Mwanangu hawezi kukaa na ana miezi mitano

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Ma-Dr. Nina mtoto wa kike ana miezi mitano ila kila akikalishwa huwa hawezi kaa. Naomba mnijuze mtoto inabidi aanze kukaa akiwa na umri gani, na kama ndani ya umri huo hajaanza kukaa tatizo linakuwa ni nini?

Natanguliza shukrani
 
Ma-Dr. Nina mtoto wa kike ana miezi mitano. ila kila akikalishwa huwa hawezi kaa. naomba mnijuze mtoto inabidi aanze kukaa akiwa na umri gani, na kama ndani ya umri huo hajaanza kukaa tatizo linakuwa ni nini? natanguliza shukrani

bado hajakaza akikaza atakaa.
acheni kumlazimisha mtoto hukua kulingana na Mungu anavyomjalia, so far bado mdogo sana na wala haihitajiki kumlazimisha kukaa yeye mwenyewe ataanza kutaman kukaa na atajiinua.
 
Usimlazimishe kukaa akiwa tayari atakaa mwenyewe...wewe unaweza kumfanyia mazoezi ukae nae lkn atakaa mwenyewe baada ya muda..ni kawaida kwa watoto wengine kuchelewa kukaa nakumbuka iuna mtoto wa rafiki yangu kakaa akiwa na miezi 6 au 7 na akaanza kutambaa hapohapo pia....kama umeshaanza kumuonjesha vyakula vya watoto unaweza umkalishe kwenye kiti cha watoto kama hiki itamsaidia akazane haraka!
 
Angalia usiwe umemuaribu mtoto na michepuko.atamaliza miez kumi bado ajakaa.kama ujafanya hivyo muache soon atakaa na kutambaa kwa pamoja
 
Sidhani kama ni tatizo. Kuna wengine katika ukuaji wao huruka baadhi ya stage. Mfano, mimi mtoto wangu hakutambaa but alianza kutembea. So usiwe na hofu.
 
Usiwe na haraka akiwa tayar mwenyewe atakaa miezi 5 bado hajachelewa..
 
Reactions: BAK
usihofu wangu alichelewa kama Huyo ila alipokaa weekiliyofuata alisimama na vitu hakutambaa kabisa.
nakushauri usimvalishe nepi nzito au pampas mchana kama anamwili mkubwakidogo mvalishe chupi au suruali tuu ili awe flexible
 
Mbona wangu alianza kukaa na miezi saba?? Acha wasiwasi,anza kumkalisha taratibu,atazoea
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…