Mwanangu ananyonya sana!

Mwanangu ananyonya sana!

Pretty bad advice.
Sio vizuri kumpa mtoto uji chini ya miezi sita.

Ntakasi hongera mwaya.
Ratiba yako ya kumnyonyesha ikoje?
Maziwa huwa yanajaa mpaka yanamwagika?

Kama huwa unampangia muda wa kunyonya (labda kila baada ya lisaa) usimpangie. Mnyonyeshe kila wakati ili maziwa nayo yaendelee kutengenezwa mwilini. Kama mama yako yupo kukusaidia that means unapata muda wa kutosha kupumzika. Utumie muda huo kukaa karibu na hako ka malaika, kakitaka nyonyo hata mara mia kwa siku we mpe.

Mwenyewe jitahidi kula vizuri mchanganyiko wa vyakula vyote na matunda. Usiishie kula vimiminika tu (uji/mtori/supu), hata kaugali/kawali laini na mboga nzuri ya majani+mchuzi ni nzuri sana. Utajisikia kushiba na maziwa mtoto atakayopata yatakuwa yanashika tumbo.

Ahsante Da Lizzy......Yanajaa wakati mwingine ila ananyonya sana hadi yanaisha kisha anaangua kilio....But..nitafuata ushauri wako.
 
Last edited by a moderator:
Dadaa jitahidi,supu,mitori,ulezi sana......baada ya wiki 2/3 atakaa sawa,tena ushukuru km ana demand san,wangu wiki ya kwanza alikuwa hataki maziwa wala nini...full vingora acha tu!nilikonda mpk baba...ila kuna mwana bodi kakushauri jaribu kina mama watu wazima wanajua mambo mengi sana na yenye faida,uzungu uzungu wetu usitufanya tusahau we are Africans!

Ahsante kwa ku'share experience na ushauri mzuri...I needed to hear that...
 
Pole kwa changamoto hiyo. Mimi nakushauri pamoja na juhudi zoote za kula vizuri,pia ongeza FREQUENCY na DURATION ya kumnyonyesha mwanao. Kwa sasa wewe ni mzazi,kazi yako ni kula na kunyonyesha. One single round isipungue 25minutes ataashiba tu,maana ukimtoa mapema anakuwa amepata yale wanaita FORE MILK ambayo hayana FAT. Nyonyesha hadi akamue HIND milk ambayo ni nzito na inaleta shibe. Kulea ni kazi mama. All da best.

Ahsante sana kwa darasa....Ubarikiwe!!.
 
Kula kwa wingi nyanya chungu, na supu ya ngisi zinasaidia kuongeza maziwa ya Mama! Hakikisha mtoto hapewi chakula kingine, kwa umru wake huyo ni maziwa tu! Clinic utafundishwa zaidi
 
Dah!
Wangu anakaribia kujifungua,nikiona thread za namna hii nabaki kusubiri tu nione kitakachonisibu na bibie.
MUNGU atusaidie.
Hongera sana kwa kujifungua salama.

Ahsante Sana Na Mungu Awajalie,Ajifungue Salama.
 
Kama.mtoto mwanaume mara nyingi huwa wananyonya sana ingawa wapo na wakike pia hunyonya sana.

Kunywa uji wa mtama, asali na uwatu, pweza kwa wingi hasa supu yake au kamba pia wanafanyisha maziwa sana.

Hayo mapili pili manga usiyashiriki sana sio mazuri yasije yakakuletea madhara ya tumbo baadae

Ahsante sana kwa ushauri mzuri.
 
Kula kwa wingi nyanya chungu, na supu ya ngisi zinasaidia kuongeza maziwa ya Mama! Hakikisha mtoto hapewi chakula kingine, kwa umru wake huyo ni maziwa tu! Clinic utafundishwa zaidi

Ahsante Kwa Ushauri....
 
Mama jitahidi kula tu mie pia nanyonyesha binti yangu 1 month old sana nakula uji wa oats naweka na uwatu,supu ya pweza,ya kuku,kunywa maji mengi glasi 8-10 pumzika vizuri pia usijipe stress kuwa na wahka pia inapunguza uzalishaji wa maziwa...

Enjoy mama kunyonyesha raha sana jinsi unavyokuwa karibu zaidi na mtoto wako na yeye huongeza mapenzi zaidi

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
How wonderful!!.....Ahsante Sana Kwa Kunitia Moyo Na Ushauri Mzuri.
BTW,Nina Binti Pia!
 
How wonderful!!.....Ahsante Sana Kwa Kunitia Moyo Na Ushauri Mzuri.
BTW,Nina Binti Pia!

Owh wow...usijali karibu sana

Hongera sana na pole kwa safar ndefu kwa kweli ni mbali sana

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Halafu ngoja nikuambie kitu @Ntakasi. How you hold your breast matters. Isije kuwa mtoto ananyonya hewa tu.The image below shows you how the breast should be held while breast feeding
.View attachment 150613
Usiweke kidole juu ya nipple asi if nipple iwe katikati ya index na middle finger. Utakuwa unalimit flow ya maziwa na mtoto atanyonya hewa.

Hii apa muhimu me pia nlikua nakosea kumnyonyesha bahati nzuri walinipeleka darasa maalum kuhusu kunyonyesha na kila kitu ila nlikua nimechoka full kusinzia

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Ama inawezekana maziwa yako ni madogo. Kunywa maji mengi sana. Usimnyime maziwa.

Sent from Samsung Note III using Tapatalk
 
Water water and more water.

You don't have to take gulps, just stay hydrated and drink more.

Soups too, milk, I wouldn't advise teas. I cut back on caffeine from pregnancy mpaka mtoto alipofika 6 months.

Hata ule nini but without fluids basically water you won't make milk.

Halafu ngoja nikuambia mwili wako hauwezi kulemewa na kumlisha mtoto umembeba for 40 weeks. Keep pumping to produce more milk.

Do you have an idea what am talking about?

I understand Da' K.....I think i need to learn a great deal of nursing and stuffs....nursing is not as simple as i once thought......Gotta work some nerves...lolz....Thanks Much!
 
Halafu ngoja nikuambie kitu @Ntakasi. How you hold your breast matters. Isije kuwa mtoto ananyonya hewa tu.The image below shows you how the breast should be held while breast feeding
.View attachment 150613
Usiweke kidole juu ya nipple asi if nipple iwe katikati ya index na middle finger. Utakuwa unalimit flow ya maziwa na mtoto atanyonya hewa.

This is very helpful!
 
Make sure mtoto ananyonya ziwa moja for not less than ten minutes. This is because mother's milk constitutes of two parts.

Maziwa yanayotoka mwanzo pale unapo breast feed ni maji mostly kwa ajili ya ku quench kiu cha mtoto. Yanayofuata ni mainly fats kwa ajili ya kurutubisha mwili so make sure the baby suckles long enough on one breast. Burp him- atoe hewa then akiwa bado anataka kunyonya move him/ her to the next breast.

Umenikumbusha mbali aisee.

Na mvua hizi ngoja nitage ka second born fasta. lol

HeeeHeee....WishIng You The Best!
 
Back
Top Bottom