I dDrink Precisely Kuincrease Hiyo Intake:..Any Sort Of Tea?
 
...pliz pliz pliz usimpe kitu chochote zaidi ya maziwa yako,jitahidi kula vizuri,mtori na vyakula laini ili maziwa yajae. Kamwe usimpe chakula chochote maana utamuathiri mtoto...
 
kula vyakula vya kuongeza maziwa uji mitori ili kuongeza maziwa mi sishauri uanze kumpa uji mlaini
 
Dadaa jitahidi,supu,mitori,ulezi sana......baada ya wiki 2/3 atakaa sawa,tena ushukuru km ana demand san,wangu wiki ya kwanza alikuwa hataki maziwa wala nini...full vingora acha tu!nilikonda mpk baba...ila kuna mwana bodi kakushauri jaribu kina mama watu wazima wanajua mambo mengi sana na yenye faida,uzungu uzungu wetu usitufanya tusahau we are Africans!
 
Pole kwa changamoto hiyo. Mimi nakushauri pamoja na juhudi zoote za kula vizuri,pia ongeza FREQUENCY na DURATION ya kumnyonyesha mwanao. Kwa sasa wewe ni mzazi,kazi yako ni kula na kunyonyesha. One single round isipungue 25minutes ataashiba tu,maana ukimtoa mapema anakuwa amepata yale wanaita FORE MILK ambayo hayana FAT. Nyonyesha hadi akamue HIND milk ambayo ni nzito na inaleta shibe. Kulea ni kazi mama. All da best.
 
Acha mama wa baadae anyonye atakavyo. kwani wewe unawania u miss ? Acha kijana afaidi hoteli ya bure.
 
Dah!
Wangu anakaribia kujifungua,nikiona thread za namna hii nabaki kusubiri tu nione kitakachonisibu na bibie.
MUNGU atusaidie.
Hongera sana kwa kujifungua salama.
 

Ndio kawaida ya watoto kunyonya. We mnyonyeshe tu kwani shida ipo wapi? Si upo likizo ya uzazi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…