Fanya hivi, anza. Kuweka akiba nono kabisa. Kama unataka asome sehemu nzuri na awe rubani wa ndege za biashara andaa angalau 200M.
Amani iwe nanyi want JF..
Naomba kueleweshwa nifanyeje ili kijana apate mafunzo ya urubani.Nasikia gharama ni kubwa sana.. je pana uwezekano wa kupata ufadhili wa serikali au shirika lolote ili kijana huyu afikie ndoto yake?
Tafadhalini naomba ushauri.. Natanguliza shukurani zangu zamdhati.
Nasikia si wana jenga chuo cha urubani kilimanjaro
200M halafu atakuja kulipwa mshahara wa kiasi gani?
Mosswood wanafundisha PPL ni 17000USD kama 36000000 hivi
Ukitoka hapo unasomea CPL ili uweze endesha hizi Taxi za Mbugani
Baada ya hapo ndo sasa akajitose nje kusomea zaidi kama ni ATR au Bombadier
Wengi husomea ndege kutokana na zilizopo kwenye mashirika yaliyo nchini kwao
Asante kwa taarifa hii mkuu. Je, kuna uwezekano wa sponsorship au loan kwa makubaliano mahsus?
Usajili unafanyikia Wizara ya mawasiliano ?