Mabula marko
Member
- Jul 18, 2022
- 44
- 38
Mwanangu, mafanikio yako utayapata Kwa juhudi
Utangulizi
Siku zote, mafanikio hayaji kwa bahati mbaya. Lazima uwe na juhudi, bidii na uvumilivu ili kufikia malengo yako na kuzishinda changamoto zote unakutana nazo katika maisha basi nasi kama taifa la Tanzania , nchi na wananchi wake hatuna budi kuwajibika kila mtu katika nafasi yake kwa usahihi na kwa bidii tuzishinde changamoto zinazoikumba nchi yetu na wananchi wake ambazo nyingi zi katika uwezo wetu mwalimu awajibike ipasavyo , mkulima alime kwa weledi kwa utumia hizi hizi rasimali za wataalamu tulio nao itatusaidia kupunguza kilio cha njaa kwa taifa madaktari pia wawajibike kwa ufasaha tutaondoa ama kupunguza vifo vitokanavyo na uzembe , mfugaji afuge kwa umakini ili kupunguza vurugu na magovi kati yake na wakulima mhandisi awajibike tupate barabara na majengo bora na kadharika daima kama nchi na taifa kwa ujumla tutapiga hatua kubwa na kufanikiwa katika Nyanja zote .
Hii ni hadithi ya mwanangu, ambaye alipitia changamoto nyingi katika maisha yake lakini alifanikiwa kwa sababu ya juhudi zake, hadithi hii nimeifananisha na wananchi wote wa Tanzania ambao hasa ndiyo watoto wa Tanzania ikiwa Tanzania ndiyo mzazi wetu akisimulia hadithi ya mwanae huku akituasa tukiyazigatia haya tunayoenda kujifunza na kila mtu akatimiza wajibu wake basi hadithii itachochea uwajibikaji na kupunguza lawama kwa serikali hata zile zilizo wajibu wetu.
Hadithi.
Mwanangu alizaliwa katika familia maskini. Walikuwa wanaishi kwenye kijiji kidogo katika mkoa wa Mbeya. Walikuwa na shida nyingi, ikiwa ni pamoja na kukosa chakula cha kutosha, maji safi na elimu bora, barabara na maradhi yalikuwa sehemu ya maisha yao. Hata hivyo, mwanangu alikuwa na ndoto kubwa za kufanikiwa maishani aliamini kila kitu kinawezekana .
Alipokuwa mdogo, alikuwa na hamu kubwa ya kusoma. Hata kama wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumlipia masomo, alijitahidi kujifunza kwa bidii. Alisoma vitabu vya shule vilivyotupwa na wanafunzi wengine na alifanya kazi za majumbani na kulima vibarua ili aweze kupata pesa za kusaidia kujilipia masomo yake lakini kuwasaidia wazazi wake walau wapate cha kuweka kinywani.
Mwanangu alikuwa na uwezo mkubwa wa kusoma na kuandika, na hii ilimsaidia kupata fursa ya kupata ufadhili wa masomo. Alisoma kwa bidii na akafaulu vizuri katika mitihani yake. Hata hivyo, alikumbana na changamoto nyingine wakati wa kusoma chuo kikuu.
Alikuwa na matatizo ya kifedha na alikuwa na wasiwasi juu ya mustakabali wake.Lakini mwanangu hakukata tamaa. Aliendelea kusoma kwa bidii na kufanya kazi za ziada ili kujipatia pesa za kuendesha maisha yake. Alifanya kazi za kusafisha ofisi, kuuza vitabu na hata kufundisha watoto wadogo. Alifanya kila kitu kwa bidii na uvumilivu ili kufikia malengo yake.
Mwishowe, mwanangu alifanikiwa. Alipata kazi nzuri na sasa anaishi maisha mazuri. Hata hivyo, alijifunza kitu muhimu katika safari yake ya mafanikio - kwamba mafanikio hayaji kwa bahati mbaya. Lazima uwe na juhudi, bidii na uvumilivu ili kufikia malengo yako.Katika jamii yetu ya Kitanzania, kuna mengi ya kufanya ili kufikia utawala bora na uwajibikaji.
Kuna matatizo mengi, ikiwa ni pamoja na rushwa, ukosefu wa ajira na huduma duni za afya na elimu. Lakini hatupaswi kulaumu viongozi wetu peke yao. Lazima tuchukue jukumu letu kama raia wa Tanzania na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yetu.
Kama mwanangu, tunapaswa kujifunza kutokana na changamoto zetu na kuendelea kusonga mbele kwa bidii na uvumilivu. Kwa pamoja, tunaweza kufikia malengo yetu na kujenga taifa letu kwa utawala bora na uwajibikaji ama kweli tusipo simama katika mstali wa kuzikabili chnagamoto tutaendelea kuilaumu serikali ikiwa mengine ni wajibu wetu kwa mfano mtu kujenga bondeni alafu baadae akutwe na mafuriko nae analaumu serikali na viongozi kumbe ni swala lake kutimiza wajibu.
Mtu anakosa chakula hajalima au aliuza akiba yote analaumu serikali na viongozi , tukubali kuwa kila mtu afanye jukumu lake kwa ufasaha naamini yale yote tunayoyapigia kelele yataisha na kama taifa tutasonga mbele mwanasiasa atomize wajibu wake kwa juhudi na kwa bidii , mwalimu afanye kazi yake kwa ufasaha , serikali na viongozi wake watimize wajibu wao kama taifa tutasonga mbele na kutimiza ndoto iliyo ya watanzania wengi walioota maisha mazuri kama mwanagu.
Hitimisho
Hadithi hii ya mwanangu iwe chachu kwa watanzania wote na taasisi zake natamani kuona taasisi za elimu ya juu zikitoa nafasi kwenye ratiba zao za vipindi nafasi za wanafunzi wao kutafuta kazi za muda(part time jobs)kwa kufanya hivo vijana watahimili ukosefu wa fedha za ufadhili wa serikali kama alivyokuwa akifanya mwanangu , pia natamani kuona wataalamu wa afya hawa wachache na teknolojia yetu hii kwenye sekta hii ikiwajibika vizuri itasaidia kuwalinda watanzania wawe na afya njema , wafanyakazi na wafanya biashara walipe kodi kama mwanangu alivyokuwa akiwakumbuka wazazi wake ili waweze kupata mkate wao wa kila siku kumbe kila mtu afanye kila kitu kwa juhudi na kwa bidii na kwa uvumilvu walimu , wakulima , wafugaji na kila mtu katika nafasi yake afanye kwa bidii hakika kama mwanangu tutafanikiwa na hatimaye tutasimama katika uwajibikaji na utawala bora.

Upvote
11