Ntakasi
JF-Expert Member
- Oct 21, 2013
- 1,428
- 456
- Thread starter
-
- #41
Pretty bad advice.
Sio vizuri kumpa mtoto uji chini ya miezi sita.
Ntakasi hongera mwaya.
Ratiba yako ya kumnyonyesha ikoje?
Maziwa huwa yanajaa mpaka yanamwagika?
Kama huwa unampangia muda wa kunyonya (labda kila baada ya lisaa) usimpangie. Mnyonyeshe kila wakati ili maziwa nayo yaendelee kutengenezwa mwilini. Kama mama yako yupo kukusaidia that means unapata muda wa kutosha kupumzika. Utumie muda huo kukaa karibu na hako ka malaika, kakitaka nyonyo hata mara mia kwa siku we mpe.
Mwenyewe jitahidi kula vizuri mchanganyiko wa vyakula vyote na matunda. Usiishie kula vimiminika tu (uji/mtori/supu), hata kaugali/kawali laini na mboga nzuri ya majani+mchuzi ni nzuri sana. Utajisikia kushiba na maziwa mtoto atakayopata yatakuwa yanashika tumbo.
Ahsante Da Lizzy......Yanajaa wakati mwingine ila ananyonya sana hadi yanaisha kisha anaangua kilio....But..nitafuata ushauri wako.
Last edited by a moderator: