Mwanangu haongei vizuri

steveslove

Senior Member
Joined
Jul 18, 2012
Posts
110
Reaction score
32
Nina mtoto ana miaka mitatu sasa bado hajajua kuongea vizuri nishampeleka hospitali kwa uchunguzi hakuonekana na tatizo ila matamshi yake yananipa utata sana anapotaka kusema bye anasema tai, suprise anasema tataizii anapohitaji kitu hawezi sema anaonyesha ishara au anakuchukua mpaka kwenye anachohitaji. Pia anaposikia mwimbo anaoupenda anaimba bila maneno anafatisha tu ule mwimbo lalalalla au oooooo.

Chakushangaza mengine anatamka like maneno see u yeye atakwambia chi u. Kuna waliosema simchanganyi sana na watoto wenzake but kiukweli huwa anacheza na wenzie na yupo na kaka yake ambaye ni muongeaji sana, wanacheza na wanaelewana ila mwenzio haongei maneno yanayoeleweka.

Je, atakuja kuongea mana miaka mitatu sasa, au daktari gani mwingine bingwa wa watoto mniambie nimtafute najiskia vibaya mwanangu kuwa hivi please nisaidieni:A S cry:
 
tatizo ni kuwa mmemfungia sana ndani hakucheza na watoto wenzie .Kukaa na kaka yake sio suluhu kaka yake anaweza akawa anawaza facebook au whatsupp akamwacha kule .mchanganye na watoto wenzake uone within two week atakuwa anaongea kama cherehani.
 
tatizo ni kuwa mmemfungia sana ndani hakucheza na watoto wenzie .Kukaa na kaka yake sio suluhu kaka yake anaweza akawa anawaza facebook au whatsupp akamwacha kule .mchanganye na watoto wenzake uone within two week atakuwa anaongea kama cherehani.

kaka yake hawezi kuwaza fb he is 7 so bado wanacheza pamoja n they real play all the time, nje anakaa ila haongeagi anacheza bt he doesn't improve
 
mkuu wangekuwepo watatu ingekuwa poa ina maanisha wewe watoto wingine wawili mkuu dada yangu alishapata hili tatizo pia yeye alichokifanya alimpeleka mtoto kwa bibi(mama) huko kijiji hii ni kutokana na yeye kuwa anachelewa kurudi kazini si unajua na foleni dar at the end of two month mtoto alikuwa na matokeo mazuri baada ya kukutana na changanyikeni huko kijijini.
kaka yake hawezi kuwaza fb he is 7 so bado wanacheza pamoja n they real play all the time, nje anakaa ila haongeagi anacheza bt he doesn't improve
 

Asante kwa ushauri kama kumchanganya ni solution i think ni better nimpeleke shule kuliko kumpeleka mbali na mie kiukweli i cnt. I will take him to school instead naamini kama ni kumchanganya zaidi then school is the best, thanks :redface:
 
kuna watoto huwa wanachelewa sana kuongea na wengine huwahi, me nazani huyo wako kachelewa tu
 
Tatizo sometymes ni meno kujaa mdomoni sasa nafasi ya ulimi kucheza inakuwa ngumu..jaribu kumuona daktari wa meno kwa ushauri zaidi..
 
Ni mtoto wa jinsia gani?
Kama ni mvulana mbona ni kawaida sana, watoto wa kiume huchelewa kujua kuongea. Mtoto wangu wa kike alipokuwa na umri wa miaka 4 alikuwa naongea vizuri kabisa lakini mtoto wangu wa kiume now ana miaka 4, anaongea lakini kuna baadhi ya maneno bado hajajua kuyatamka vizuri. Lakini pia kama mchangiaji mmoja alivyosema hapo juu, mwachie time acheze na wenzake huko atajifunza maneno mapya au ikibidi mpeleke kindergarten itamsaidia
 
Kama hana tatizo lolote (frenulum) basi ataongea tu sababu milestone kuna baadhi ya watoto wanakuwa tofauti!!!!

Ushauri wa wadau hapo kuwa anahitaji kukutana na watu/watoto mchanganyiko ni zuri lifanyie kazi!!!!
 
Naomba niwe tofauti kidogo na wachangiaji wengi. Ulimnyonyesha kwa mda gani?
Naanzia hapo
 
Naomba niwe tofauti kidogo na wachangiaji wengi. Ulimnyonyesha kwa mda gani?
Naanzia hapo

nashukuru kwakua na wazo kama langu..nlitaka kumuuliza kama alimkatisha nyonyo mapema au ana ujauzito?
 
Gap kati ya mtoto wa miaka 7 na miaka 3 ni kubwa sana kwa mtoto. Miaka 7 anajiona ni mkubwa kwa mdogo wake (hata interest zinatofautiana sana) hivyo hawezi kumchangamsha kama ambavyo unadhani anaweza. Kama hamna watoto wengine karibu (3-5yrs) mpeleke day care akachangamshwe na wenzie. Alafu tumia muda mwingi kuongea nae, msemeshe, msikilize na akipatia kitu msifie. Watoto ni wepesi kujifunza haswa anapojua mnamfurahia akijua kitu.

ram sio watoto wote wa kiume wanachelewa bana. Wangu wa miazi 15 ameshajua maneno kibao, mpaka twende nje
(ende nje) anasema. Watoto wanachelewe kutembea/kuongea kwasababu wazazi hawana muda wa kutosha kuwa nao. Ukiwa na muda wa kutosha na mwanao pia usipomlimit (sijui chini ya miezi sita asikae ataumia, kumbeba beba kila saa ndio vitu vinavyolemaza watoto.) mbona atakuwa kama mashine.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: ram
mimi ni audiologist, kwa uzoefu wangu mwanao ana speech disoder, angekuwa hasikii na haongei(bubu) ningekushauri ila kwa tatizo la mwanao speech organ zake ni nzito, mpeleke CCBRT Kuna speech therapist watakusaidia kumuintervene, kwani umefanya jambo la maana kudiscaver mapema tatizo la mwanao. wazazi tusifiche ulemauvu wa watoto kwa wao pia wanaweza.
 

Interesting!!!!!!
Hebu funguka zaid mkuu kwa faida y jamvi
 
tunakungoja mtoa maada kujua umeshapata ufumbuzi wa mtoto wetu??,kama laa fuata maelekezo niliyokupa hapo juu
 
Nimekupata mamaaa kubwa
But ile hadithi yetu ya zawadi iliishiaga wapi mamito?


 
Last edited by a moderator:
Ni kawaida sana. Ataongea tu wala huna haja ya kupoteza muda wako kutafuta daktari. Mtoto wa rafiki yangu alianza kutamka maneno vizuri baada ya kufikisha miaka 6, na sasa anasoma darasa la tano, anaongea vizuri kabisa!
 

he is a boy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…